Ushauri kwa watu wa mkoani wanaoishi Dar: Pangeni mjini na nje ya mji

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,120
27,126
Mwaka 2020 jirani yangu alifukuzwa na mama mwenye nyumba wake (muhaya) usiku.

Alikuwa na mke na watoto watatu. Hakuwa na pa kwenda. Kwa kuwa alikuwa na mazoea na Mimi (tulikuwa tunakunywa wote plus wote Yanga) akaja kuomba msaada kwangu.

Msaada nilio mpa:

1. Nilimpa Hifadhi yeye na familia yake nyumbani kwangu kwa usiku huo.

2. Kesho yake nikamshauri apange nyumba nje ya mji huku anajiandaa kutafuta sehemu ya kuishi. Kwa kuanzia nikamwambia shambani kwangu homboza(ipo mbele ya chanika) kuna nafasi ambayo ninaweza kumpangisha kwa bei ya chini sana. Anaweza kuanza na kodi ya miezi mitatu akaiweka familia yake huko huku akiendelea kupambana (homboza ni gari moja hadi kariakoo).

Kweli jamaa akaenda homboza akapapenda sana baada ya wiki tatu akanilipa kodi ya miezi Sita kabisa. Wiki moja baadae akaja tena mjini akapanga sehemu nyingine. Kule kijijini hakuachia nyumba,alimtoa mdogo wake kwao Mwanza then kumuweka huko shamba homboza akaanzisha kamradi mdogo wake akawa anasimamia.

Fast forward: Jamaa sasa hivi ameshakamilisha nyumba yake homboza (alinunua eneo huko)

Akapanga mjini kwake ni Homboza. Anajua hata alifukuzwa kodi anapanda gari moja tu hadi homboza amefika tofauti n.a. kwenda kusimangwa kwa ndugu au kurudi kwao mwanza.

Anasema sasa hivi ameamua kuwa kama Seyyid Said anahamisha mwanao makuu ya familia yake kutoka Mwanza hadi Homboza.

Anakaa mjini kwa sababu ya:

1. Ukaribu na ofisi yake.

2. Ukaribu na shule nzuri wanazosoma watoto wake.

Ushauri kwa watu wa mkoani wanao Anza maisha Dar.

Kama huna uhakika na hela ya kodi katika sehemu unayo kaa nakushauri tafuta chumba au nyumba ya ziada nje ya mji(kama vipi nenda hata kisarawe maneromango huko)

Siku ukikwama mjini unakimbia zako shamba kuliko kuadhirika mjini na watoto wako..

#having one hoe is close to having no hoe.

# hakunaga kitu kimoja kimoja hata kwenye mwili wako Mungu ameumba vitu viwili viwili. Mikono miwili, tundu za pua mbili, macho mawili, miguu miwili etc
 
Ushauri mzuri, ila ukiangalia gharama za usafiri na muds unaotumia kutoka huko Homboza hadi kazini(town) hazipishani sana na aliyepanga town. Advantage kubwa ni fursa za viwanja, mashamba na kilimo huko shamba anapokaa.
Ukizoea ni kawaida tu plus chumba cha shamba kinakuwa chumba chako cha ziada in case ukipata matatizo mjini
 
Ushauri mzuri, ila ukiangalia gharama za usafiri na muds unaotumia kutoka huko Homboza hadi kazini(town) hazipishani sana na aliyepanga town. Advantage kubwa ni fursa za viwanja, mashamba na kilimo huko shamba anapokaa.
Mwenye nyumba siku zote anataka Kodi ya mkupuo miezi 6, akipanga nje ya mji anapata muda wa kujipanga na ndio maana hata jamaa alipojenga bado alipanga mjini kwa ukaribu wa ofisi yake na shule za watoto wake.
 
Mwaka 2020 jirani yangu alifukuzwa na mama mwenye nyumba wake (muhaya) usiku.

Alikuwa na mke na watoto watatu. Hakuwa na pa kwenda. Kwa kuwa alikuwa na mazoea na Mimi (tulikuwa tunakunywa wote plus wote Yanga) akaja kuomba msaada kwangu.

Msaada nilio mpa:

1. Nilimpa Hifadhi yeye na familia yake nyumbani kwangu kwa usiku huo.

2. Kesho yake nikamshauri apange nyumba nje ya mji huku anajiandaa kutafuta sehemu ya kuishi. Kwa kuanzia nikamwambia shambani kwangu homboza(ipo mbele ya chanika) kuna nafasi ambayo ninaweza kumpangisha kwa bei ya chini sana. Anaweza kuanza na kodi ya miezi mitatu akaiweka familia yake huko huku akiendelea kupambana (homboza ni gari moja hadi kariakoo).

Kweli jamaa akaenda homboza akapapenda sana baada ya wiki tatu akanilipa kodi ya miezi Sita kabisa. Wiki moja baadae akaja tena mjini akapanga sehemu nyingine. Kule kijijini hakuachia nyumba,alimtoa mdogo wake kwao Mwanza then kumuweka huko shamba homboza akaanzisha kamradi mdogo wake akawa anasimamia.

Fast forward: Jamaa sasa hivi ameshakamilisha nyumba yake homboza (alinunua eneo huko)

Akapanga mjini kwake ni Homboza. Anajua hata alifukuzwa kodi anapanda gari moja tu hadi homboza amefika tofauti n.a. kwenda kusimangwa kwa ndugu au kurudi kwao mwanza.

Anasema sasa hivi ameamua kuwa kama Seyyid Said anahamisha mwanao makuu ya familia yake kutoka Mwanza hadi Homboza.

Anakaa mjini kwa sababu ya:

1. Ukaribu na ofisi yake.

2. Ukaribu na shule nzuri wanazosoma watoto wake.

Ushauri kwa watu wa mkoani wanao Anza maisha Dar.

Kama huna uhakika na hela ya kodi katika sehemu unayo kaa nakushauri tafuta chumba au nyumba ya ziada nje ya mji(kama vipi nenda hata kisarawe maneromango huko)

Siku ukikwama mjini unakimbia zako shamba kuliko kuadhirika mjini na watoto wako..

#having one hoe is close to having no hoe.

# hakunaga kitu kimoja kimoja hata kwenye mwili wako Mungu ameumba vitu viwili viwili. Mikono miwili, tundu za pua mbili, macho mawili, miguu miwili etc
Ushauri ambao unafaa pia wanunue viwanja, wasiangalie ubaya wa eneo. Cha muhimu eneo liwe legitimate. Kinyerezi na Goba miaka kumi na tano iliyopita yalikuwa mapori. Lakini leo viwanja havishikiki.
 
Sahihi
 
Back
Top Bottom