Misamaha ya kodi na punguzo la tozo katika miamala

Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,402
942
Serikali katika Mwaka mpya wa Fedha 2022/23 imeanza kutekeleza punguzo la tozo katika miamala ya simu katika kutuma na kupokea fedha kwa 43%. (Tozo ya juu kabisa itapungua

Kwa kutambua ukuaji wa sekta ya Sanaa na kujiajiri kwa vijana, serikali inatekeleza suala la punguzo la kodi(with holding tax) katika Tasnia ya Filamu kutoka 15% hadi 10%.

Kwa kutambua kupanda kwa bidhaa katika Soko la Dunia, serikali imewezesha kuondolewa kwa kodi (Zero rating) kwa bidhaa za mafuta ya kula (edible oils).

Kwa kutambua umuhimu wa Sekta ya Kilimo, Serikali imewezesha kuondolewa kwa kodi (Zero rating) kwa mbolea inayozalishwa hapa nchini na mahitaji mengine muhimu ya wakulima, Wafugaji na Wavuvi.

Epuka matapeli wanaotumia mitandao ya kijamii kufifisha kazi kubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kustawisha maisha ya wananchi.
 
Kodi ndo maendeleo pasi kulipa Kodi hakuna maendeleo serikali shika hapo hapo mpaka unyumbu uishe kwa Watanzakiza
 
Back
Top Bottom