Prof. Mollel: We are proud of David Kafulila

Prof. Mollel: We are proud of David Kafulila

Mia770

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2024
Posts
341
Reaction score
252
Prof. Henry Mollel, Rasi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Mbeya, anasema kuwa “forum ya Mihadhara vyuoni inayoendeshwa na Kafulila kupitia PPPC ni muhimu sana kwani ni nafasi kubwa kwa vijana wetu ambao hivi sasa tunawaandaa , wanapata elimu hii muhimu"

Prof. Mollel anaendelea kusema “ikiwa kama sehemu ya maandalizi, forum hiyo itaibua mambo mengi yatakayotumika katika kuboresha mitaala yetu, ili wanafunzi wawe wanapata concept mbalimbali ikiwepo PPP kwani ni fursa kwao pia kuelewa PPP ni nini"

Prof. Mollel anaongeza kuwa," kama nilivyokuwa nikisema huko nyuma PPP ilikuwa ni mutedly spoken yaani ilikuwa inazungunzwa lakini siyo kwa namna ambayo ilikuwa na impactive kwenye mindset na kwenye transfer. Anasema kuwa sasa PPP inaanza kuleta tijia katika maisha ya uhalisia na katika kutengeneza maendeleo yenye matokeo kwa Taifa".

Anasisitiza kuwa" tunapopata fursa kama hii ya mhadhara, tunaamini kabisa wanafunzi wetu wanapata a very good understanding ya concept yenyewe, lakini pia understanding ya ulimwengu wenyewe kwa sasa unafikiria wapi. Anasema kuwa wanafunzi wataelewa ukubwa wa concept hiyo katika kutengeneza fursa, na watakapokuwa wamemaliza hapa, wanaweza kuchangia vizuri katika maendeleo ya nchi kwa kuzingatia fursa zilizopo, ikiwemo ya public-private partnership"

Aidha, Prof. Mollel anaeleza "hii inaendelea kuwa fursa kwetu na kwenu ya kumpata Mr. David Kafulila, na anasisitiza kuwa we are proud of him. Anasema pia kuwa Kafulila anaendelea kuwa alumni wa Mzumbe, jambo linalowapa fahari kubwa".

Prof. Mollel anahitimisha kwa kusema kuwa "Siku zote nitaendelea kusema, Mzumbe inaendelea kutengeneza watu wengi sana, wapo wengine ambao wakati mwingine hawatajwi, lakini bado mchango wao unaendelea kuwa mkubwa. Anasisitiza tena: "we are so proud, Mr. Kafulila"

Zaidi ya hayo, Prof. Mollel anasema kuwa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Mbeya wako tayari kuendelea kushirikiana na PPP Centre kwenye masuala ya PPP, wakionyesha dhamira ya chuo kuendelea kushiriki kikamilifu katika kuendeleza ubia kati ya sekta ya umma na binafsi kwa manufaa ya Taifa

 
Porojo tu hizo,
PPP nchi hii Iko miaka yote, watu wanachopinga ni ufisadi kwenye mikataba na kutaka uwazi wa mashirikiano yoyote ya kibiashara kati ya serikali na kampuni binafsi.
 
Nahisi kuna kikundi kinalipwa na Kafulila huku jf ili kumfanyia promotion. Maana nyuzi za kumsifia ni nyingi mnooo. Sasa sijui kwaajili ya nini?
 
Tumbili hii ID ndio umeona ni mpya hatutaijua ila mwandiko wako ni ule ule kujipiga kifua.
 
Porojo tu hizo,
PPP nchi hii Iko miaka yote, watu wanachopinga ni ufisadi kwenye mikataba na kutaka uwazi wa mashirikiano yoyote ya kibiashara kati ya serikali na kampuni binafsi.
Naona hufahamu vizuri dhana ya PPP
 
Back
Top Bottom