Uchumi unakufa sababu ya kupotea kwa dola, wafanyabiashara wa nchi za kigeni/wawekezaji huenda ndio chanzo

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
2,546
2,989
Sijui vizuri mambo yanayohusu uchumi ila utaalamu wangu upo kwenye kumanage rasilimali watu pekee na kusuluhisha mambo ila binafsi nimeona malalamiko mengi ya kupotea kwa dola, panda shuka ya bidhaa (inflation) ambapo kwa kiasi kikubwa machungu hubebeshwa mwananchi wa kawaida na kwa bahati mbaya serikali haina dhamira ya dhati katika kuwafanya wananchi kupata unafuu wa maisha.

Imagine serikali yetu inaendeshwa na michezo ya chajuu Tanzania kuna wakandarasi wengi wazawa lakini, bado serikali inatuma vijana wakasomee nje ya nchi kwa lengo la kuifanya nchi ipate huduma stahiki lakini, wanasiasa na watumishi walafi wanajitahidi kuachana na hizi taasisi za ndani na kwenye nje kutafuta wawekezaji wenye gharama kubwa japokuwa wazawa nao wanamatatizo makubwa.

Pesa nyingi zinazoenda kwenye hizi kampuni za nje zinasababisha dola kupanda na hatimaye thamani ya pesa yetu inakufa, bidhaa zinapanda bei athari yake inakuwa kubwa zaidi kwenye ustawi wa nchi, wananchi wakizichoka hizi athari CCM itakuja kukukumbuka shuka wakati kumekucha.

INAKUWAJE TUNASHINDWA? NI KWELI HATUWEZI KUBADILISHA KATIBA AMBAYO NDIYO KINGA YA HAYA MATATIZO?
 
Back
Top Bottom