Wewe unaelewa nini kuhusiana na storage?
Unadhani kwenye pc au simu au server kuna shimo la taka ukiambiwa parmanent deleted hizo takataka zinachomwa moto?
Ukiweka content kwenye PC au Simu au server, uwa inapewa address ili iwe accessible na user wa kawaida. Uki delete, iyo content inapewa address ambayo wewe user huwezi access hiyo content.
Parmanent deleted inamaanisha hiyo content ya kwenye simu wewe user wa kawaida huwezi access. Ila hiyo content ipo kwenye hicho kifaa. Manufactures na hackers wana access na hiyo content kama wakiitaka wanaipata.
Na pia kuhusu watumiaji wa social media kama wakiweka contents kwenye whatsapp, FB, twitter, jf e.t.c wakizifuta huwa address inabadilika ya kwamba user wa kawaida hawezi pata hiyo content ila ukienda kwenye servers za FB, whatsapp, jf etc hizo contents zipo.
Kaa ukijua ya kwamba ukiweka content kwenye devices ya simu au pc au kwenye internet kamwe haifutiki kwenye hicho kifaa. Contents za kwenye internet zipo kwenye servers zinazomiliki hiyo tuvuti au platform.
mfano:
1. Kama umepiga picha au video chafu kwenye simu yako kisha ukazifuta, mimi ukinipa hiyo simu yako nina uwezo wa kuzrudisha hizo picha na video zako. Na pia kama hizo picha na video umeziweka kwenye simu ya samsung, tecno au iphone, hawa manufactures wana uwezo mkubwa wa kupata hzo picha na video zako ulizo futa.
2. Kama umeweka picha au viedo chafu kwenye account yako ya fb, whatsap au jf. Hizo picha ukizifuta kwenye account yako haimaanishi ya kwamba umezifuta kwenye server. Hacker akifanikiwa kuhack facebook au whatsapp au jamiiforums hizo picha au video zako atazipata. Pia wamiliki wa hiyo mitandao wana access ya hizo data zoto mnazoziweka kwenye platform zao.