Rais Samia Ingilia kati. Kodi zinazolipwa na wananchi zimezidi na haziendani na Miradi ya Maendeleo inayofanywa na Serikali

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
302
274
Wanabodi,

Tumeshuhudia nguvu iliyotumiwa na serikali katika kuhakikisha kwamba kuna tozo kwenye miamala ya kielektroniki inayofanywa na wananchi. Hii inaweza ikawa njia ya serikali kutanua wigo wa kodi ya kuwa wezesha kufanya shughuli zingine za ziada ambazo zinaweza zikawa na manufaa kwa wananchi.

Lakini je, kodi hizi za ziada zinatumikaje na zinaleta manufaa kwa wananchi kwa njia zipi?

kwanza kabisa tukubaliane kwamba mwananchi yeyote wa nchi hii analipa kodi nyingi sana ambazo zinaweza zikawa za moja kwa moja au kwa njia ambayo siyo za moja kwa moja.

Kama umeajiriwa kwenye shirika lolote, utakuwa unalipa "Pay as you earn (PAYE)" na katika shughuli zako zingine ambazo hazina uhusiano na ajira yako, utakuwa unalipa kodi zingine. Kwa mfano: kodi ya majengo, kodi kila unapo nunua bidhaa zozote, kodi kila unapo nunua vocha za simu, kodi kila unapo nunua kifurushi cha intaneti, kodi kila unapo hamisha fedha kutoka kwenye akaunti yako ya benki kwenda kwenye akaunti yako ya M-PESA, tigo pesa n.k.

Hata ukinunua kitu chochote kutoka kwa mtu mwenye biashara yake, hata mwenye biashara lazima naye alipe kodi kulingana na mauzo yake. Kodi kila unapo nunua umeme, kodi kila unapo nunua pombe, kodi kila unapo nunua mafuta, kodi kwenye pensheni yako utakapo staafu, Kodi kila unaposhinda bahati nasibu na kadhalika.

Kwa haraka haraka ni rahisi sana kuona na kuelewa kwamba karibia nusu au zaidi ya mapato ya watanzania yanarudi serikalini. Kitu ambacho nimezidi kutafakari na bado sijapata jibu ni kama mapato haya yanatumiwa kwa ufanisi zaidi kuhakikisha kwamba wananchi wanafaidika kwa njia moja au nyingine.

Kila mwaka, serikali huwasilisha bajeti bungeni katika mchakato ambao huweka wazi matumizi ya serikali kwa kipindi hicho. Kitu cha kushangaza ni kwamba serikali yetu bado haiwezi kumudu kugharamikia bajeti yake kila mwaka na pia kodi katika sekta mbalimbali na bidhaa tofauti tofauti hupanda karibia kila mwaka katika njia inayotumiwa na serikali kuongeza mapato na kutanua wigo wa kodi kwenye sekta ambazo hazikuwa zinatozwa kodi katika kipindi cha awali.

kila mwaka kuna asilimia fulani ya mfumuko wa bei na kwasababu hiyo, ongezeko la kodi kwenye bajeti na ongezeko la mishahara haiendani na uhalisia uliopo mitaani. Je, huu ni ungwana?

Na kama serikali ina mantiki ya kuweka kodi hizo je fedha hizi zote huelekezwa katika miradi ipi?. Ni kweli, kodi inayo kusanywa na serikali haiendani na miradi ya maendeleo inayofanywa.
 
Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii..
FbUWVzSWQAEIVvh.jpg
 
Siku hizi imekuwa ngumu kutofautisha kati ya kodi na tozo kipi kinafanya nini, na huu mkanganyiko ndio unatumiwa na yule mjanja kutupiga..

Lazima tuambiwe kila mwezi wanakusanya tozo kiasi gani, na matumizi yake yatakuwa yapi, huu ukimya uliopo hapa naamini pia unatoa mwanya wa kuibiwa.

Rais nae yupo kimya tu, hao anaowaita wanangu sasa ajue wanamzunguka wanatuumiza watanzania, nao wanamjaza kichwa kwa kutuambia watanzania tumuombee Rais.
 
Tatizo mmejikita kwenye umbea na siasa za chuki mtashituka mnakamuliwa mpaka kodi za ndoa nyie endeleeni kujifanya wafia chama.
 
Kutoka mshahara ambao ni 100% kabla ya makato, anza sasa kutoa hizo.

HSELB - 6%
NHIF - ..%
Social Funds - 10% or 5%
Workers - 2%
Paye - 7% to 30%
VAT - 18%
EWURA - ..%
REA - ..%
TOZO zote - ...%
Jengo - ..%

Na katika zote hizo, ambapo si ajabu mzani ushaelemea upande wa pili tayari, hakuna inayomuhudumia mtanzania vile anavyostahili.

Matibabu hovyo, umeme ovyo, njia ovyo, mafao ovyo, VIONGOZI ovyo, ELIMU ovyo n.k
 
Ukiwa unapata KILA kitu bure ni ngumu Sana kujua magumu ya wengine
 
Kiujumla wamekosa ubunifu nje ya kukamua wananchi, mbona vyanzo vya pesa vipo vingi Sana wala uhitaji kodi au tozo kuendeshea nchi ikiwemo maendeleo.
 
Serikali imesema imepunguza tozo mbali mbali na pia kutoa nyongeza ya mshahara kwa 23%, bado hamridhiki na bajeti mlioipitisha wenyewe ?

images - 2022-08-29T193449.612.jpeg
 
Kodi na tozo ni moja ya tools zitumiwazo na watawala kwenye nchi za kiafrica kuwafanya wananchi wao wawe masikini Ili waweze kuwatawala, watawala wa kiafrica hawana confidence ya kuwatawala walioshiba. Kwa macho ya kawaida wanahubiri maendeleo lakini indirect way hawamaanishi maendeleo, thus wanaweka mazingira magumu ya wananchi wao kuweza kufanikiwa mfano halisi ni kodi ya uagizaji vitu vinavyokuja kuchochea ukuaji uchumi ikiwemo vitu vya uzalishaji mfano raw materials, magari ya biashara, nk
 
Back
Top Bottom