mchagger
JF-Expert Member
- Oct 15, 2019
- 861
- 1,049
Changamoto inayokabili huwez Anza biashara ukiwa umeshibaHabari wakuu,
Ukosefu wa ajira serikalini, taasisi mbali mbali, viwandani n.k imekuwa ndio chanzo cha vijana wengi mpaka wazee kukimbilia kwenye biashara,
Wengi tunapoanza biashara huwa hatuna uelewa wa kutosha, maarifa tunayoyapata kwa kuulizia ulizia kwa watu, mtandaoni au kwa ndugu na marafiki huwa hayajitoshelezi, hili jambo ni hatari sana.
Unakuta mtu ameanzisha biashara yake mpya hapo hapo anaitegemea imlipie kodi ya fremu, umeme, TRA, taka, ulinzi, kodi ya anakoishi, maji, chakula, vocha, usafiri n.k,
Ukiona upo kwenye hali kama hiyo jua moja kwa moja ushaanguka, siku si nyingi utafilisika au kuanza kuhisi unachawiwa kumbe tatizo niwewe mwenyewe,
ukitaka kuanzisha biashara hakikisha una kazi (ajira), kipato kingine cha ziada cha kukulisha, kukuvisha, kukulipia kodi ya nyumba, vocha n.k hapo utatoboa mapema tu ndani ya miezi hata 9 au 10,
ila ukianzisha biashara wakati unanjaa, au umepigika ndugu wamekuchangia mtaji wa milioni 3 au umekusanya pesa ukaacha kazi, au umefungua biashara kwa pesa za pensheni baada ya kustaafu tegemea anguko, kufirisika kuhama mtaa au kurudi nyumbani kwenu. Ndio maana waswahili wanasema mwenye nacho huongezewa
Hii ndio sababu inayopelekea biashara nyingi mpya kufa haraka hata bila kumaliza miezi 8 au mwaka,
NB: USIANZISHE BIASHARA WAKATI UKIWA NA NJAA. Akili ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO
Nawasilisha