Jinsi ya kuacha ajira na kujiajiri bila kujutia mbeleni

pmanlima

New Member
May 13, 2022
4
9
  1. USIACHE AJIRA KABLA YA KUJITATHIMINI KWANZA: hapa namaanisha ujiulize je ajira yako inakupa furaha au inakukera na unaenda tu ili uweze kukidhi mahitaji yako ? na je ukijitathimini ukiwa uzeeni kwako baada ya kuendelea na hiyo ajira bila kujaribu kujiajiri utajilaumu au hautajilaumu? basi kama inakupa furaha na hautojilaumu uzeeni basi endelea nayo hiyo kazi na unaweza kuishia kusoma hapa. ila kama majibu ni tofauti basi soma kipengele kinachofata.
  2. USIAMKE ASUBUHI HUJUI UNAKULA WAPI KWENDA KUFANYA WAZO LAKO LA BISHARA WALA USIACHE AJIRA GHAFLA BIN VUU KWENDA KUJIAJIRI: hapa ntatumia mfano mmoja wa wagonjwa, kuna baadhi ya magonjwa unakuta mtu anatumia dawa zaidi ya moja kwa pamoja yaani inaanza moja inapandishwa dozi kila baada ya muda flani afu dozi ikifika juu kabisa inaanza kushushwa afu dawa ya pili inaanzishwa na kupandishwa dozi kama ya mwanzoni . kwa hiyo kama hapo juu kwenye mfano katika swala la ajira na kujiajiri unatakiwa utafute ajira au kitu cha kukulisha kwanza hata kama sio ajira utulie nacho kwa muda hata kama unakichukia ukiwa unajikuza kiuchumi. ila usifanye utoto na upunguwani wa kuamka tu asubuhi siku moja kwenda kufanya wazo lako la biashara ambayo hujawahi kuifanya afu utegemee kula humohumo aisee utakufa njaa na ubongo wako ulokupa hilo wazo utalisahau wazo lenyewe au kama uko kwenye ajira tiyari usiache tu ghafla bin vuu ukaingia kwenye kujiajiri kwa hisia bila akili au kwa kusikia watu wanakwambia eti woga wako ndo umasikini wako bali unatakiwa utumie ajira yako kuanzisha biashara pembeni na kuilea mpaka iwe imara kama ajira yako kwa maana kuwa inakuingizia kipato ambacho kinalingana na ajira yako na hakiporomokiporomoki ovyo ovyo kwa muda wa angalau miezi 6-12. baada ya hapo sasa unaanza kujitoa kwenye ajira polepolena kuongeza nguvu kwenye biashara na mwishoni unaondoka jumla. kuhusu woga ukweli ni kuwa woga ni hisia ambayo kila mtu anayo kwanini??? kwa sababu ina matumizi yake usidhani woga ni ujinga .kwa hiyo utumie woga wako badala ya kuwa mtumwa wake wala usiache kuusikiliza woga wako unajaribu kukwambia nini afu uishie kujuta mbeleni.
  3. USIACHE AJIRA KAMA HUWEZI KUTENGA PEMBENI HELA YA KUENDESHA MAISHA YAKO BILA KUJIBANA KWA MIEZI6-12. kwanza kabisa hakikisha unapiga hesabu na kuanza kusave hela ya matumizi yako yote ya kutosha miezi 6-12 kuanzia kodi chakula mavazi umeme mafuta maji ada za watoto na kila kitu hadi cha sh. 100 bila kusahau bima ya afya kwa familia yako yote . afu hii hela iweke kwenye savings account.kama huwezi kuipata hii hela inamaanisha kuwa ikitokea biashara yako ikafeli basi maisha yako yatakuwa ya msoto au yakuanza kujibana na kukopa na utaanza kuingiwa na wasiwasi na majuto ya kuacha ajira pamoja na kushindwa kuwa na utulivu wa akili na muda kwenye biashara yako ili kutatua chamgamoto zake na kuisimamisha tena maana utakuwa bize kutafuta namna ya kulisha familia. lakini kama uliiweka pembeni wala hutaanza kuwalisha watoto wako chakula tofauti na cha mwanzo au kuwahamisha shule au kuhama nyumba au kuanza kupanda daladala tena kukopa au kuchekwa na marafiki na wafanyakazi wenzako wa zamani.
  4. ACHA KAZI BILA UGOMVI WALA KUMTUKANA BOSS. baada ya biashara yako kuwa stable kwa miezi 6-12 na wewe kutenga hela ya matumizi yako ya miezi 6-12 then utakuwa huna sababu za kukuzuia kuacha kazi jumla
  5. USIBWETEKE NA BIASHARA YA AINA MOJA TU HATA KAMA INAKULIPA MAMILIONI KWA SIKU ANZISHA BIASHARA TOFAUTI KABISA NA HIYO YA MWANZO HATA KAMA INAKULIPA 5000 kwanini??? sababu ni ndogo tu maisha ya hapa duniani kwetu yanabadilika sana hata kama wewe kwako unaona uko vizuri tu ni kwa sababu tuko watu wengi sana na zamu yako bado haijafika kama unakumbuka kuna watu walikuwa na hela chafu ila alivoingia tu rais mpya wakawa wanalalamika kuliko hata masikini kwanini??? kwa sababu walikuwa wamenogewa na mahela yaliyokuwa kwenye biashara yao moja tu kwa hiyo wakawekeza hela yao yote huko then rais alivyokuja na sera zake baadhi ya biashara ziliathirika kiasi kwamba kama ulikuwa una biashara ya aina moja tu inakula kwako. ko hakikisha baada ya kuacha kazi ndani ya miezi 6-12 mingine umeanzisha biashara nyingine tofauti kabisa na ile ya mwanzo (diversification). kwa maana kuwa kama ulikuwa unauza nguo anzisha chakula ,hapa simaanishi anzisha duka la nguo sehemu nyingine , hilo unaweza anzisha hata kumi ukitaka maana moja likiungua moto mengine yataendelea kukupa hela ila lakini nachomaanisha utakuwa salama zaidi ukichanganya aina za biashara ili hata kama corona ikiingia mzigo wa nguo ukashindwa kuletwa kwa muda toka china basi mgahawa wako wa chakula ambao hautegemei china unaendelea kukupa hela hata kama hailingani na duka la nguo. na usiishie mbili nenda mpaka biashara 6-8 kulingana na uwezo wako wa kumanage kiufupi usimalize mwaka bila biashara mpya kama nyingine zinafanya vizuri lakini pia usiwe nazo nyingi kupitiliza.
 
Pia usisahau kuangalia akili yako kama imekaa kibusiness, not all people can fit in the business world as it requires creativity, attitude, appearance, discipline and so forth to determine ones success in the future.
Yeah umeongea kitu cha msingi hapa ni kweli kuwa kuna baadhi ya traits mtu anazaliwa nazo katika haiba (personality) yake kama creativity attitude na discipline ambazo huwa ni ngumu kuzibadili especially ukubwani ingawa nyingine kama appearance unaweza badili hata kesho ukitaka.

Lakini pia ni muhimu sana especially kwa watu creative kupitiliza kuwa makini haswa na hii njia nliyoiandika hapo juu maana hawa ndo wahanga haswa wa kufeli kimaisha kisa creativity yao. ahsante
 
Kuna biashara ambazo hazihitaji uwe involved muda wote, mfano umemkodisha mtu gari akuletee hesabu. haitakuhitaji siku nzima uwe kwenye biashara. utafanya ukaguzi wa chombo mara chache tu na kusubiria hesabu while doing other issues.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom