Ukistaajabu tozo za miamala kuna na hili la Kodi ya Jengo kulipwa kutumia LUKU

cotyledon

JF-Expert Member
Aug 25, 2018
914
1,000
WATANZANIA HATUNA UTAMADUNI WA KULIPA KODI, na hatupendi KULIPA KODI. Nchi haiwezi kujengwa bila kodi za wananchi wazalendo,nakumbuka kuna kipindi kodi za majengo zilikuwa elfu kumi (10,000) tu kwa mwaka ila tulikuwa hatulipi/tunalipa kwa shida sana. Naomba tubadirike tuungane na Mhe. Rais SSH kuijenga Nchi yetu.
Kodi ya nyumbani kupitia luku siyo halali. Kwahiyo tuseme wameshindwa kubuni mbinu halali za kukusanya kodi.
 

Deeboyfrexh

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
2,076
2,000
Kodi ya nyumbani kupitia luku siyo halali. Kwahiyo tuseme wameshindwa kubuni mbinu halali za kukusanya kodi.
Wanachokifanya hawa jamaa ni sawa na wewe uwe na noti ya elfu kumi uvunje vunje na kuiweka kwenye mifuko yako tofauti ya surali na koti halafu uje usikusanye sehemu moja ukitarajia hela zitakuwa nyingi
 

Deeboyfrexh

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
2,076
2,000
Habari Greater thinker! Asante kwa uchambuzi, lakini naona umeonyeshwa udhaifu bila kupendekeza suluhisho. Njia zipo mbili na kila moja ina faida na hasara,

1. Mpangaji kulipa na kuwa refunded na mwenye nyumba kama ambavyo mwenye duka nakusanya VAT kutoka kwa mtumiaji kwa niaba ya Serikali. Faida hapa mpangaji atahakikisha kuwa analipa kwa wakati ili kuwa na uhakika wa umeme,kwani ukikatwa ni mwathirika wa kwanza

2. Mwenye nyumba kulipa moja kwa moja kupitia kulipa umeme,yaweza kuwa njia bora ila anaweza kuchelewa kulipa na kusababisha hasara kwa mpangaji. Njia zote zina faida na hasara nadhani tuje na suluhisho kuliko KULALAMIKA MWANZO MWISHO.

Mwisho, niliwahi kusema WATANZANIA HATUNA UTAMADUNI WA KULIPA KODI, na htupendi KULIPA KODI. Nchi haiwezi kujengwa bila kodi za wananchi wazalendo,nakumbuka kuna kipindi kodi za majengo zilikuwa elfu kumi (10,000) tu kwa mwaka ila tulikuwa hatulipi/tunalipa kwa shida sana. Naomba tubadirike tuungane na Mhe. Rais SSH kuijenga Nchi yetu.
Kodi unazilipaje na una kipato kidogo? We uwezo wako kumeki ni 10000 kwa siku familia ile na uache hela ya kesho!
Tungekuwa na uchumi wa hata dollar 15 kwa siku atleast watu wangemudu sababu mtu wa kipato cha chini anamudu kupata 35,000 kwa siku ni hela ambayo hata ukitaka achangie 5000 kwa siku haimuathiri chochote!
 

Chitiva

JF-Expert Member
Apr 15, 2020
352
500
Mi binafsi nilishapata mbinu ya kuhakikisha mwenye nyumba analipa Kodi yake yeye mwenyewe. Ni kumtaka mwenye nyumba atoe Kodi yake ya nyumba mapema atukabidhi halafu tutachangishana na wapangaji wenzangu na ile yake tunaenda kununua umeme. Asipotoa Kodi yake hapati
 

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
4,295
2,000
Kodi hii ni buku 10 kwa mwaka yaani kama mpo wapangaji 4 na luku ni moja kila mtu anatoa buku 2500 kwa mwaka punguzeni kulamika
Wewe na familia yako ni wanufaika wa hiyo Kodi.
Mm na familia yangu tutatumia solar mwanzo mwisho hadi huu ukhanithi utakapoisha.!
 

GANG MO

JF-Expert Member
Dec 6, 2016
2,006
2,000
Hazina hakuna kitu
IMG_20210717_131509.jpg


Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
18,587
2,000
Yaani sijui wachumi wa rais Samia ni watu wa namna gani, wako out of touch kabisa na maisha ya mtanzania halisi.

Lakini tatizo kubwa ni kuteua watu wanaojipendekezapendekeza kwa watawala kwa ajili ya ambition binafsi, badala ya kuteua watu ambao wana principles zao, ambao wanawaza faida za maamuzi kwa faida ya wananchi wengi badala ya maslahi yao binafsi

Leo eti kuna kodi ya Jengo ambayo kusheria na kikawaida inabidi ilipwe na mwenye Jengo husika, Lakini leo akina Mwigulu wanasema hapana, Kodi hii alipe Mpangaji kwenye hilo jengo kupitia LUKU pindi anaponunua umeme, halafu eti Mpangaji na Mwenye Jengo watajuana wenyewe kwa wenyewe watarudishianaje hiyo hela!

Yaani hapa Wajibu wa serikali wa kukusanya kodi anatwishwa mpangaji ambaye ni wananchi wengi, eti mwananchi awe ndo mwenye kumlipia mwenye jengo kodi ya jengo lake halafu eti yeye atazireclaim hizo pesa.

Hapa Serikali isitake kutupiga changa la macho, technically wajibu wa kidi ya nyumba serikali imeuhamishia kwa mpangaji badala ya mwenye jengo kwa sababu kwanza

1. Serikali haijafanya survey ya majengo yote nchini ili kujua kila jengo linastahiki kodi ipi ya jengo

2. Nyumba za kupanga wakati mwingine wanakaa mpanfaji zaidi ya mmoja, wakati mwingine kila mpangaji na mita yake, na wakati. mwingine wapangaji wote wanashare mita. Sasa katika mazingira haya ambayo kila mpangaji ana mkataba binafsi na mwenye nyumba convenience ya kuingiza makato hayo ya LUKU kwenye mkataba wa upangaji yanakuwaje rahisi?.

3. Kiwango cha matumizi ya umeme ya wapangaji katika nyumba wanayoshare ni tofautitofauti, Sasa mechanism ya kukukotoa refund kutoka kwa mwenye nyumba imekaaje?

4. Serikali haijatunga sheria kulazimisha refund ya mwenye jengo kwenda kwa mpangaji, pindi mpangaji atakapolipa kodi ya Jengo kwa niaba ya mwenye Jengo pindi mpangaji akinunua LUKU

Kiufupi Samia yeye anakwenda kuchokonoachokonoa angle zote ambazo ziliwapa wananchi unafuu kwenye maisha yao ya kila siku, yaani hapimi consequence za makodikodi yake. Anayafanya maisha yetu kuwa magumu sana.

Hatuwezi kufika kwa mtindo huu
Angalia tu namma walivyoingia madarakani
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
9,790
2,000
Wakapimwe akili.
Mwenzao Dialo alisema huwa tunachagua vichaa
Diallo ana akili sana! Hivi katika hali ya kawaida, unapata wapi ujasiri wa kumteua mwigulu kuwa Waziri wa Fedha!!

Mtu amekaa kiujanja ujanja na kiupigaji pigaji tu!
 

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
18,020
2,000
1. Serikali haijafanya survey ya majengo yote nchini ili kujua kila jengo linastahiki kodi ipi ya jengo

2. Nyumba za kupanga wakati mwingine wanakaa mpanfaji zaidi ya mmoja, wakati mwingine kila mpangaji na mita yake, na wakati. mwingine wapangaji wote wanashare mita. Sasa katika mazingira haya ambayo kila mpangaji ana mkataba binafsi na mwenye nyumba convenience ya kuingiza makato hayo ya LUKU kwenye mkataba wa upangaji yanakuwaje rahisi?.

3. Kiwango cha matumizi ya umeme ya wapangaji katika nyumba wanayoshare ni tofautitofauti, Sasa mechanism ya kukukotoa refund kutoka kwa mwenye nyumba imekaaje?

4. Serikali haijatunga sheria kulazimisha refund ya mwenye jengo kwenda kwa mpangaji, pindi mpangaji atakapolipa kodi ya Jengo kwa niaba ya mwenye Jengo pindi mpangaji akinunua LUKU
Serikali imeishiwa pumzi, labda sasa waseme ni kodi ya nishati tutawaelewa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom