Ukistaajabu ya tozo, tazama wafanyabiashara tunavyoumizwa na serikali

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,276
21,395
Huwa namshangaa sana kiongozi anayewashauri watu wajiajiri!

Kujiajiri Tanzania inabidi kwanza ujitoe ufahamu kabla ya kupata faida!
Ebu fikilia haya malipo ya serikali yalivyo hayana uhalisia!
  • Unatafta wazo la biashara,mtaji na fursa lakini TRA hawanaga grace period kwa wafanyabiashara wadogo kama ilivyo kwa uwekezaji mkubwa
  • TRA hawana muda wa kufikilia TIN zenye msamaha wa kodi kwa wafanya biashara wanaoanza!
  • Malipo ya pango la biashara lazima mfanyabiashara ukalipie 10% ...wakati aliyetakiwa kutoa hiyo ni mwenye nyumba ulipo panga wewe! Lakini kwasababu mfanyabiashara unashida wanakubana wewe!
  • HATA mtu hujafanya biashara mwaka huo wa usajili TRA ikifikia kufaili return za mwaka lazima mahesabu yako yahakikiwe na kampuni ya uhasibu editor firm ambako gharama zipo juu sana hadi laki tano au zaidi hata kama UNAFAILI NIL (yaani hujafanya biashara), sijui kwanini Sera na sheria ya TRA wasingeweka utaratibu mrahisi kwa biashara changa ufaili hata kwa mhasibu personal wa kawaida kwa miaka 5 ya kwanza
  • Halmashauri na manispaa pasipo kukupa msaada wowote, ukifuata leseni wanakutoza pesa kuanzia elf 80 hadi laki tano kulingana na biashara yako! Tena kibaya zaidi unawafuata ofisini kwao ukapange foleni hata juisi ya kufuta jasho la nauli kwa kuwapelekea pesa ofisini hawakupi, sasa ebu jiuloze pesa zote hizo manispaa wanachukua kwa mchango UPI waliompa mfanyabiashara kama siyo dhulma?
  • Malipo ya leseni yanaumiza sana kwasababu kwanza hawajishughulishi hata kukupa elimu ya biashara, hawakutaftii wateja hawakupi ofa yoyote zaidi ya kukukamua tena wakiwa ofisini kwao.
  • Ukifanikiwa kufungua matawi ya biashara yako, ajabu kila manispaa utaombwa kulipia mfano! Kama leseni ni tsh 350000 ukiweka tawi kila wilaya utatakiwa kuilipa pesa hiyo kila wilaya utazani ni nchi tofauti wakati uko Tanzania moja
  • Yote tisa kote pesa wamechukua pasipo hata grace period, ukitaka kuweka bango la kujitangaza biashara yako watakuja Kudai ULIPIE BANGO Lako la kujitangaza, wanakuchaji kwa square meter.
  • Ukishalipa bei ya leseni manispaa bado unatakiwa kulipia TOZO ya leseni hiyo hiyo kila mwezi
  • Brela ukilipa na kusajiliwa bado wanataka Uendelee kuilipia TOZO certificate ya brela (Return au faini kila mwezi wakati wameshakusajili)
  • Ukituma unakatwa makato
  • Ukipokea unakatwa
  • Ukinunua kiwanja unakatwa VAT na ukitoa pesa kwenye akaunti unakatwa TOZO
  • Ukinunua umeme Tozo, ukilala Giza TOZO ya pango
WAKATI HAYO YAKIENDELEA MISHAHARA NA POSHO ZA WABUNGE NA VIONGOZI HAWAKATWI KODI, NA WAKISTAAFU WANALIPWA KWA MKUPUO!

Yapo mengi sana wafanyabiashara tunadhulumiwa na selikali kuna wakati natamani katiba iseme wazi kabisa! KIONGOZI YOYOTE LAZIMA AWE MFANYABIASHARA Mwenye biashara ya jina lake iliyofanya kazi angalau miaka 10 na kuendelea! Labda itasaidia kutuelewa tunavyoumia wafanyabiashara.

Manispaa wanapata pesa za bure sana na sielewi kwanini LESENI ZAO zisiwe bure au wapunguze anagalau bei ya juu kabisa kwa duka,yard au kampuni isizidi lakimoja!

Na ikiwrzekana makao makuu ya ofisini ilipo ndipo inatakiwa kulipiwa leseni na huko kwenye matawi ipelekwe nakala au walipie kwa nusu bei!

Ndiyo maana VIONGOZI wakitumbuliwa au kustaafu hutamani tena teuzi kwasababu mazingira ya biashara wanajua yalivyo magumu sana!

IMG-20220822-WA0001.jpg
 
Hapo bado hawajaja kukwambia inatakiwa utoe mchango wa mwenge yan hapo hawaombi Bali wanataka pia utaskia tusaidie Lita 10 za diesel OCD anaomba hujakaa sawa unaambiwa kuna kikao na mkuu wa mkoa/wilaya tunawaomba kamchango kidogo.

Hujakaa sawa Askari wa fire hao wanakwambia unataka ulipie fire sa sijui huwa n kazi gan si nibora wanihimize niwe hata na fire extinguisher.

Kidogo unaona Askari wengine wamekuja na jamaa wawili wanakwambia mbona huna certificate ya TBS Sasa hapo unashindwa kuelewa dukani na certificate ya TBS wapi na wapi?

Baada ya siku mbili unawaona TMDA hao Tena hujatulia vizuri wanakuja watu wanakiita bodi ya maziwa nao wanataka hela.

Ukijiongeza ukasema wacha nifanye distribution ninunue kigari Cha kusambaza utashangaa ya LATRA.

Ukitaka kujua taasisi za serikali hawajielewi na kujitambua nenda TRA waambie nataka kufungua Biashara naombeni viwango vya kulipia kuanzia kidogo hadi kikubwa wakikupa niite mbwa tofauti na kukulazimisha ujazo mifomu alafu wake kukutembelea ilihali wewe unataka kupata taarifa tuu.
Hayo yote hakuna sehemu serikali inakusaidia ushauri hata kukudhamini mtaji kitu watakachokisaidia Ni kukutafutia polisi wakukamate wakakufunge au wakutoze pesa kubwa ushindwe kuendeleza Biashara yako na ufunge urudi kuilaumu serikali.

Wakija wageni kutoka nchi flan wanakuja na begi tuu wanaaminiwa n wawekezaji serikali na taasisi zake wanawapa msamaha wa Kodi wanaenda mbali Hadi kuwadhamini mitaji alafu watokeo yake wanakimbia najiuliza sisi tukiomba pesa tunaambiwa lete hati ya nyumba au shamba sasa hao ambao sio raia wa Tanzania sijui huwa wanapeleka hati ya Nini.

Ili utoboe tanzania hii lazima uwe magumashi mingi sana vinginevyo utalia vibaya mno.
 
Hawako kiweledi zaidi ya utapeli, ni vigumu sana kutofautisha professionalism yao na dhulmat
 
Back
Top Bottom