Ukistaajabu ya tozo, tazama wafanyabiashara tunavyoumizwa na serikali

Tofauti ipo dmkali hawa wanalindwa na sheria wale dhamana za mahakamani...yaani mtu anatoka huko kwenye kikao eti cha Tozo ya bando akiamka bank akiamka sijui viingereza vya Railway Levy hawataishia hapo hawa...
Dawa yao siku ni kugoma mgomo mzito kama Sri lanka
 
Yaan utitiri wa kodi mpaka mtu unafikria au bora niajiriwe labda cku moja ntapata mwanya nami niwe kati yao? Mana if you cant fight them, then join them.
 
Dawa yao siku ni kugoma mgomo mzito kama Sri lanka
Yap kama itawezekana ni hatari sana aisee hii ya Bank sikuwahi kufikiri kama inaweza kuwepo lakini nilivyoona ishu ya mafuta walivyoichezea nikajua pana ujinga mwingi utaongezeka...mafuta yamepanda bei badala ya kufuta baadhi ya kodi wao wakashauri waweke ruzuku ya 100 Billion kipo wapi hali ni vile vile...
 
Kibongo bongo kufanya biashara bila kupiga kona kona,hutoboi kamwe.
 
Alafu Kuna mbuzi inasema toa risiti yaani sitoi nitafanya where necessary!! Nchi ya hovyo sana hii Kila mtu ashinde mechi zake.
 
Alafu Kuna mbuzi inasema toa risiti yaani sitoi nitafanya where necessary!! Nchi ya hovyo sana hii Kila mtu ashinde mechi zake.
Bidhaa moja inakodi 10 unatoaje risiti sasa! Haivutii hata kuwa mzalendo
 
Huwa namshangaa sana kiongozi anayewashauri watu wajiajiri!

Kujiajiri Tanzania inabidi kwanza ujitoe ufahamu kabla ya kupata faida!
Ebu fikilia haya malipo ya serikali yalivyo hayana uhalisia!
  • Unatafta wazo la biashara,mtaji na fursa lakini TRA hawanaga grace period kwa wafanyabiashara wadogo kama ilivyo kwa uwekezaji mkubwa
  • TRA hawana muda wa kufikilia TIN zenye msamaha wa kodi kwa wafanya biashara wanaoanza!
  • Malipo ya pango la biashara lazima mfanyabiashara ukalipie 10% ...wakati aliyetakiwa kutoa hiyo ni mwenye nyumba ulipo panga wewe! Lakini kwasababu mfanyabiashara unashida wanakubana wewe!
  • HATA mtu hujafanya biashara mwaka huo wa usajili TRA ikifikia kufaili return za mwaka lazima mahesabu yako yahakikiwe na kampuni ya uhasibu editor firm ambako gharama zipo juu sana hadi laki tano au zaidi hata kama UNAFAILI NIL (yaani hujafanya biashara), sijui kwanini Sera na sheria ya TRA wasingeweka utaratibu mrahisi kwa biashara changa ufaili hata kwa mhasibu personal wa kawaida kwa miaka 5 ya kwanza
  • Halmashauri na manispaa pasipo kukupa msaada wowote, ukifuata leseni wanakutoza pesa kuanzia elf 80 hadi laki tano kulingana na biashara yako! Tena kibaya zaidi unawafuata ofisini kwao ukapange foleni hata juisi ya kufuta jasho la nauli kwa kuwapelekea pesa ofisini hawakupi, sasa ebu jiuloze pesa zote hizo manispaa wanachukua kwa mchango UPI waliompa mfanyabiashara kama siyo dhulma?
  • Malipo ya leseni yanaumiza sana kwasababu kwanza hawajishughulishi hata kukupa elimu ya biashara, hawakutaftii wateja hawakupi ofa yoyote zaidi ya kukukamua tena wakiwa ofisini kwao.
  • Ukifanikiwa kufungua matawi ya biashara yako, ajabu kila manispaa utaombwa kulipia mfano! Kama leseni ni tsh 350000 ukiweka tawi kila wilaya utatakiwa kuilipa pesa hiyo kila wilaya utazani ni nchi tofauti wakati uko Tanzania moja
  • Yote tisa kote pesa wamechukua pasipo hata grace period, ukitaka kuweka bango la kujitangaza biashara yako watakuja Kudai ULIPIE BANGO Lako la kujitangaza, wanakuchaji kwa square meter.
Yapo mengi sana wafanyabiashara tunadhulumiwa na selikali kuna wakati natamani katiba iseme wazi kabisa! KIONGOZI YOYOTE LAZIMA AWE MFANYABIASHARA Mwenye biashara ya jina lake iliyofanya kazi angalau miaka 10 na kuendelea! Labda itasaidia kutuelewa tunavyoumia wafanyabiashara.

Manispaa wanapata pesa za bure sana na sielewi kwanini LESENI ZAO zisiwe bure au wapunguze anagalau bei ya juu kabisa kwa duka,yard au kampuni isizidi lakimoja!

Na ikiwrzekana makao makuu ya ofisini ilipo ndipo inatakiwa kulipiwa leseni na huko kwenye matawi ipelekwe nakala au walipie kwa nusu bei!

Ndiyo maana VIONGOZI wakitumbuliwa au kustaafu hutamani tena teuzi kwasababu mazingira ya biashara wanajua yalivyo magumu sana!

View attachment 2330892
Tozo ni mchango wa maendeleo, na kodi ni kwa mujibu wa sheria!
Inabidi tuwakumbusha watunga sheria wetu, hawa wengine tunawaonea bure maana ni watekelezaji wa sheria zilizotungwa na bunge
 
Tozo ni mchango wa maendeleo, na kodi ni kwa mujibu wa sheria!
Inabidi tuwakumbusha watunga sheria wetu, hawa wengine tunawaonea bure maana ni watekelezaji wa sheria zilizotungwa na bunge
Bunge la wananchi, lakini maslahi ni yetu hayasikilizwi
 
Kuna wakati unapata stress mpaka basi ila ndio hivo huwezi kuacha.
Mbaya zaidi ukute unafanya zile biashara ambazo mpaka ufanye lazima uwe na kibali ndio utajua hujui.
Na wasione sehemu kuna fursa ya kupata pesa watakuandama hao wala hawana huruma yaani wanapokezana au kuambiana huku wakijifanya wanakusaidia upate ahueni kumbe wanakutafuna.Hao hata biashara ya pipi hawajawahi fanya waujue uchungu na msoto wa biashara kazi kupenda vya bure na ndio mana wanakuwaga na mwisho mbaya.
Mtu yeyote anayefanya biashara anaelewa changamoto na lazima amuelewe mfanya biashara mwenzie ila hao ambao hawajui wala hawajawahi wakiona unafanya wanaona unapata sana kumbe masikini tunakaza roho.
Sometimes huwa natamani nipate ajira niwe na mimi nasubiria mwisho wa mwezi kuliko hizi heka heka.
 
Nasikia story ya Hamza chimbuko ilikuwa hivyo
 
Yote tisa wananchi hii mitandao pia inapiga sana hela wanakata mara 12 zaidi ya tozo. Serikali iingilie kati.
Makampuni ya kigeni yanajinufaisha sana.kupitia makato yao.....
 
Yote tisa wananchi hii mitandao pia inapiga sana hela wanakata mara 12 zaidi ya tozo. Serikali iingilie kati.
Makampuni ya kigeni yanajinufaisha sana.kupitia makato yao.....
Wala hakuna msikilizaji
 
Back
Top Bottom