Ukifuta picha kwenye simu zinakwenda wapi?

Ukifuta picha kwenye simu zinakwenda wapi?

Ukifuta yaani "delete" picha ni kama umeificha tu kwenye simu na unaijulisha simu yako kuwa hiyo nafasi inayotumiwa na hiyo picha inaweza kutumika kuhifadhi kitu kingine. Hiyo picha inaweza kurudishwa kwa kutumia programu mbali mbali, njia pekee ya kuifanya hiyo picha isiweze kurudishwa ni kama ume delete hiyo picha na sehemu (space) iliyokuwa inatumika na hiyo picha ikatumika na faili lingine. Kuna programu zinazofuta kabisa "erase" file, hizo huchukua muda mrefu maana hufuta hiyo picha na kuandika data nyingi kwenye simu au kompyuta ili kupunguza uwezekano wa hiyo picha yako kurudishwa.

Nakumbuka zamani nilikuwa nasaidia watu walioformat flash disk au kufuta file kimakosa, hatua ya kwanza ilikuwa ni kuhakikisha haweki kitu chochote kwenye hiyo flash, kuna programu ukiweka file zote zinarudi.
Ila file zingine nasikia zinarudi zikiwa zimeharibika kiasi flani. Niliwahi pewa mfano uichukue karatasi ukunje sana the uje uikunjue haitokuwa sawa kama awali.
 
Nilikuwa nafanya kazi photography moja hivi town uwa tulikuwa tunasafisha picha, tunapiga piga, tunatengeneza frame za picha na mambo mengi tu ya edit na nk

Nilikuwa nipo reception sometimes natoka naenda operator room, kuna siku kaja mdada akawa anatafuta baadhi ya picha aziprint palee oficen kwetu Na akashindwa kuzitafuta yeye mwenyewe

Akanipa sim nikaiunganisha na laptop kupitia wire cable kazi ikaanza ya kuzitafuta picha zake, wee si ndio nikafika sehemu nikakuta amejichukua picha na video za utupu wee ilikuwa hatari maana tulikuwa tunaangalia wote kwa pamoja tulipokuwa tunatafuta

Alichukua mkono wake kwanza na akauweka begani kwangu na akanambia, sorry kaka angu na kuanza kujielezea kuwa alishazifuta zote na sim aliifrash, akaniomba nimfutie tena na akaniomba nisizicopy, nikamwambia asijali kwani mm nipo kazini na siwezi fanya chochote kibaya na akaniombaga namba yangu ila sikutakaga mazoea nae kabsa

Taarifa zako kwenye sim hazifutiki maana kuna program maalum za kuzirudisha hata kama ukizifuta vipi? Recover zipo za uwezo tofaut za kupata chochote kutoka kwenye sim yako hata kama ukifuta

Be careful
Ndiomna kuna watu huwa wanatumia sim mpaka ife alafu wanaihifadhi tu[emoji23][emoji1787] hizi sim zina mambo mengi mtu kajipiga mapicha ya uchi kisha kafuta kumbe bado zipo!!

Wadada badilikeni
 
Habari wadau wa JF!

Naomba kuuliza kwa yeyote aliye na ufahamu juu ya hili. Hivi tukifuta PICHA kwenye Simu huwa zinakwenda wapi?

Kuna PRIVACY kweli kwenye vifaa hivi?

Msaada kwa anajua
mwaka jana niinunua pixel 4 nikafutaga picha zangu zote nlizopoga na ile sim mpaka google.

last month nmenunua pixel 6pro naenda kwenye gallery nakuta picha zangu zote zipo
 
Ndiomna kuna watu huwa wanatumia sim mpaka ife alafu wanaihifadhi tu[emoji23][emoji1787] hizi sim zina mambo mengi mtu kajipiga mapicha ya uchi kisha kafuta kumbe bado zipo!!

Wadada badilikeni
😁😁😁
 
Mara nyingi, picha zinapofutwa kwenye simu, zinahamishwa kwenye folda ya takataka (trash folder) au kwenye folda ya kufutwa (deleted folder) badala ya kuondolewa kabisa kutoka kwenye kumbukumbu ya simu. Hii inamaanisha kwamba picha hizo bado zipo kwenye kumbukumbu ya simu kwa muda fulani kabla ya kufutwa kabisa.

Hata hivyo, baada ya muda fulani, picha hizo zinafutwa kabisa kutoka kwenye kumbukumbu ya simu na huwezi kuzipata tena. Kwa hiyo, ni muhimu kufuta picha zako za kibinafsi kwa makini na kuhakikisha zimefutwa kabisa kutoka kwenye kumbukumbu ya simu.

Kuhusu usalama wa faragha kwenye simu, kuna hatua mbalimbali za usalama ambazo unaweza kuchukua ili kuhakikisha faragha yako imelindwa. Kwa mfano, unaweza kuweka nenosiri au kufunga skrini ya simu yako ili kuzuia watu wasiweze kupata ufikivu kwenye data yako ya kibinafsi.

Kadhalika, unaweza kufunga programu za usalama kwenye simu yako kama vile programu za kuondoa virusi na programu za kufuatilia utendaji wa simu yako. Hii itasaidia kuzuia au kugundua matumizi yasiyoidhinishwa ya faragha yako au uvamizi wa faragha.

Kwa hiyo, faragha kwenye simu inaweza kulindwa kwa kuchukua hatua za usalama na kufuta data yako ya kibinafsi kwa makini.
 
Mkuu vip kwa maana Kuna recover app je haziwezi rudishia hivyo vitu vilivyo futika
 
Mfano program gani
Kwa PC tool kama Easeus data recovery na Disk Genius Data Recovery na Disk Digger zinarudisha mataka taka yote uliyowahi hifadhi kwenye PC yako toka umeinunua ila endapo tu kama HDD hujaiformat zaidi ya mara 5.. Hata hizi flash na memory card ukiformat zaidi ya mara 5 ukuja kurecover data usitegemee zitarudi zote, mostly zitarudi ulizofuta recently tu, kama haijafikia idadi ya hizo formats hapo since imetengenezwa na kuanza kuwekewa data ukirecover zitarudi...
 
Asante, na kwa simu?
 
Back
Top Bottom