Ukistaajabu ya tozo, tazama wafanyabiashara tunavyoumizwa na serikali

Mkuu umesahau ile Kodi nyingine inayotozwa na Manispaa mara baada ya kulipa Kodi ya Leseni inaitwa Service Levy. Ukiwauliza hiyo kodi ni ya nini wanasema ni kwa ajili ya elimu, afya na barabara. Ingawa tunatozwa tena VAT na Tozo za Benki na Simu kwa ajili ya huduma hizo hizo. Kujiajiri ni shida nchi hii.
Iko siku yanamwisho! Ndiyo maana wakistaafu wanarudi kuteuana tena hadi wafie madarakani kwasababu mazingira ya biashara wanayajua ni magumu
 
Huwa namshangaa sana kiongozi anayewashauri watu wajiajiri!

Kujiajiri Tanzania inabidi kwanza ujitoe ufahamu kabla ya kupata faida!
Ebu fikilia haya malipo ya serikali yalivyo hayana uhalisia!
  • Unatafta wazo la biashara,mtaji na fursa lakini TRA hawanaga grace period kwa wafanyabiashara wadogo kama ilivyo kwa uwekezaji mkubwa
  • TRA hawana muda wa kufikilia TIN zenye msamaha wa kodi kwa wafanya biashara wanaoanza!
  • Malipo ya pango la biashara lazima mfanyabiashara ukalipie 10% ...wakati aliyetakiwa kutoa hiyo ni mwenye nyumba ulipo panga wewe! Lakini kwasababu mfanyabiashara unashida wanakubana wewe!
  • Halmashauri na manispaa pasipo kukupa msaada wowote, ukifuata leseni wanakutoza pesa kuanzia elf 80 hadi laki tano kulingana na biashara yako! Tena kibaya zaidi unawafuata ofisini kwao ukapange foleni hata juisi ya kufuta jasho la nauli kwa kuwapelekea pesa ofisini hawakupi, sasa ebu jiuloze pesa zote hizo manispaa wanachukua kwa mchango UPI waliompa mfanyabiashara kama siyo dhulma?
  • Malipo ya leseni yanaumiza sana kwasababu kwanza hawajishughulishi hata kukupa elimu ya biashara, hawakutaftii wateja hawakupi ofa yoyote zaidi ya kukukamua tena wakiwa ofisini kwao.
  • Ukifanikiwa kufungua matawi ya biashara yako, ajabu kila manispaa utaombwa kulipia mfano! Kama leseni ni tsh 350000 ukiweka tawi kila wilaya utatakiwa kuilipa pesa hiyo kila wilaya utazani ni nchi tofauti wakati uko Tanzania moja
  • Yote tisa kote pesa wamechukua pasipo hata grace period, ukitaka kuweka bango la kujitangaza biashara yako watakuja Kudai ULIPIE BANGO Lako la kujitangaza, wanakuchaji kwa square meter.
Yapo mengi sana wafanyabiashara tunadhulumiwa na selikali kuna wakati natamani katiba iseme wazi kabisa! KIONGOZI YOYOTE LAZIMA AWE MFANYABIASHARA Mwenye biashara ya jina lake iliyofanya kazi angalau miaka 10 na kuendelea! Labda itasaidia kutuelewa tunavyoumia wafanyabiashara.

Manispaa wanapata pesa za bure sana na sielewi kwanini LESENI ZAO zisiwe bure au wapunguze anagalau bei ya juu kabisa kwa duka,yard au kampuni isizidi lakimoja!

Na ikiwrzekana makao makuu ya ofisini ilipo ndipo inatakiwa kulipiwa leseni na huko kwenye matawi ipelekwe nakala au walipie kwa nusu bei!

View attachment 2330892
Hili la grace period linaandaliwa ila wafanyabiashara hakuna wa kuwachekea hamlipi Kodi nyie.
 
Hili la grace period linaandaliwa ila wafanyabiashara hakuna wa kuwachekea hamlipi Kodi nyie.
Alokwambia kuna mtu anataka kicheko nani? Tunahitaji Sera rafiki katika utozaji kodi!

Watanzania wengi tupo tayali kulipia kodi shida utitili na milolongo ya kila hatua kodi!
Ndiyo maana hata ajira haziongezeki
 
Hapo bado hawajaja kukwambia inatakiwa utoe mchango wa mwenge yan hapo hawaombi Bali wanataka pia utaskia tusaidie Lita 10 za diesel OCD anaomba hujakaa sawa unaambiwa kuna kikao na mkuu wa mkoa/wilaya tunawaomba kamchango kidogo.

Hujakaa sawa Askari wa fire hao wanakwambia unataka ulipie fire sa sijui huwa n kazi gan si nibora wanihimize niwe hata na fire extinguisher.

Kidogo unaona Askari wengine wamekuja na jamaa wawili wanakwambia mbona huna certificate ya TBS Sasa hapo unashindwa kuelewa dukani na certificate ya TBS wapi na wapi?

Baada ya siku mbili unawaona TMDA hao Tena hujatulia vizuri wanakuja watu wanakiita bodi ya maziwa nao wanataka hela.

Ukijiongeza ukasema wacha nifanye distribution ninunue kigari Cha kusambaza utashangaa ya LATRA.

Ukitaka kujua taasisi za serikali hawajielewi na kujitambua nenda TRA waambie nataka kufungua Biashara naombeni viwango vya kulipia kuanzia kidogo hadi kikubwa wakikupa niite mbwa tofauti na kukulazimisha ujazo mifomu alafu wake kukutembelea ilihali wewe unataka kupata taarifa tuu.
Hayo yote hakuna sehemu serikali inakusaidia ushauri hata kukudhamini mtaji kitu watakachokisaidia Ni kukutafutia polisi wakukamate wakakufunge au wakutoze pesa kubwa ushindwe kuendeleza Biashara yako na ufunge urudi kuilaumu serikali.

Wakija wageni kutoka nchi flan wanakuja na begi tuu wanaaminiwa n wawekezaji serikali na taasisi zake wanawapa msamaha wa Kodi wanaenda mbali Hadi kuwadhamini mitaji alafu watokeo yake wanakimbia najiuliza sisi tukiomba pesa tunaambiwa lete hati ya nyumba au shamba sasa hao ambao sio raia wa Tanzania sijui huwa wanapeleka hati ya Nini.

Ili utoboe tanzania hii lazima uwe magumashi mingi sana vinginevyo utalia vibaya mno.
We ndio umeongea ukweli na hili hata Marehemu Mengi kwenye kitabu chake kaliongelea ,CCM ni laana hii nchi . Ndio wanaotoa incentives za watu kuwa crooks , watu ni wezi ,wakwepa Kodi , criminals NK sio Kwa ajali Bali ni vitu vinavyotokea kama outcomes za upuuz unaofanywa na serikali hii ya CCM
 
Alokwambia kuna mtu anataka kicheko nani? Tunahitaji Sera rafiki katika utozaji kodi!

Watanzania wengi tupo tayali kulipia kodi shida utitili na milolongo ya kila hatua kodi!
Ndiyo maana hata ajira haziongezeki
Kabisa , hili suala Lina impacts kubwa mpaka kwenye ajira hasa private sectors . Kampuni kama inaelemewa na mizigo ya kodi za kipuuz zisizostaimilivu hata kuajiri itakuwa ni kidogo Sana sanasana ni redundancy / kupunguza wafanyakazi totally
 
Amepunguza ushuru wa mabasi kwenye budget Mpya aisee.
Sema jamaa wanaofanya biashara kwa hela za ofisini ni ngumu saba kutoboa..sababh unakuta unaiba ofisini kuendesha biashara mtaani siku upo kijiweni ndo una realize kwamba ulikua unaendesha biashara kwa wizi wa ofisini...
 
Hivi kila line ya simu wakiitoza 1000 kwa mwezi si itakuwa vizuri sana ili waondoe kodi sumbufu.
Zipo nchi kumiliki line sio kitu cha mchezo mchezo, wafunge macho waanzishe hili.
Almost 40ml.ppls wanamiliki line × 1000/- 40, 000, 000,000/-p/m, gains, na waondoe kodi sumbufu za majumba ya wastaafu.
 
Hapo bado hawajaja kukwambia inatakiwa utoe mchango wa mwenge yan hapo hawaombi Bali wanataka pia utaskia tusaidie Lita 10 za diesel OCD anaomba hujakaa sawa unaambiwa kuna kikao na mkuu wa mkoa/wilaya tunawaomba kamchango kidogo.

Hujakaa sawa Askari wa fire hao wanakwambia unataka ulipie fire sa sijui huwa n kazi gan si nibora wanihimize niwe hata na fire extinguisher.

Kidogo unaona Askari wengine wamekuja na jamaa wawili wanakwambia mbona huna certificate ya TBS Sasa hapo unashindwa kuelewa dukani na certificate ya TBS wapi na wapi?

Baada ya siku mbili unawaona TMDA hao Tena hujatulia vizuri wanakuja watu wanakiita bodi ya maziwa nao wanataka hela.

Ukijiongeza ukasema wacha nifanye distribution ninunue kigari Cha kusambaza utashangaa ya LATRA.

Ukitaka kujua taasisi za serikali hawajielewi na kujitambua nenda TRA waambie nataka kufungua Biashara naombeni viwango vya kulipia kuanzia kidogo hadi kikubwa wakikupa niite mbwa tofauti na kukulazimisha ujazo mifomu alafu wake kukutembelea ilihali wewe unataka kupata taarifa tuu.
Hayo yote hakuna sehemu serikali inakusaidia ushauri hata kukudhamini mtaji kitu watakachokisaidia Ni kukutafutia polisi wakukamate wakakufunge au wakutoze pesa kubwa ushindwe kuendeleza Biashara yako na ufunge urudi kuilaumu serikali.

Wakija wageni kutoka nchi flan wanakuja na begi tuu wanaaminiwa n wawekezaji serikali na taasisi zake wanawapa msamaha wa Kodi wanaenda mbali Hadi kuwadhamini mitaji alafu watokeo yake wanakimbia najiuliza sisi tukiomba pesa tunaambiwa lete hati ya nyumba au shamba sasa hao ambao sio raia wa Tanzania sijui huwa wanapeleka hati ya Nini.

Ili utoboe tanzania hii lazima uwe magumashi mingi sana vinginevyo utalia vibaya mno.

Umeandika point zote hongera sana.
Unazijua changamoto za kibiashara Tanzania
 
Back
Top Bottom