Ukitaka kwenda kuishi Marekani inabidi ujipange

Ukitaka kwenda kuishi Marekani inabidi ujipange

Shida sio njaa ya mafanikio. Shida siwezi kuishi kwenye utamaduni wa design hiyo ya Marekani. Maisha sio kutafuta pesa tu.

Kuna mdau huko juu kasema, ukiwa unasaka maisha huko hata ukipata mtoto ni tabu nyingine umejiletea. Kwa mimi hiyo naona ni mateso tupu

Nchi huwezi kupiga story hata na jirani kila mtu bussy na mambo yake, hapohapo hata mtoto kuzaa ni kwa mahesabu makali aisee! Mimi loniless ingeniua. Nendeni mnaoweza sie hapahapa kwa Nyerere panatutosha, tena ukiwa na hela hapa bongo mbona tambarare tu.
Kule umeambiwa ni full capitalism, wewe unataka ukakae kwa jirani upige nae stori masaa matatu,wakati maisha kule ni ghali,utamlipia bills?Nenda kule kama una kiu ya mafanikio mkuu.
 
Umeandika kwa weledi wa hali ya juu sana. Hongera. Hapa Tanzania kuingiza laki kwa siku inawezekana lakini inahitaji utulivu pia kama huko Marekani. Ila watu wengi TZ bado vipato vyetu viko chini kwahiyo kufikiria kuja Marekani bado ni wazo lenye uhai.
Ndugu yangu, ushauri wangu kwa vijana wa kitanzania ni kwamba kama unaona maisha hayana muelekeo Bongo si vibaya kabisa kujaribu nje ya nchi, kabla sijaja Marekani nilikua nchi moja ya Afrika Magharibi, vijana wengi kutoka Kenya na Uganda walikua huko wakifanya kazi kwenye Mashirika kama Unicef nk, na kazi hizo zilikua ni volunteering, mshahara si mkubwa lakini zilikuwa na nia ya kuwapatia CV's lengo ni kupata kazi za kudumu, kwa sababu kazi nyingi za Mashirika ya UN unaanzia kama intern. Watanzania tulikua wachache sana.
Hivyo kama maisha yamekwama Tanzania si mbaya kujaribu nje ya nchi, na kwa mtazamo wangu Marekani ni nchi yenye fursa nyingi, lakini si nyepesi vile vile. Narudia kazi ya chini Marekani ni tofauti kabisa na Tanzania, na kazi nyingi Tanzania ambazo tunazidunisha kama Nursing, madereva wa magari makubwa, ni kazi za zenye kipato kikubwa.Na sijui kwa Tanzania, safari ya kuwa Nurse Marekani si nyepesi pia! Lazima uende shule, na tatizo unaenda shule ukiwa unafanya kazi.

Hivyo usije Marekani ukategemea kutoka ghafla! Nchi hii ina mfumo na utaratibu wake, inabidi upate mtu wa kukuongoza, na ukiongozwa vibaya imekula kwako! Epuka kuwa na record mbaya polisi, kutolipa madeni, kunyanyasa wanawake au kuzaa na mwanamke bila kuwa na ndoa! Itakula pesa yako kwa child support! Hivyo hangaika kwanza matanuzi yatakuja baadaye.

Jamaa zetu wa Kenya na Nigeria huja Marekani wakiwa wanajua wamekuja kufanya nini, na wanajaribu kwa mbinu zote nzuri na chafu! Ujasiri huo wabongo hatuna!
 
Mtu mwenye bachelor degree ya early childhood education,hapati kazi huko,hata ya uyaya?
Vyeti vingi nikiwa na maana Diploma/Degree za nchi za nje Marekani na hata Canada ni makaratasi tu! Inabidi vifanyiwe certification kukubaliwa Marekani! vitafanyiwa tathimini kwa malipo si haba, na utaambia uongeza masomo fulani kukubaliwa, ni vigumu sana kuingia na baadhi ya vyeti vikakubalika US. Wale waliosoma IT na kufanya mitihani inayotambuliwa Ulimwenguni nimeona wanakua na ahueni.
 
Tatizo la USA miguu ya kuku na manati ya mzungu kila kona ,dakika 0 wahuni washakufumua ubongo bila sababu yeyote.
Amalinze the Cat, Si kweli ndugu yangu, media inaweza kabisa kukupa picha tofauti ya kila mahali! Kama vile baadhi ya Wamerekani wanaamini bado tunaishi na nyani kwenye miti. Naishi Texas, the gun loving State hakuna kupigana risasi kama inavyosemekana! Sijawahi wahi kuwa na hofu ya kupigwa risasi Texas, magomvi mengi ni visa na visasi, ukiacha wendewazimu wachache ambao hupiga risasi pasipo sababu! Kuna maeneo kweli ukienda kuna risks ya kutumiana risasi, kama strips clubs ambako wengi ni wahuni! Unapoenda clubs za usiku lazima uwe mwangalifu! Ingawa kuingia humo lazima uwe umepekuliwa kama una silaha! Na kwa kuishi kwangu tTexas natambua kwamba asilimia kubwa barabarani kila mtu ana mguu wa kuku! Hivyo unaepuka magomvi au mizozo ya kijinga. Kwa wingi wa bunduki zilizomo mikononi mwa watu Texas, kama watu wengekua fyatu mauji yengekua makubwa sana! Hivyo ondoa hofu hiyo! Inatokea ndio, kama ambavyo bongo unasikia mtu kamchoma kisu mwenziwe! Hii aifanye niseme bongo wanachomana visu inipe hofu.Karibu Marekani Amalinze the Cat.
 
DV lottery Ni nin
Instabul, DV lottery ni bahati nasibu ya watu kuingia na kufanya kazi Marekani, kuicheza ni bure, lakini uikiipata kuna gharama si kubwa za kufanya process, hiyo inakupa uhahali wa kuishi Marekani na kufanya kazi, kwenda shule/Chuo na baadaye kama untaka kuwa raia.
 
Boss, nilitaka kukupuuza lakini nimeona sintowatendea haki vijana walioanzisha huu uzi na kutaka kujua mambo! Ujuzi unapoupata uwe unakufaa au haukufai tayari ni wako kama utautumia is up to you!

Mzee kwanza unaonekana una makasiriko sana, nikushauri kitu, ukiona uzi haupo kwenye interest zako achana nao, dunia hii mzee ina mambo mengi sana kama ilivyo JamiiForums, ina nyuzi za kutosha nenda kasome na na kuchangia za kiume. Mzee kazi za kiume ni zipi? Unaonekana umepitwa sana na wakati, ni uhasibu, uhandisi, ujenzi, uchimbaji wa madini, uanajeshi, mgambo au ni nini unamaanisha? Najua kazi pekee inayoweza kufanywa na mwanaume tu ni kutom... Zingine zote duniani hazina jinsia kila mtu anafanya, ndio maana Rais ni mwanamke au hiyo nayo ya kike?. Una haki ya kuchagua chochote ufanye ila uwe na adabu kwa mambo yasiyokuhusu. Kama hayakupendezi unapita tu kushoto.

Hiyo unayosema kazi ya kike mwaka jana imenipa $195,000 na tax refund $45,000 wewe yako ya kiume imekupa ngapi? Yani nipo sawa na vyeti vyangu vingine vimekaa vinachakaa. Wanangu hapa baada ya graduation wakiamua kurudi Tz watashindana na watoto wa Lowasa na wa ngazi hizo. Sio hao 60,000 plus wanaokwenda kudhalilishwa Mkapa stadium kugombea nafasi 1000 za TRA. Akija anakuja kuchukua senior position popote ndani na mfumobongo bila shaka. Yani mwanao na mwanangu wa kike hawatakaa waonane popote au na wewe. Usidharau usivyovijua wakati huna cha kuonyesha na hata hivyo kama umefanikiwa sana na kazi za kiume why kuhangaika na wengine? Fanya yako dunia kubwa hii, kila mtu angekuwa wewe si ingekuwa inaboa sana? Mmoja akilima nyanya, we lima bamia mkivuna wote mnapata mchuzi!!!

Hamna kati yetu aliyeanzisha huu uzi hapa kujisifia kama unavosema, tumejibu maswali ya vijana wanaohangaika kujua kupata hali halisi na ni hiyari yao kuchukua au kuacha, uwanja mpana huu. Wabongo bana mkiuliza mkajibiwa shida, wakikaa kimya wana roho mbaya, tukoje sisi? Sorry kwa watakaokwazika.
Najua kazi pekee inayoweza kufanywa na mwanaume tu ni kutom... Zingine zote duniani hazina jinsia kila mtu anafanya, ndio maana Rais ni mwanamke au hiyo nayo ya kike?.

Hapa umefafanua in deep umeeleweka mkuu

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Laiti ungejua Katika kazi marekani zinazolipa pesa nyingi kwa saa ni RN (dola 100)kwa saa
RN ni mojawapo ambayo ni kimbilio la wengi hasa watu wa kuja, lakini kuna kazi nyingi Marekani zinalipa mno zaidi ya hapo Bushmamy! Engineers, Lawyers, bankers wanaosimamia investments! Mishahara yao ni mikubwa sana! Kwa wengi wetu njia ya mkato ni nursing, na wengine hawajui kabisa kuna kazi zaidi ya nursing, rafiki yangu Lawyer kumuona kwa ushauri tu ni $400 kwa saa! Nursing ni kimbilio la watu wengi wa kuja.
 
Kiongozi ndo maana nimesema dunia na maisha is about choices na usijudge choices za za mtu. Hapa nina MBA na PMP license but I chose RN. Naweza kufanya chochote as long as nimependa sio aibuke mtu unakutana naye kwenye uzi aanze kupangia watu choice zake, period.
 
Boss, nilitaka kukupuuza lakini nimeona sintowatendea haki vijana walioanzisha huu uzi na kutaka kujua mambo! Ujuzi unapoupata uwe unakufaa au haukufai tayari ni wako kama utautumia is up to you!

Mzee kwanza unaonekana una makasiriko sana, nikushauri kitu, ukiona uzi haupo kwenye interest zako achana nao, dunia hii mzee ina mambo mengi sana kama ilivyo JamiiForums, ina nyuzi za kutosha nenda kasome na na kuchangia za kiume. Mzee kazi za kiume ni zipi? Unaonekana umepitwa sana na wakati, ni uhasibu, uhandisi, ujenzi, uchimbaji wa madini, uanajeshi, mgambo au ni nini unamaanisha? Najua kazi pekee inayoweza kufanywa na mwanaume tu ni kutom... Zingine zote duniani hazina jinsia kila mtu anafanya, ndio maana Rais ni mwanamke au hiyo nayo ya kike?. Una haki ya kuchagua chochote ufanye ila uwe na adabu kwa mambo yasiyokuhusu. Kama hayakupendezi unapita tu kushoto.

Hiyo unayosema kazi ya kike mwaka jana imenipa $195,000 na tax refund $45,000 wewe yako ya kiume imekupa ngapi? Yani nipo sawa na vyeti vyangu vingine vimekaa vinachakaa. Wanangu hapa baada ya graduation wakiamua kurudi Tz watashindana na watoto wa Lowasa na wa ngazi hizo. Sio hao 60,000 plus wanaokwenda kudhalilishwa Mkapa stadium kugombea nafasi 1000 za TRA. Akija anakuja kuchukua senior position popote ndani na mfumobongo bila shaka. Yani mwanao na mwanangu wa kike hawatakaa waonane popote au na wewe. Usidharau usivyovijua wakati huna cha kuonyesha na hata hivyo kama umefanikiwa sana na kazi za kiume why kuhangaika na wengine? Fanya yako dunia kubwa hii, kila mtu angekuwa wewe si ingekuwa inaboa sana? Mmoja akilima nyanya, we lima bamia mkivuna wote mnapata mchuzi!!!

Hamna kati yetu aliyeanzisha huu uzi hapa kujisifia kama unavosema, tumejibu maswali ya vijana wanaohangaika kujua kupata hali halisi na ni hiyari yao kuchukua au kuacha, uwanja mpana huu. Wabongo bana mkiuliza mkajibiwa shida, wakikaa kimya wana roho mbaya, tukoje sisi? Sorry kwa watakaokwazika.
Mzuzu asante sana! wengi katika jamii ya kitanzania wana mawazo mgando! Ukitoka nje utaona kazi ni kazi! mradi inakupa maisha, na hakuna anayekudharau kwa sababu halipii maisha yako! Naogopa sana mfumo wa Tanzania umefanya watu wawe na wamawazo ya ubosile! Nimepiga box Marekani, ndani ya kiwanda Supervisors/Managers wanaweza kufanya kazi ya kawaida kabisa kama kuna upungufu wa watu, nimeona Meneja akiendesha Forklift, Supervisor akitoa garbage cans, kinyume kabisa na ilivyo bongo! Bosi ni bosi! Huyo supervisor/ Meneja haipunguzi kabisa hadhi yake akifanya kazi hizo.Mambo ya kazi ya kiume/kike yamepitwa na wakati mno!
 
Kiongozi ndo maana nimesema dunia na maisha is about choices na usijudge choices za za mtu. Hapa nina MBA na PMP license but I chose RN. Naweza kufanya chochote as long as nimependa sio aibuke mtu unakutana naye kwenye uzi aanze kupangia watu choice zake, period.
Nakuelewa Mkuu, sikuwa na muda na biology ilinikataa toka bongo! Kila heri mkuu.
 
Nakuelewa Mkuu, sikuwa na muda na biology ilinikataa toka bongo! Kila heri mkuu.
Yes exactly, tunachowaambia vijana ni kwamba ukiwa huku una nafasi nyingi na unafungua milango yako. Tanzania hauna hata choice inapotokea unataka kufanya chochote unakuta njia zote zimefungwa. Sio kwamba tunachofanya personally is the best. Ukiingia kihalali una potential kubwa sana ya kufanikiwa kuliko nyumbani. Wote tunapenda nyumbani ila tuchukulie kuhama ni kama kutoka Shinyanga kwenda kutafuta maisha Rukwa. Kama kuna opportunity unahama tu. Dunia leo hii ni kijiji na maisha ni mafupi sana, so fanya unachokipenda na kukupa furaha au kutimiza malengo yako.
 
Mtu mwenye bachelor degree ya early childhood education,hapati kazi huko,hata ya uyaya?
since saa 7 nipo kwenye huu uzi napitia nondo za ma bro waliopo mbele ila hii komenti imenichekeaha saana. imebidi niache kusoma nireply tu. eti uyaya [emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom