Ukiitegemea biashara yako mpya ikulishe, ikulipie kodi ya nyumba na kadhalika, jiandae kuanguka

Bishara yoyote inaweza kukutoa ukitumia akili vizuri. Najua kuna jamaa ana turnover ya 400M kwa mwaka kwa kuuza lollipop (Pipi za kulamba).
 
Huo ndiyo Ukweli Mkuu!

Nilianza biashara ya M-Pesa kwa miaka 6 iliyopita. Niliweka pesa kama Million 2 tu, baada ya kulipia frame, leseni na kila kitu. Lakini, sikuwa na wazo lolote la kuniletea faida kwa wakati huo.

Mwezi wa kwanza katika biashara nilipata 36,000 tu. Imagine kama ndiyo nilikuwa naitegemea initoe.

Biashara hiyo ilinipigisha kwata miezi nane bila return ya maana. Hata mdada aliyekuwa akinisaidia nammegea sehemu ya Mshahara wangu.

Baadae hali ikachachamaa, mambo yakaanza kuwa mazuri. Angalau sasa malipo ya binti yakaanza kulipwa na Commission. Sipati kitu. Lakini it worth fighting.

Miaka sita sasa, nina mtaji wa zaidi ya Million 40 na sijawahi kutia mia yangu nyingine tangu niweke ile 2M. Imejizalisha mpaka kufika hapo.

Sema nilikuwa sichukui faida. Ikipatikana, narudisha humo humo. 2019 mwishoni ndiyo nikaanza kuchukua Commission inayopatikana huku kiasi kingine nakiacha.

Sasa imagine kama ndiyo nilikuwa naitegemea. Ndani ya miezi mitatu tu hiyo hela ingeshaisha. Kuwa na kipato kingine tofauti kitakachokuwezesha kuishi wewe kama wewe na backup ya biashara yako kama beginner.
This is impressing.
 
Ntakushukuru vipi na hujajua biashara pia!
Bytheway frame ishalipiwa!

kwa ulichosema sijui Kama kinaeleweka.
Yani ili niwe na biashara mpya inabidi niwe na biashara ndogo kwanza!?

kuna biashara isiyogusa maisha!?
Hapo ndio kwenye makosa.
What is that!!?😂

(naheshim wazo lako)

na kwanini kila anaeanza biashara anaita biashara ndogo ndogo!?
Kwanini uanze na fikra ndogo!?

na kama kwako haijafanyakazi haimaanishi wote haijawezekana.

kama uliweka mkakati wako sawa
Ukajua unachotaka hiwezi ita biashara yako ndogo.

kwanza mtaji si pesa Pekee(ingawa ni mhimili mkubwa)
WAZO lako kwanza ni mtaji.
The rest is to get your butt up and work hard

PERIOD.
Jamaa mbona ana point ya wazi mkuu? Alichomaanisha ni lazima uwe na primary business kabla ya kuanzisha secondary business. Uwe na kabiashara au source ya pesa ya kukuwezesha kuwa unakula na kuishi bila kuitegemea biashara mpya ambayo ndio umeianzisha tu!
 
Vipi kuhusu usimamizi wa biashara ukiwa muajiriwa? Wapo walioanguka kibiashara wakiwa waajiriwa na hawakuwa tegemezi wa biashara zoo ila changamoto kubwa ni usimamizi wa hizo biashara zao
Kingine lazma ujue hamna mtu yupo kwa ajili ya kukutengenezea wewe elf 50 halafu umpe sh.3000 kwa siku! Huyo mtu hayupo kwa hio inakupasa ubalance maslahi
 
  • Thanks
Reactions: B51
Kitu pekee ninachoweza kushauri watu katika hili:
1. Lazima ujifunze kutambua business location kabla ya ku inject money.
2. Kama pesa umekopa, make sure marejesho ya hiyo pesa haitegemei ustawi wa biashara yako mpya

3. Persistence, hili ni muhimu sana. Wabongo wengi tunafanya biashara kwa hearsay, fremu A leo utaona ni salon, six months later, fremu A utakuta ni duka la nguo za watoto, 9 months later , fremu hiyo hiyo utakuta imekuwa Restaurant.... yaani unaona kabisa hawa watu waliokuwa wanapita humo hawakuwa na long term business strategy and probably walikurupuka na nje ya mategemeo wakajiona kuwa kumbe ni ndoto.

Muhindi akichukua Fremu , basi anakuwa amefanya research ya long term na short term .... na utamkuta hapo hata baada ya miaka 10 na wajukuu zake pia watakuwepo. Na itafika mahali watu wanatoka mbali kuja hapo kupata huduma.

Kwa Experience yangu , a business unatakiwa kuanza kuijudge baada ya miaka 2 yaani 24 months , ndani ya kipindi hicho utakuwa pia wateja wauhakika that is wanakuja hapo kwa ajili yako na service zako.

Sasa wabongo anataka kuijudge biashara baada ya miezi 2, unapotea.

4. Jua mtu wa kumuweka kwenye biashara yako. Hili watu wanalipuuza. Some people hawana mvuto wa kukaa dukani nikiwa na maana kuwa they are irritable na hawana convincing kwa mteja. Unaweza ukaona hakuna biashara kumbe uliyemuweka au wewe Mwenyewe uliyekaa hapo dukani hufai kukaa dukani , huna mvuto kwa wateja or unachukiza Tu jinsi unavowasiliana na wateja hata kama huwajibu hovyo, I mean you are not presentable to customers.

5. Kama Una means , anzisha biashara kwa pesa yako , baada ya miezi kadhaa ya kuona movement na challenge na fast moving items, ndiyo ukakope bank purposely based on the weaknesses you have noticed kwa kipindi husika.

6. All in all biashara ni risk taking , usiogope ku fail , kufail ndiyo kupata Experience Na itakusaidia snaa kwa baadae.

Halafu haya maisha usichukulie SERIOUS sana; end of the day we all gonna die ... and leave everything. So we jaribu unapoweza, ukifeli jifunze, lianzishe tena songa mbele , it is just a game , play it and don’t take it too serious.... kupitia game hiyo , utakuja Tu kupata majibu ya maswali yako na utatoboa.

Keep playing the game , never stop eti kwa kuwa umefeli game ya kwanza.
Persistence ndio ngumu hasa kwa wabongo ambao anataka akifungua biashara ianze kuingiza faida baada ya miezi miwili tu 😂! Apate hela ya kuendea Dubai shopping matokeo yake zile faida za laki kwa siku hazionekani kama alivyofungwa mota anaamua kushut down business!
 
This is impressing.
Be inspired!.

Screenshot_20210812_152025.jpg

Hiyo hapo juu ni Commission ya mwezi July!.

Hapo sijaweka za Voda ambazo direct hushukia kwangu.

It is a business that only made a 36k commission at first.

Baada ya makorokocho yote ikiwa kulipa wafanyakazi, kodi na kila kitu, 5 Million profit is a must.

Mind u, hata kazi bado sijaacha and I'm not planning to.
 
Nimefungua fremu ya viatu vya watoto na wanawake siku 8 sijauza hata pair 1, frame laki 2x 6 months!! Naona nyotanyota! Mzigo (gharama)1.5m, leseni+bills (bado sijapigia hesabu). Halafu utashangaa TRA sijui manispaa na ving'ora.
Marketing strategies zako zikoje mkuu? Biashara haiitaji ukimya biashara inahitaji "makelele" I mean kutangazwa usifungue biashara kinyonge..
 
Marketing strategies zako zikoje mkuu? Biashara haiitaji ukimya biashara inahitaji "makelele" I mean kutangazwa usifungue biashara kinyonge..
Viatu vya mtumba ukatangaze ITV? Fremu ipo uswazi nyomi Kama yote tatizo hela
 
Be inspired!.

View attachment 1889601
Hiyo hapo juu ni Commission ya mwezi July!.

Hapo sijaweka za Voda ambazo direct hushukia kwangu.

It is a business that only made a 36k commission at first.

Baada ya makorokocho yote ikiwa kulipa wafanyakazi, kodi na kila kitu, 5 Million profit is a must.

Mind u, hata kazi bado sijaacha and I'm not planning to.
Congrats mkuu, nina swali business yako ya uwakala ipo moja tu, au ipo zaid ya moja, nkiwa na maana je una sehemu mbali mbali umeweka ofisi ya uwakala?
 
Halafu bado kuna machuma ulete nao wanazengea zengea hapa kwenye tuduka twetu twa mabanzi
 
Back
Top Bottom