Lavit
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 13,136
- 27,083
Hizi biashara za kuuza bidhaa zinataka moyo sana..Kuna jirani yangu yeye alifungua mini-supermarket daily anatupa vitu vilivyooza/haribika hajawahi kuuza hata mkate 1pc. Kweli biashara hizi tuwaachie Wapemba/wahindi/waarabu sisi waswahili tuendelee kupiga domo Kama Msemaji (aliyetimuliwa)
Mimi kuna miaka nilikuwa na biashara ya hardware, nikabebwa na ule ujinga wa vitu vya hardware haviozi, ndio haviozi ila je mzunguko upo?
Kuna items niliweka toka nafungua duka mpka limekuja kunishinda hazijauzika kabisa na hapo ni kama miaka mitatu.
Hizi physical business zimenipa uoga sana, hata kama nitarudi kwenye biashara basi nitafanya services na sio kuuza bidhaa.
Ila cha ajabu watu humo humo wanatoboa na wanafanya mambo makubwa kabisa ukiwa na imani ndogo utasema wanaroga .