Ukiondoa kupita bila kupingwa unakua umeaondoa ununuzi na utekaji wa wagombea kwenye chaguzi. Ushauri, rekebisha Sheria kwa maslahi ya demokrasia

kagoshima

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,638
5,145
Mazee mpo? Naenda kwenye hoja.

Kiukweli moja ya uchafuzi mkubwa wa Democrasia ya vyama vingi ni ununuzi na utekaji wa wagombea wakati wa uchaguzi.

Tumeamua multiparty democracy,ni vyema tukawa serious kidogo. Haiwezekani Tanzania Kila jambo linafanywa kisanii sanii.

Democracy ni kuruhusu raia wachague kiongoz wanayeona anawafaa kuongoza. Kinyume chake imekua ikitokea Tanzania, wenye pesa zao kununua wapinzani wao hivyo kupita bila kupingwa kwa Sheria za Sasa. Hii inatunyima raia kuchagua kiongoz Bora na kuongozwa na bora kiongozi.

Kumbuka ili Taifa liendelee tunahitaji Elimu Bora, siasa safi na uongozi Bora or else we are doomed to fail.
Pia upenyo kwenye Sheria wa kupita bila kupingwa umekua ukisababisha utekaji wa wagombea, kunyanganywa na kuchaniwa form kwa wagombea hata mauaji ili mtu apite bila kupingwa kuwa diwani au mbunge.

Kwenye marekebisho ya Sheria tuondoe Sheria ya kupita bila kupingwa ili

1. Tuondoe Hila za utekaji, rushwa, na rafu zingine kwenye uchaguzi

2. Raia tuongozwe na diwani, mbunge ,raisi tuliye mchagua kidemocrasia kwa kura zetu.

3. Kiongozi aliyechagualiwa ajisikie fahari ya kuongoza raia waliompigia kura hivyo kuwatumikia kwa dhati

Nawasilisha wadau
 
Back
Top Bottom