Ukibahatika kuwa na hela nyingi usizitumie kufanya uovu. Kuna faida gani kuoa mwanaume mwenzio sababu ya pesa?

Matongee

JF-Expert Member
Jun 17, 2023
253
629
WanaJF ninaandika huu uzi baada ya kusoma machapisho mbalimbali mitandaoni na mimi mwenyewe kujionea mambo mengi maovu. Watu wengi wenye pesa wamekuwa chanzo cha maovu mengi sana. Ni kawaida watu wengi wenye pesa kutaka kufanya mambo ambayo ni ufedhuli uliopotiliza. Kuna wengi wanatumia fedha kupora haki za wenzao na kunyanyasa. Kuna watu wengi wako jela kwasababu kuna tajiri fulani alitumia nguvu za pesa kudhulumu haki. Kuna wengine ndo zimevunjwa na matajiri.

Wakati huu wa hili janga la ushoga tumeona wengi wenye hela wakihusishwa. Mitandaoni kuna vijana wanaotuhumiwa kuwa mashoga kwa maana ya kuingiliwa kinyume na maumbile kitu kinachofanya watu wajiulize ni kina nani hawa wanaowaingilia vijana? Kuna vijana wengine wanatajwa kuwa wameolewa, je nani anawaoa vijana wa kiume? MAJIBU MENGI yanasema kuna tajiri/mfanyabiashara/kiongozi wa dini/ mkubwa/mheshimiwa fulani ndo mhusika. Kiufupi wengi wanaotajwa kuharibu vijana ni watu wenye hela nyingi na wengine ni viongozi wakubwa. Hata viongozi wa dini wengi wametajwa. Viongozi wa dini za kimila ndo sijasikia wakitajwa.

Ninakusihi ndugu unayesoma hapa usifanye vitendo viovu baada ya kufanikiwa kiuchumi. Pesa zako unaweza fanyia mambo mengi mema kwenye nchi maskini kama yetu. Najua kuna kitu kinaitwa MONEY FEVER kwamba mtu akipata hela anakuwa na hali flani hivi kama ya kuchanganyikiwa na kutaka kufanya kila kitu ila tafadhali kuwe na balance. Hao vijana wa kike na kiume wenye njaa kali unaweza kuwasaidia kubadili mitazamo yao ya maisha badala ya kuwaingilia kinyume na maumbile na kuwalipa hela.
 
Back
Top Bottom