Kutulia inategemea tu ndugu yangu. Unaweza pata mwanamke mdogo haelewi chochote, umemchukua na kumwamini. Utandawazi ukamfumbua macho. Unaweza tamani kujitoa uhai.
Mimi nninachofikiria muda mwingine, mwanamke anaweza akabadilishwa kuwa mzuri au mbaya kutokana na wewe mwenyewe. Imagine umeoa, kila leo unarudi umelewa, hakuna kusikilizana, kila mara fujo. Nitavumilia mwanzo. Lakini yakinishinda, nitaanza kutafuta suluhisho. Mwanamke akikutana na mkaka mwingine ambaye anaonekana anajali, anasikiliza, mnapatana, urudi kwenye shida kufanya nini?
Lakini kwa upande mwingine, unajua majukumu yako, unajali, unampenda mkeo, unajitahidi kuwa naye karibu, kusikilizana na kumfanyia vitu vingi, je atoke nje kutafuta nini?
Ila pia, wapo ambao watatoka hata ufanye nini. Ni tabia zao na akili zao. N ndio hao ambao uwa wanarudi mbio wakilia baada ya maji kumwagika.
Hasa hivi vitoto vidogo ndivyo vinavyoongoza kwa tabia mbovu kutokana na either kuwa limbukeni na dunia, kufata makundi ya watu ili asionekane mshamba au malezi.
Ni kumuomba Mungu tu.