Ujumbe wa Mengi katika Twitter, kejeli kwa Prof. Muhongo?

Ujumbe wa Mengi katika Twitter, kejeli kwa Prof. Muhongo?

Reginald Mengi ni CCM na Prof Muohngo ni CCM
Ukikuta wakubwa wa CCM wameanza kupigana ni dalili ya Mataifa kuanzisha Vita na hiyo ndo dalili kuu ya anguko la CCM
well said mjomba
 
umemwaga sera zote hapa
Mkuu unabishana na taahira! Hajui miaka hiyo shule za sekondari zilikuwa chache sana na ushindani ulikuwa mkubwa sana tofauti na sasa ambapo mpaka kata zina shule 2 za sekondari! Hivyo miaka hiyo kukosa nafasi ya kwenda sekondari ilikuwa kugusa tu!! Pia miaka hiyo shule moja ikishindisha watoto wengi ilikuwa inafungiwa miaka karibia 5 bila kupeleka mwanafunzi hata mmoja!

Kwa kifupi sasa hivi magoli yametanuliwa mno ndo maana sasa hivi hatushangai tena tunaposikia hata asiyejua kusoma anaenda sekondari!
 
Apunguze arrogance kwa sababu kuna watu hawajawahi kufeli.
Ndio maana alienda kusomea miamba na sio kule kwenye fani zenye ushindani.
na between the line hiki ndicho Mengi anachomaanisha pia
 
Reginald Mengi ni CCM na Prof Muohngo ni CCM
Ukikuta wakubwa wa CCM wameanza kupigana ni dalili ya Mataifa kuanzisha Vita na hiyo ndo dalili kuu ya anguko la CCM
CCM ni chama cha Mapingamizi, hata hawa wanawekeana mapingamizi sasa
 
Mzee aliwaonea wivu hadi kina joti

Hana akili,huwezi kua na akili timam ukagombana na akina joti sijui nani.

Muhongo kamuweka wazi kwamba ana hela ya juisi,huo ukweli hautaki anabaki kujibaraguza,watanzania hawataki ukweli,ukweli kwao ni tusi.

Mbona bharesa,rostam na muhamed hawamlaumu muhongo au wao sio matajiri?kwa nini mengi?

Zee zima na mipasho ya kike.
 
Apunguze arrogance kwa sababu kuna watu hawajawahi kufeli.
Ndio maana alienda kusomea miamba na sio kule kwenye fani zenye ushindani.

mengi anaota kama anamlenga muhongo hajui ugumu wa sayansi ya miamba.
elimu yake ni kukopa na kuchoma ushahidi
 
K. Lyn au!

Hoja ya Mengi ina nguvu sana hamaanishi uprof wake hebu tuulize watu waliyesoma Prof Muhongo maandiko yake ya kupata master, PhD ana uprof yak kwenye maktaba ipi hapa Tanzania na kama sio hapa nchini kwetu atutajie nchi na maktaba ambapo maandiko yamehifadhiwa huenda akawa miongoni mwa wasomi waliopata kubebwa
 
Hio mpya!

Hivi si ndo huyu alidharau elimu ya Ole-Sendeka kumbe nae kaungaunga tu!

ImageUploadedByJamiiForums1420172526.706107.jpg

Teeeeh
 
Sasa Tanzania kama hujaungaunga shule za kata ungetokaje na wewe siyo mtoto wa mwalimu,miaka ya 90 huko shule ya msingi yote anaweza asifaulu hata mmoja watu wanarudia japo wafaulu,kwahiyo mheshimiwa kurudia primary sishangai
Nafikiri walikuwa wanafaulu, ila hawakuwa wakipangiwa shule za kuendelea kidato cha kwanza kutokana na nafasi kuwa chache. Mkoa mzima shule moja au mbili za sekondari. Mbaya zaidi hawakuwa wanatoa matokeo ili kujua mtu kapata nini.
 
Muongo kurudia kwake mara nyingi ndio kunamnanga kuwa si mwelewa bali anakalili
 
mzee katupa jiwe gizani hapo watakao lalamika wote limeshawapata
 
Mengi Hakutakiwa kutumia maneno yale... Kiungwana, kibusara, kihekima alitakiwa awasilishe ujumbe wake kwa maneno haya "Tujitathimini tulipofika na nyazifa tulizonazo kisha tukumbuke tulikotoka, na tunyenyekee".
 
Jana Mr Reginald Mengi alipost kwenye Istagram yake kwamba kuna Mtu aliwahi kurudia la Saba mara tau na leo ni Le Porofeseri bila shaka akimaanisha Sospeter Muhongo

Je ana hoja>?

Kati ya watu wapuuzi kabisa ni huyo anayeshangaa kuhusu watu kurudia darasa,hapa ninapoweza pia kuamini kwamba wakati mwingine kuwa na elimu ama hela inaweza isiksaidie pia kuwa na uwezo wa kuchanganua mambo!wivu wa kijinga kama alirudia darasa la saba mara tatu na bado akaweza kuupata uprofesa wake kupitia elimu ya darasani basi he is the champ,lkn kama ni huu wa heshima basi hapo mnaweza kumkejeli.
 
Je ana hoja>?

Hana hoja,sikutegemea mtu kama mengi angepost uharo namna ile.

Ok,kama alianguka mtihani mara 3 akabadili jina na shule sasa na profesa,what next?inatufundisha nini?

Ile post imekaa kishambenga sana,utafikiri ni mariam wa migomba wa tbc au gea habib kapost kumbe ni mengi.

Mengi kwa mipasho yuko vizuri.
 
Reginald Mengi ni CCM na Prof Muohngo ni CCM
Ukikuta wakubwa wa CCM wameanza kupigana ni dalili ya Mataifa kuanzisha Vita na hiyo ndo dalili kuu ya anguko la CCM

We acha uongo. Nani aliyekwambia Mengi kada wa ccm? Kwa taarifa yako mengi ni mwanasacoss ya uchagani Chadema.
 
Maana ya Mengi ni kwamba kujikwaa si kuanguka. Kwamba with wasikate Tamara. Ukifanya jambo likashindika endelea kujaribu kwa kusahihisha makosa.
 
Back
Top Bottom