Ushauri: Ndugu wameharibu ndoa ya dada yangu

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,638
99,753
Wakuu,

Mwezi Mei mwaka jana, kuna dada yangu mmoja aligombana na mumewe na kukimbilia kwangu. Nilipoongea na mumewe, akasema yeye hana tatizo nae, arudi tu wayamalize.

Nilipomsihi dada arudi wakayamalize, akawa hataki, anang'ang'ania aendelee kuishi kwangu tu. Nikaamua kumfukuza aondoke, kwangu sina nafasi ya kuhifadhi mke wa mtu mimi.

Kumbe alivotoka kwangu akahamia kwa ndugu wengine wakampokea akaishi. Nikawa naskia tu, sasa dada anakaa kwa ndugu flani, mara kahamia kwa ndugu mwingine, kwa mumewe kagoma kabisa kurudi.

Nimewasihi ndugu zangu sio vizuri kukaa na mke wa mtu majumbani kwenu, hawataki kunielewa, wanadai namtetea sana mume wa dada yangu, nataka mpk afe ndo nijue mumewe ni mnyanyasaji wa kijinsia.

Wakasema kama mumewe anamtaka mkewe basi amfate mwnyw ukweni na akaiombe radhi familia, vinginevyo asahau kabisa kama alishawai kumuoa ndugu yao. Nikaamua kujiweka kando na hayo mambo.

Amekuja kurudi kwa mumewe mwezi huu tar 02 (miezi 11 imepita) akiwa na mimba ya kubwa sana. Mumewe kagoma kabisa kumpokea akidai mkewe aliondoka akiwa hana mimba, inakuaje arud kwake akiwa na mimba? Hiyo mimba sio yake.

Nmemhoji dada yangu, anadai ile mimba ni ya mumewe 100% na aliondoka nayo, ila alishindwa kumtaarifu mumewe kutokana na ugomvi uliokuepo kati yao.

Ndugu waliomhifadhi miezi yote hiyo wananipigia kunisihi niongee na shemeji yangu, ampokee mkewe maana ni mjamzito sana anaweza kujifungua muda wowote. Nimewaambia hiyo kazi siifanyi, fanyeni nyie wenyewe mlioyasababisha. Wanadai jamaa hawezi kuwaelewa, walishagombana tayari na hawapokelei kabisa simu zao.

Nmemtafuta shemeji, anachosema ni kwamba, kama kweli mkewe aliondoka na mimba yake ile mwezi Mei mwaka jana walipogombana, basi mwaka huu mwezi January au February alitakiwa awe tayari keshajifungua mtoto.

Sasa hivi ni mwezi March, ni miezi 11 tangu mkewe aondoke bado ni mjamzito hajajifungua, hivyo kwa vyovyote vile ile mimba sio yake. Kaipatia huko huko kwa ndugu zake na kwa tafsiri hiyo, hamna ndoa tena hapa.

Kiukweli mpaka sasa kichwa kimepata moto, sielewi nifanye nini dada yangu akae sawa maana analia muda wote (na hii mimba alionayo nahisi itamletea shida au huenda akajidhuru).

Pia nishauri nini kifayike ikiwezekana arudiane na mumewe, maana jamaa hataki hata kumskia mkewe wala habari zake na kahama kabisa pale nyumbani, kaenda kupanga sehemu nyumba nyingine kabisa.

Nawasilisha. 🙏
 
Wakuu,
Mwezi MEI Mwaka Jana Kuna dada yangu mmoja aligombana na Mumewe na kukimbilia kwangu, Nilipoongea na Mumewe, Akasema yeye Hana tatzo nae, arudi TU wayamalize.

Nilipomsihi dada arudi wakayamalize, akawa hataki, anang'ang'ania aendelee kuishi kwangu tu. Nikaamua kumfukuza aondoke, kwangu Sina nafasi ya kuhifadhi MKE wa mtu mimi.

Kumbe alivotoka kwangu akahamia kwa ndugu wengine wakampokea akaishi. Nikawa naskia TU, sahv dada anakaa kwa ndugu flani, Mara kahamia kwa ndugu mwingine, kwa mumewe kagoma kabisa kurudi.

Nmewasihi ndugu zangu sio vzur kukaa na MKE wa mtu majumbani kwenu, hawataki kunielewa, wanadai namtetea Sana mume wa dada yangu, nataka mpk afe ndo nijue mumewe Ni mnyanyasaji wa kijinsia.

Wakasema Kama mumewe anamtaka mkewe Basi amfate mwnyw ukweni na akaiombe radhi familia, vinginevyo asahau kabisa Kama alishawai kumuoa ndugu Yao. Nikaamua kujiweka kando na hayo Mambo.

Amekuja kurudi kwa mumewe mwezi huu tar 02 (miez 11 imepita) akiwa na mimba ya kubwa Sana. Mumewe kagoma kabisa kumpokea akidai mkewe aliondoka akiwa Hana mimba, inakuaje arud kwake akiwa na mimba?. Hiyo mimba sio Yake.

Nmemhoji dada yangu, anadai Ile mimba Ni ya mumewe 100% na aliondoka nayo , ila alishindwa kumtaarifu mumewe kutokana na ugomvi uliokuepo Kati yao.

Ndugu waliomhifadhi miezi yote hiyo wananipigia kunisihi niongee na shemej yangu, ampokee mkewe maana Ni mjamzito sn anaweza kujifungua MDA wowote. Nimewaambia hiyo Kazi siifanyi, fanyeni nyie wenyewe mlioyasababisha. Wanadai jamaa hawezi kuwaelewa, walishagombana tyr na hawapokelei kbs simu zao.

Nmemtafuta shemej, anachosema Ni kwamba Kama kweli mkewe aliondoka na mimba Yake ile mwezi MEI Mwaka Jana walipogombana, Basi mwaka huu mwezi January au February alitakiwa awe tayar keshajifungua.

Sahv Ni mwezi MARCH,miezi 11 tangu mkewe aondoke bado Ni mjamzito hajajifungua, hivyo kwa vyovyote vile ile mimba sio Yake. Kaipatia huko huko kwa ndugu zake. Na kwa tafsiri hiyo, hamna ndoa Tena hapa.

Kiukweli mpk sasa kichwa kimepata Moto, sielewi nifanye Dada yangu akae sawa maana analia muda wore. (Na mimba alionayo nahisi itamletea shida na huenda akajidhuru).

Pia nishaur Nini kifayike ikiwezekana arudiane na mumewe, maana jamaa hatak hata kumskia mkewe Wala habar zake na kahama kbs pale nyumbani, kaenda kupanga sehem nyumba nyingine kbs.

Nawasilisha
Simple tu aliyempa mimba ailee asiwasumbue..!
 
Kwahiyo anataka arudi tena kwa mnyanyasaji, hawa viumbee 😱

Ushauri wangu usijibebeshe mzgo haukuhusu ndo mana ulimtimua mwanzoni apambane! umemsaidia saana mpe fungu kidogo la kujifungua na matumizi awe comfortable, na asikae kwa ndugu arudi kwao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom