Ingawa najua Muhungo ni mropokaji na mara nyingi amekuwa si makini lakini kama kweli Mengi amesema maneno haya kumkejeli kwamba alirudia shule amekosea sana.
Naomba tuweke rekodi sawa kuhusu suala la kurudia shule. Miaka ya 1997 kurudi nyuma suala la kurudia shule lilikuwa changamoto kwa watu wengi. Wengi waliokuwa wasomi wa leo hata kushika nyadhifa kubwa serikalini wamerudia shule. HUWEZI KUWALAUMU ila kulaumu mfumo hafifu wa elimu Enzi hizo ambako hakukuwa na shule za sekondari za kutosha hivyo ni watu wachache tu pengine asilimia 5 ya watu waliofaulu mitihani yao walioweza kuchaguliwa kujiunga na shule. Huu mfumo umeanza toka ukoloni mpaka hivi majuzi tu ambapo shule za sekondari zimejengwa nyingi kuwasajili wanafunzi wengi wanaofaulu. Enzi hizo mtu angepata alama 90 na asipate nafasi ya kuingia sekondari. Issue ya pili inayokuja lazima itakuwa kwamba wale waliokuwa na nafasi serikalini walitumia mwanya huo kupitisha watu wao. Hivyo watu wa vijijini waliachiwa nafasi chache kugombania. Ungekuta kata nzima hakuna shule iliyofaulisha mwanafunzi licha ya kwambamba kwenye mitihani ya majaribio wapo waliokuwa wanapata alama A wengi.
Kwa kuwa hakukuwa na nafasi ndio maana unaweza kuona kuwa mtu kama Prof Muhongo aliyekuwa na uwezo mkubwa (Ni kweli licha flaws zake nyingi katika mawasiliano, kitaaluma Muhongo ni moto wa kuotea mbali) alishindwa kwenda sekondari, akarudia, akarudia na kurudia. Wapo wengi wanaofanana na Muhongo laiti kungekuwa na nafasi kubwa ya elimu ya sekondari enzi hizo wengi leo wasingekuwa kama walivyo leo.
Kosa kubwa aliyofanya Mwalimu Nyerere ilikuwa katika sekta ya elimu. Sera ya serikali kugharamia elimu peke yake ilikuwa na gharama kubwa na inaigharimu serikali hadi leo. Ni kwamba sera hii ilisababisha sehemu ndogo tu ya gharama iliyogharimiwa na serikali kufanya kazi hivyo shule zikajengwa chache na vyuo vichache. Njia muafaka ingekuwa serikali kugharamia elimu lakini wazazi pia kugharamia ili kuweka wigo mpana. Matokeo yake wengi wamekosa kuendelea na masomi si kwamba hawakuwa na uwezo lakini kwa kuwa nafasi zilikuwa chache.
Ifike mahali serikali ikubali kuwa ilifanya makosa hivyo wale waliorudia shule Enzi hizo wahalalilishwe kwa kuwa ni mfumo mbovu wa elimu uliowafanya warudie shule licha ya kuwa na uwezo mkubwa kitaaluma. Ni kosa la serikali na taifa kwa ujumla, si kosa la warudiaji.