Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,502
- 51,098
Yaani sijui wachumi wa rais Samia ni watu wa namna gani, wako out of touch kabisa na maisha ya mtanzania halisi.
Lakini tatizo kubwa ni kuteua watu wanaojipendekezapendekeza kwa watawala kwa ajili ya ambition binafsi, badala ya kuteua watu ambao wana principles zao, ambao wanawaza faida za maamuzi kwa faida ya wananchi wengi badala ya maslahi yao binafsi
Leo eti kuna kodi ya Jengo ambayo kusheria na kikawaida inabidi ilipwe na mwenye Jengo husika, Lakini leo akina Mwigulu wanasema hapana, Kodi hii alipe Mpangaji kwenye hilo jengo kupitia LUKU pindi anaponunua umeme, halafu eti Mpangaji na Mwenye Jengo watajuana wenyewe kwa wenyewe watarudishianaje hiyo hela!
Yaani hapa Wajibu wa serikali wa kukusanya kodi anatwishwa mpangaji ambaye ni wananchi wengi, eti mwananchi awe ndo mwenye kumlipia mwenye jengo kodi ya jengo lake halafu eti yeye atazireclaim hizo pesa.
Hapa Serikali isitake kutupiga changa la macho, technically wajibu wa kidi ya nyumba serikali imeuhamishia kwa mpangaji badala ya mwenye jengo kwa sababu kwanza
1. Serikali haijafanya survey ya majengo yote nchini ili kujua kila jengo linastahiki kodi ipi ya jengo
2. Nyumba za kupanga wakati mwingine wanakaa mpanfaji zaidi ya mmoja, wakati mwingine kila mpangaji na mita yake, na wakati. mwingine wapangaji wote wanashare mita. Sasa katika mazingira haya ambayo kila mpangaji ana mkataba binafsi na mwenye nyumba convenience ya kuingiza makato hayo ya LUKU kwenye mkataba wa upangaji yanakuwaje rahisi?.
3. Kiwango cha matumizi ya umeme ya wapangaji katika nyumba wanayoshare ni tofautitofauti, Sasa mechanism ya kukukotoa refund kutoka kwa mwenye nyumba imekaaje?
4. Serikali haijatunga sheria kulazimisha refund ya mwenye jengo kwenda kwa mpangaji, pindi mpangaji atakapolipa kodi ya Jengo kwa niaba ya mwenye Jengo pindi mpangaji akinunua LUKU
Kiufupi Samia yeye anakwenda kuchokonoachokonoa angle zote ambazo ziliwapa wananchi unafuu kwenye maisha yao ya kila siku, yaani hapimi consequence za makodikodi yake. Anayafanya maisha yetu kuwa magumu sana.
Hatuwezi kufika kwa mtindo huu