Hio ya flash kuwa na size ndogo kuliko iliyoandikwa kwenye flash mfano 4Gb kuwa 3.7Gb sababu yake ni kama ifuatavyo;
Nitatumia hesabu ndogo mfano kwanini 1 TB inakuwa na usable space ya 931 GB?
Mtengenezaji ametengenesa flash inayo kuwa na 1,000,000,000,000 bytes.
Lakini kwakuwa computer inaitambua 1KB kama 1024 na sio 1000 bytes then naafasi (storage) halisi itapungua na kuwa ndogo;
Tunafahamu kuwa:
1 TB = 1000,000,000,000 Bytes
Lakini kwenye computer, 1000,000,000,000 bytes = 1000,000,000,000/1024 KB. = 976562500 KB.
Vilevile ukichukuwa;
976562500 KB = 976562500/1024 MB = 953674.32 MB.
Alafu itakuwa

953674 MB = 953674.32/1024 GB = 931.32 GB.
1 GB = 1024 MB
1 MB = 1024 KB
1 KB = 1024 B
Hence 931GB
Ndio maana flash drive yenye storage space ya 1Tb storage yake halisi ni 931 GB.
Naomba kuwasilisha na nipo tayari kukosolewa ili nifahamu zaidi.
Sent from my TECNO PR651H using
JamiiForums mobile app