Maoni binafsi: Namna/Jinsi wanawake wanavyosababisha wanaume wengi kuchepuka katika ndoa

MUCOS

Member
Jun 24, 2024
40
213
Wasalaam,
Wana JF wote.

Leo nina mada kidogo kuhusu suala la uchepukaji kwa wanaume hususani walioko katika ndoa kunakosababishwa na wanawake wenyewe.

Nikiwa miongoni mwa wanaume walioko katika ndoa nimeonelea ni vema nikatoa maoni yangu kuhusu suala la wanaume wengi kuchepuka kwenye ndoa kunakosababishwa na wanawake wenyewe. Maoni yangu ni kutokana na uzoefu wangu katika kuiishi ndoa na pia harakati zangu katika kusuluhisha migogoro ya kindoa. Andiko langu linaambatanishwa na mfano kutoka kwa wanandoa wawili ambao ni dada "Tunu" na kaka "Hamisi" pamoja na mchepuko wa Hamisi uitwao "Hamida".

Sababu zitakazojadiliwa ni zile ndogo ndogo tu ambazo pengine jamii ya wanawake inaweza kuzichukulia poa tu lakini kiukweli zinabeba maana na ajenda kubwa kwenye dunia ya wanaume. Sababu kuu sita zinazopelekea wanaume kuchepuka ni:

1. Mwanamke wa ndoani kupuuza suala la urembo na kujipamba awapo nyumbani.

Je ushawahi kujiuliza ni kwa nini wanaume wengi hugeukageuka kutazama wanawake wawapo majiani?.
Je ushajiuliza ni kwa nini wawake wa baani hutongozwa sana na wanaume tena waliopo ndoani?. Je ushajiuliza ni kwa nini wanawake wanaojiuza hawakosi wateja tena wengi wakiwa ni waume za watu? Je ushajiuliza ni kwa nini kwenye ceremonial events kama harusi n.k wadada wengi huombwa namba za simu na kutongozwa kwa wingi tena na waume za watu.?....

Jibu ni kwamba maeneo hayo kuna wanawake wazuri na warembo kwa muonekano wa nje. Ni have katika maeneo hayo utashuhudia wanawake wakiwa kwenye mavazi mazuri yanayosanifu maumbile yao vema. Utashangazwa na vifua vya haja vilivyobustiwa na sidiria huku sehemu ndogo ya chuchu zikiachwa kuamsha fikra chochezi kwenye ubongo wa mwanaume. Pia utaweza kuona viuno dondola vyenye kubeba milima ya makalio yaliyofungashwa vema kwenye vijiguo vilivyoshonwa barabara na fundi Maiko. Ndugu yangu huko utashuhudia kila aina ya mibano ya nywele zenye kuchokoza hisia za mwanaume na pia make up zilizopandishwa hadhi daraja la kwanza. Hayo hufanywa na wanawake ili kuwa na mvuto mbele ya halaiki. Na amini ama usiamini baadhi ya wanawake hao kama sio wengi wao ni wake za watu na wana ndoa kamili kama ilivyo kwa mwanadada "Tunu" ambaye ni mke halisi wa kijana shababi "Hamisi". Sasa kumbuka mwanaume yeyote yule aliye rijali na shababi kama Hamisi ameumbiwa tamaa ya kupenda vile vilivyo vizuri kwa muonekano wa nje kabla ya kujua vilivyoko ndani.

Sasa turudi kwa dada yetu "Tunu" ndoani. Leo ni wikiend hajaenda kazini, hajaenda kwenye mialiko ya harusi wala hajahudhuria kwenye vikoba, na pia hajaenda kanisani. Leo amepata fursa ya kukaa nyumbani na mumewe kipenzi "Hamisi".

Tangu alivyodamka asubuhi na sasa ni saa kumi jioni, amejiachia kwenye dera lake kubwa linalopwaya na kuficha kila sehemu ya uzuri wa maumbile yake aliyojaaliwa na maulana. Nywele zake bora na maridadi zionekanapo pindi awapo kazini, shereheni au barabarani akatizapo hazipo na hazionekani tena. Nywele zilizopo na ambazo Hamisi anazishangaa ni kama zile za mwanamke mgonjwa aliyepo hospitalini akipata matibabu ya ugonjwa wa kichaa uliomtafuna zaidi ya mwezi mmoja. Au waweza kuzifananisha na zile za mwanamke mjane aliyetoka kumlilia marehemu mumewe. Zile make up zake alizozoea kuweka akiwa ofisini hazipo tena. Tunu kapauka balaa, miguu imejaa vumbi, kinywa hakijafanya zoezi la kutafuna bigijii kwa muda sasa tofauti na ilivyozoeka. Makalio yake mazuri yalizoeka kuonekana awapo kanisani zimefichwa kwenye dera pana. Zile chuchu mbinuko na mchongoko kama midomo ya kuku imejilalia kwa sasa kwani hakuna sidiria za kuzipiga jeki tena. Kwa kifupi Tunu anaoneka kijitu badala jitu, anaonekana mwala badala ya mwali. Tunu amechoka, ana harufu kali ya jasho ya kwapa. Ile harufu nzuri ya pafyumu inayovutia wanaume kila apitapo imeyeyuka.

Hamisi haelewi moja wala mbili juu ya kinachoendela. Anawaza na kuwazua Tunu wake kaenda wapi? na huyu aliyeko mbele yake ni nani?. Anaona hebu usinichezee ngoja niende zangu baani ama harusini huenda huko nikampata Tunu wangu wa halali. Safari yake hii inamfikisha baani na inamkutanisha na mwanamwali "Hamida" katika ubora wake. Hamisi anaanza kujisemea moyoni .."yeees! huyu ndiye Tunu wangu halisi". Katika mazingira haya mwanaume kuchepuka ni lazima.

Dada yangu Tunu, niamini mimi. Wanawake warembo kwa muonekano wa nje na kimavazi wapo barabarani, wapo maofisini, wapo baani, wapo makanisani na kwenye kumbi za starehe ila sio huku majumbani wanaume tunamoishi. Amini nakuapia, Tunu wa ofisini au harusini sio Tunu huyu wa nyumbani siku za wikiend. Ni watu wawili kabisa tena maadui ambao wakikutana uso kwa uso watazichapa laivu.

Hakika Hamisi akikutana na Tunu huyu wa kwenye sherehe za harusi, kumbi za starehe, fukwe za baharini na ama katika ibada za kila wiki atamtongoza tena na kumuachia vibunda kadhaa. Naomba niweke sawa hili kuwa, Hamisi ameamua kuw a na Hamida kama mchepuko wake sio kwa kuwa anampenda bali ni kwamba amevutiwa na pambo la mwanamke huyu kwa nje na pengine hii ndio sababu kuu hajataka kumpa talaka Tunu wake wa nyumbani licha ya kuwa na pambo na urembo mbovu kwa nje.

2. Mwanamke wa ndoani kukosa ubunifu katika mpangilio na muonekano wa chumba na nyumba kwa ujumla.

Kaka Hamisi je wakumbuka kipindi kile cha uchumba wenu ulipomtembelea mchumbako Tunu?, au yeye Tunu alipokutembelea kwa getoni kwako?. Dada yangu Tunu je wakumbuka kipindi kile cha uchumba kaka Hamisi alipokuja kukutembelea kwenye geto lako?, au ulipomtembelea kwenye geto lake?.. Je wakumbuka mlivyopambana kuweka chumba na nyumba katika muonekano bora? Je mwakumbuka kubadilishwa kwa mashuka kila mara? , vipi kubadilishwa kwa mipangilio ya sofa pale sebuleni?, vipi kuhusu upangaji wa vyombo kwenye kabati? na vipi kuhusu staili za utandikwaji wa shuka pale kwa kitanda?.. Je mlienjoy ee? Mlifurahi eee?.....Haya yote yalikuwa yanamfurahisha kaka Hamisi na kumfanya akufikirie wewe tu kila wakati na kila saa.

Turudi kwa mwanamke wa "ndoani". kwa kuwa dada Tunu ulishaolewa na kaka Hamisi na hivyo lengo lako la kupata ndoa kutimizwa, na kwa kuwa umesafiri ndoani kwa miaka saba sasa, ule mchecheto wako katika ubunifu na muonekano wa nyumba yako imetoweka kabisa. Ni mwaka sasa kitanda chako kiko palepale kilipokuwapo jana, kinatandikwa mashuka yaleyale tena hovyo, hakuna tena staili mpya ya kutandika mashuka. Sebule yako ni jana leo na hata milele hakuna ubunifu tena, jiko lako sasa hata nisiseme chochote. Unasingizia majukumu ya kikazi na malezi ya watoto.

Sasa dada Tunu wacha nikusanue, huyu Hamisi wako anaye mchepuko wake aitwaye "Hamida" ambaye pengine hana kazi nzuri kama yako huko serikalini na pengine ni baamedi. Huyu sio mzuri ukilinganisha na wewe. Lakini amini usiamini huyu amegeuka kuwa wewe wa kipindi kile cha uchumba. Kila mara Hamisi afikapo nyumbani kwake hukuta mpangilio wa viti sebuleni umebadilika, staili ya tandiko la shuka chumbani ni mpya, hajakaa sawa kaletewa chakula kwenye sahani ya kesho yaani tofauti na ile ya jana na leo. Hapa kaka Hamisi ni lazima achepuke tu. Hamisi anayawaza haya yote. Ubunifu na mpangilio wa vitu ndani ya nyumba inamvutia. Anaona mandhari ya kuvutia kwa ajili ya kupumzika pia anahisi kuivuta hewa iliyochujwa barabara. Anawaza kumdivosi mke wake Tunu asiyejua kuipangilia nyumba yake vema ili amuoe "Hamida". Ndipo moyo wake unamkumbusha kuwa pendo lake liko kwa Tunu na sio kiumbe mwingine. Anampenda Tunu kwa kuwa anampenda na si vinginevyo. Hapa anaamua "Hamida" kuwa mchepuko wake na sio vinginevyo.

Hapa naomba ikumbukwe kuwa, mwanume ameumbiwa tamaa na tamaa hiyo ikiwa ni pamoja kuona mandhari nzuri na yenye kuvutia yenye kumulikwa na hewa safi ya oksijeni . Hivyo kwa mwanaume kuchepuka haiepukiki.

3. Mwanamke wa ndoani kuwa na tabia za ujeuri kiburi na ufedhuli.

Waneni walipata kunena "ishi na mtu kwa muda mrefu ujue tabiaze". Ukweli ni kwamba kaka Hamisi na dada Tunu kwenye kipindi cha uchumba wenu kila moja alijitahidi kuficha tabia/hulka yake hasi na halisi ili isijulikane kwa mwenziwe na hivyo kuipoteza zawadi nono ya ndoa. Sasa baada ya kupiga hatua tano katika ndoa, makucha hufunguka na tabia hasi au halisi zilizofichwa hapo mwanzo huonekana vema kwani haziwezi kuvumilia kufichwa tena. Kwa leo nipo na tabia zako hasi dada Tunu wa miaka tano katika ndoa.

Mwanaume hapendi dharau Tunu, mwanaume wa kweli havumilii kibri wala ukaidi. Haijalishi yeye ni mkosefu au lah hasha! hapendi sudi za kuvunjiwa heshima. Dada Tunu sasa umemzoea mumeo Hamisi kwa kiwango kikubwa. Ile tabia yako ya kuongea kwa nidhamu na kujishusha uwapo mbele zake haipo tena. Ile haiba yako ya kikike ya kumkosoa mumeo kwa staha na adabu imeibwa. Ule utamaduni wako wa kuomba msamaha kwa kupiga goti mbele ya kipenzicho pindi ufanyapo madhila umetaifishwa. Ile kaliba yako ya kuitikia kwa upole "labeka mume wangu" pindi uitwapo na mumeo imenyamazishwa, na mwisho ile haiba yako ya kumpikia chakula kitamu mumeo na kumkaribisha kwa tabasamu bashasha mekoni kwa ajili ya chakula imemezwa na zimwi.

Dada Tunu umekuwa jeuri, umekuwa na kibri, umekuwa jasiri mbele ya mume wako kuishinda dini. Umekuwa nunda kwelikweli. Kiburi kimekujaa, unajiona hadhi sawa na mwanaume wako. Ukiitwa unaitika kijeuri, ukikosolewa kwa upole unakuja juu na kubwabwaja maneno lukuki, ukiona mumeo amekukosea unamshushua kwa maneno makali bila staha, adabu wala nidhamu. Umekuwa mkali kama pilipili kichaa. Hakika nakuapia dada Tunu usipoachika kwenye ndoa yako kwa sababu ya upendo na huruma ya Kaka Hamisi kwako, hakika mchepuko ni halali yako kwani mpaka sasa mchepuko "Hamida" ashakupiga goli 12-0. Hautaachwa. Narudia tena hautaachwa ila mchepuko utakuwa suluhisho dhidi ya machungu na madhila anayopitia mumeo Hamisi kwani sasa ndiye amegeuka kuwa yule Tunu wa kabla ya ndoani aliyemfanya kaka Hamisi aseme kweli nimepata mke.

Naomba kusisitiza hapa, kama dada Tunu mumeo sio yule wa kanisani anayeamini kwamba "ndoa ni mpaka kifo", au yule anayeamini katika "tuna watoto wawili naogopa wasije pata mateso", au yule ambaye "hana kazi wala kipato na wewe ndiye unamlisha na kumvalisha", hakika utapigwa talaka tatu juu na chenji ya mahari kudaiwa bila hiyana. But kama ni mojawapo katika hao hapo juu "mchepuko" ni halali yako.

4. Mwanamke wa ndoani kuwa mchafu kupitiliza.

Uchafu ni tabia isiyopendwa na mtu yeyote yule ikiwemo mwanaume. Yaani huwezi amini hadi mwanaume mchafu hampendi na kamwe hataki kuwa na mwanamke mchafu na siku zote maombi yake kwa Maulana ni kumpata mwanamke msafi.

Dada Tunu jaribu kuwa msafi ili kutengeneza mazingira ya kaka Hamisi kuvutiwa nawe pamoja na kuvutiwa na kwake. Baada ya kusafiri miaka minne ya ndoa na kujaliwa watoto wawili umesahau kabisa suala la usafi. Mtoto wako mkubwa nguoze zi chafu chikichiki, mikamasi ka yote inamtiririka huko michezoni achezapo na rikaze. Huyu mdogo pampasi hujambadilisha toka asubuhi. Alijenyea tangu saa mbili asubuhi hadi sasa ni saa nane na hajaoshwa. Wewe mwenyewe umejiachia balaa, chuchu zako ziko nje zikiwa zimening'inia na kujilalia zikiwa na huzuni ya kukosa matunzo huku wewe ukijifu ni kwa sababu " ninanyonyesha kwa sasa.." Nguo zako chafu na zinukazo zimetupwa hovyo hapo ndani zingine kochini na zingine kitandani. Hizi ni nguo za familia zikiwemo za kwako, za mumeo na watoto wako ambazo zimevaliwa na kurudiwa kwa wiki tatu sasa. Sufuria zako ni chafu, hazina mvuto wa kimapishi, ni nyeusi balaa kwa kuzidiwa na masizi ya mwezi mzima. Viti, kabati na masofa yamejawa na vumbi tukufu, huku utando wa buibui ikipendezesha nyumba yako kwa namna ya ajabu na kushangaza.

Asee kwa namna hii kaka Hamisi kila akitoka kazini lazima apitie baani au mpirani kuepuka madhila ya uchafu wako. Huko ndipo ampatapo mchepuko wake "Hamida" ambaye ni msafi kuliko wewe. Nakwambia Hamida ni single mother lakini mtoto wake "Kashen" yuko katika hali ya usafi muda wote, nyumba yake imepangiliwa vema, sufuria zake zinang'aa kama bati jipya, nguo zake zimeogeshwa na kupingwa pasi na kisha kuhifadhiwa kabatini kwa ustadi mkubwa. Viti, kabati na TV zinang'aa na kuvutia usoni. Kumbuka ikiwa mumeo Hamisi anaona aibu kupokelewa na kuitwa baba na watoto wake "Kandili" na "Mwadawa" punde atokapo kazini kwa namna walivyokuwa wachafu na wanatisha kwa mavazi yao ya hovyo, huku kwa Hamida amejitolea kuwa baba wa hiari kwa mtoto "Kashen" ambaye ni msafi na smart muda wote. Hapa kaka Hamisi anaona bora kuwa na mchepuko wake "Hamida" kwa sababu yeye ni msafi kuliko wewe. Hamisi atokapo kazini huona ni bora akajifiche kwa kimada wake Hamida na kwako Tunu atakuja usiku wa manane ili kuepuka uchafu wako.

5. Mwanamke wa ndoani kuwa na tabia ya ubinafsi na kutomjali mume wake.

Hii huenda isiwe kwa wanawake wote lakini baadhi ya wanawake ni wabinafsi na wachoyo kwa kiwango cha juu sana. Dada Tunu mwanzoni kabla ya kwenda ndoani ulimpenda Hamisi, ulimjali Hamisi, uliwapenda na kuwajali ndugu wa Hamisi. Ulijali mawifi, uliwapenda mashemeji na kuwatunza wakwe. Chochote kitu ulichopata ulishea naye. Na hata pale Hamisi alipoonekana kuzidiwa kimajukumu ulikuwa radhi kukopa hela kwa kaka yako "Mdoe" ili kumpiga jeki. Kaka Hamisi akakupenda, akakujali na kuona sasa nimepata mke.

Leo ni mvua sita ndoani, dada Tunu umekuwa mbinafsi. Umekuwa mchoyo kwa mumeo na kwa nduguze .Huwajali tena kama zamani. Unajijali na kujipenda wewe mwenyewe na nduguzo. Vihela vyako unaficha mithili ya uchi wa msichana bikra, samahani namaanisha guchi , kwani hutaki mumeo ajue mahali zilipo. Unawapenda ndugu zako balaa na unajitoa kwao but kwa ndugu wa mumeo umewapa kisogo. Huwapendi tena kama zamani. Kila ajenda ikiwekwa mezani utasikia...."mume unajua mdogo wangu yule mdogo ame..., mama yangu mkubwa yule wa Mpanda ana....., Unajua bebi shemeji ako yule wa chuo ame...." Hata siku moja haujawahi kuzungumzia upande wa mume wako. Hujawahi kumzungumzia mama yake, wadogo zake n.k. Umeanzisha/umeanzishiwa biashara ikubusti au la hasha una kazi yako nzuri aidha serikalini au private lakini humsaidii mumeo kwa chochote. Hujali hata kidogo pindi akwamapo. Labda ukijali kidogoo unamkopesha. Umemezeshwa kauli kuwa "hela ya mwanamke ni kwake pekee na sio kwa mume wake". Ni kwa nini umeanzisha ujenzi wa nyumba kwa kushirikiana na mama yako bila kumshirikisha mume wako?.

Kaka Hamisi amechanganyikiwa kuhusu wewe kwani ni kweli anajua kuhusu sudi yako ya ubinafsi. Hana hakika kama utamvumilia endapo atakosa kazi yake inayokusababisha uzidi kuwa naye kwa sasa. Hana hakika kama utawajali nduguze pindi akianguka. Solution la suala hili ni mchepuko wake "Hamida" ambaye akiwa naye kidogo akili yake inasahau balaa lako na matatizo yake kwa masaa kadhaa kabla hayajamvaa tena. Hapa uchepukaji ni lazima.

6. Mwanamke wa ndoani kuwa na imani juu ya watu wengine na sio mume wake.

Kabla ya kwenda ndoani, dada Tunu ulikuwa ukimuamini mumeo kwa kila kitu. Ulimshirikisha kila Jambo lako liwe la heri au la shari ili akupe mwongozo. Ulimsikiza kwa kila kitu hata pale mama yako alipokuzuia ulimkasirikia. Alichokisema ulikifanyia kazi kwa bidii na kwa ufasaha mkubwa.

Leo ni miaka miwili tangu safari ya ndoa kuanza. Tunu umebdilika sana. Humuamini tena Hamisi wala huzingatii maagizi na marudi yake. Umeijenga imani yako kwa watu wa nje, namaanisha nje ya ndoa.

Dada Tunu leo unamwamini baba mchungaji wako kuliko mumeo Hamisi. Unayapokea na kufanyia kazi mashauri ya askofu na nabii hata kama ni hasi kwa ustawi wa familia yako. Leo unamwamini yule mganga wako wa Sumbawanga anayekudanya na kula hela zako kuliko mumeo. Unaona ni bora ukapeleka hela zako kwake badala ya kumsapoti mume wako Hamisi anayepambana kutafuta hela kwa ajili ya ya kupata japo ekari moja ya ardhi apate kusimamisha walau pagala kwani baba wa nyumba amemchosha kwa masimango na matusi yake.

Dada Tunu ni kwa nini leo unamuamini mama yako mzazi katika kila kitu chako badala ya kumuamini mumeo Hamisi. Eeee. Nakuuliza tena ni kwa nini? Je wajua ni mumeo peke yake ndiye anakupenda kwa dhati hapa duniani? Ngoja nikwambie mama yako anakupenda kwa kuwa wewe ni mtoto wake na kwamba hiyo sifa ya kuwa mtoto wake ikitoweka hatakupenda tena. Ni mumeo tu ndio anakupenda kwa kuwa ni wewe na sio kitu chochote. Tunu nakuuliza ni kwa nini leo mashoga zako "Werima" na "Kareni" wamekuwa washauri wako wakuu badala ya mwandani wako Hamisi?. Ni kwa nini ? , nauliza tena ni kwa nini?. Kwa nini unamwaga siri ya ndoa yako kwa mama yako na mashoga zako?. Ni kwa nini unapanga mipango yako na mama yako pia mashoga zako na sio mume wako Hamisi? Ni kwa nini umemtelekeza Hamisi?

Je wadhani mumeo Hamisi hajui kuhusu hili la kuamini mitume na manabii kuliko yeye? Je wadhani hatambui kuhusu siri zake zote unazommwagia mama yako? Au je wadhani hajui kuwa mashoga zako "Werima" na "Kareni" ndio wanakuamulia ufanye nini na usifanye nini? La hasha! unajidanganya.

Kwa taarifa yako, Mume wako Hamisi analijua hili vema. Anajua vizuri kabisa kuwa humwamini tena. Na labda nikuambie kwamba jambo hili linamuumiza sana. Sasa jawabu pekee kwa Hamisi juu ya Jambo hili ni mchepuko wake "Hamida". Amemweleza yote anayopitia na ndipo Hamida amejifanya kumjali sana ili aendelee kutafuna hela zake kwani kwa upande wa pili Hamida ni kama wewe tu. Pengine Hamisi ataomba ushauri kutoka kwa marafiki ambao watamshauri kukutandika talaka tatu au kuwa na mchepuko Hamida kama mbadala wako. Hivyo Hamisi atampenda na kumuamini mchepuko wake Hamida na kadri siku zitavyozidi kusonga ndipo ataanza kuegemea upande wa Hamida kuliko upande wako.

Hitimisho

Ndugu mwanaJF katika bandiko langu hili nimejikita upande mmoja wa namna au jinsi wanawake wanavyopelekea wanaume kuwa wachepukaji katika ndoa. Huenda sababu zangu zikaonekana hazina mashiko kwa kuwa nimeangazia mambo madogo madogo tu ambayo huenda jamii ikaona hazina mashiko lakini kwa utafiti wangu nimegundua ni mambo madogo madogo yanayofanywa na wanawake ndio husababisha anguko la ndoa zao. Siku nyingine ikimpendeza Mungu nitaandika kuhusu wanaume wanavyopelekea wanawake kuwa wachepukaji katika ndoa.

Mada yangu hii inaweza ikawa na dosari za hapa na pale hivyo natumai mtanivumilia mapungufu yangu. Pia kwa wale wasiopenda maelezo marefu mtanisamehe kwani nimelenga kutoa ufafanuzi wa kina wenye kuambatana na mifano hai ili kufanya uzi wangu uwe na mantiki. Itoshe tu kusema asanteni kwa kunipa muda wenu.

Muico
Jumatano 31.07.2027
1:25 PM

Wazinzi tuna

Wazinzi tuna sababu za Kila aina asee!!!

Mkeo avae sketi fupi ama aachie maziwa na uswahilini watu wanavyojua kutembeleana. Vile mara mjomba kaja ghafla tu,kaka,dada ndo usiseme muda wote wanapishana tu kama Kuna ziara ya mwenge atavaa sangapi hizo nguo Nje na maadili? Ukumbuke wote hatuishi kwenye geti.

Pia ukumbuke Watoto wanapaswa wajifunze kutoka Kwa mama Yao maadili mema!

Mimi nishapiga maarufuku hayo mavazi Kwa wife. Mwanamke ukimruhusu hivyo hata kwenye mkusanyiko wa watu atavaa hivo na hutomwambia kitu maana ushamruhusu.
 
Uasherati wenu tu unawasumbua 😎😎😥😕 sijasoma yote ila ni uasherati tu ndio umsukuma mwanaume kuchepuka. Yan mtajitafutisha sababu weeeee ilimradi tu kuhalalisha uasherati wenu.

Hela tutafute, tupike, tufue, tuzae, tulee, bado tuangaike na vimini sijui nywele. Mara adabu, Mara kupangilia chumba. Mxuuuuuu. Sijipi fistula za ovyoovyo mi. 😁😁😁😀
Kwa miujiza gani mliyonayo. Tupumzisheni batoto ba baba mkweeee.
 
Yaani hadithi yote hiyo ni issue za nyege tu. embu andika chapisho la kibiashara achana na hayo mambo ya kingese
 
Kila mtu na mtizamo wake mie na muunga mtoa mada kabisa hadi mko wawili chumbani anatupia dela kama sio kunitafuta sababu
 
Daaah!!! Uko wapi...
 
Utaishi single wewe kama usipo badilika
 
Uasherati wenu tu unawasumbua 😎😎😥😕 sijasoma yote ila ni uasherati tu ndio umsukuma mwanaume kuchepuka. Yan mtajitafutisha sababu weeeee ilimradi tu kuhalalisha uasherati wenu.

Hela tutafute, tupike, tufue, tuzae, tulee, bado tuangaike na vimini sijui nywele. Mara adabu, Mara kupangilia chumba. Mxuuuuuu. Sijipi fistula za ovyoovyo mi. 😁😁😁😀
Kwa miujiza gani mliyonayo.
Yaani hadithi yote hiyo ni issue za nyege tu. embu andika chapisho la kibiashara achana na hayo mambo ya kingese
Tupumzisheni batoto ba baba mkweeee.
Hahaha! Hahaha! Umenichekesha kwa kweli mkuu....eti kupangilia chumba😃😃
 
Kila mtu na mtizamo wake mie na muunga mtoa mada kabisa hadi mko wawili chumbani anatupia dela kama sio kunitafuta sababu
Life style yetu ndo inapingana na hayo maisha. Mimi yetu hii ya Kila siku wageni. Mimi Huwa anavaa Wakati wa ibada tunaenda kulala sawa sio mchana mara madogo zangu wapo halafu waone titi muda huo Mimi npo job. Mimi hapana kwakweli
 
Kwahio mchana ndio nywele zake aziache bila kuzichana?
 
Wewe umetazama nywele tu? Mmesema avae nguo kama za mabamed nyumbani Ili akuvutie. Labda kama unaishi kisiwani ama sisi maisha ya mwingiliano tunayoishi ni tofaut na yenu.

Kwa kifupi binti aliyekulia kijijn Kwa miaka yote ukamuoa ni ngumu sana kuvaa kama alivyopendekeza ni ngumu mno.

Halafu tunasahau kitu kimoja sisi wanaume hata avae vipi Bado kutamani Nje kuko palepale asee.
 
Back
Top Bottom