kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 8,992
- 17,892
Sisi wanaume huwa hatuzingatii haya ila ni muhimu sana wewe na mke wako mkaishi kwa upendo na hawa mabinti wa kazi mfano:-
Wape mshahara kwa wakati
Kuepuka kuwapiga kuwafokea au kuwatisha wanapofanya kazi. Watreat sawa na unavyotreat familia yako kuanzia chakula malazi afya nk
Wapewe muda wa kupumzika wa kutosha saa zingine ukiona kafanya kazi sana mstopishe aache apumzike mimi na mke wangu tuna kanuni moja tulishampiga marufuku kufanya kazi kupitiliza na kulala lazima alale muda wa kutosha na nikinunuaga zawadi za sikukuu au vizawadi au vitu vidogo vidogo nyumbani nikigawa lazima na yeye nimjuishie huko na huwa sina ubaguzi wowote kila kitu nacholeta kwa ajili ya watoto na yeye namletea
Kama nyumbani wife na watoto wapo na ni wa wakubwa kiasi au wanafamilia wapo basi kazi nyingine wazifanye wenyewe tu au wamsaidie dada wa kazi sio kila kazi anaachiwa dada wa kazi.
Wapewe uhuru kwa namna inayofaa, kuna nyumba nyingine dada wa kazi haruhusiwi kushika simu au kuwa na simu yaani eti akitaka kuwasiliana na ndugu hadi aombe simu ya mwajiri wake huu sio utu hata kidogo.
Wengine wanawazuia wasifate imani yao mfano housegirl muislam anazuiwa kwenda msikitini au kuswali akiwa kwa mkristo au housegirl mkristo anazuiwa kwenda kanisani au kwenye maombi akiwa kwa muislam. Sasa mnamzuia mtu na imani yake ili iweje jee unapata nini kumzuia? Akikufuata kiimani utafaidi nini? Au utakua tajiri?
Au ndo utaenda peponi/mbinguni? Mimi dini ya mtu inanihusu nini? Hata kama angekuwa anaabudu ng'ombe fresh tu ndo imani yake. Mimi kwangu ni waislam dada wa kazi ni imani tofauti na yetu lakini tumempa uhuru wa kuabudu atakavyo jumapili ikifika anafanya kazi chache mnoo ni siku yake ya kwenda kuabudu siku hiyo kazi nyingi anafanyaga wife tu.
Kikubwa ni kuwapa usawa tu kama ilivyo kwa wanao mkeo au wanafamilia wengine ukifanya hivi hakika utakua na familia yenye furaha na amani kwasababu hawa dada wa kazi aka beki tatu mara nyingi ndo wanashinda majumbani na kuangalia familia kwenye kila kitu.