Ujue ufisadi huu POLISI

Naona huyu mwanakijiji mpya tena hapa, mambo inakwendaje tena?!!!!!

Lasthope, kwani benki ilipofungua account hawana hata picha yako? kama ku-block debit card imekuwa shida sidhani kama hiyo bank inakufaa kabisa, angalia ustaarabu sehemu ingine kabisa!
 
Members hili limenisikitisha sana na sina pa kulisemea zaidi ya hapa. nilipoteza wallet yangu8 tarehe 21 ikiwa na id's zangu pamoja na ATM card yangu, sasa nikaenda bank niblock account yangu. Nikaambiwa haiwezekani hadi niende polisi nipewe lost report. Hapo bank wakanipa form ya kunitambulisha huko polisi kama mteja wao. Nikaenda police pale Udsm mlimani , wakaandika maelezo yangu then nikaambiwa inabidi niende kituo cha magomeni au oysterbay nikalipie shilingi mia tano (500) kwa sababu wao hawana mhasibu pale, nipewe risiti niirudishe pale polisi ndio wanipe hiyo lost report ili nende bank kublock account yangu na kuanza process ya kupewa ATM mpya. Kwa kuwa ilikuwa jioni definately nisingemkuta huyo mhasibu, nilivyoenda oysterbay nikaambiwa hawana risiti zimeisha niende magomeni, nikaenda magomeni nikaambiwa risiti zimeisha niende baada ya siku tatu au niende msimbazi, kumbuka siku zinapita sijablock account yangu, mchana huu nimeenda msimbazi, nimeambiwa risiti hakuna. Sasa nikauliza inakuwaje kwenye ishu kama hii wananizungusha hivi na accaunt yangu inaweza kuibiwa wanasema there is nothing they can do. I am so mad hata sijui nfanyeje, tena bila aibu polisi huyo ananiambia rudi kule mlimani wabembeleze wape chochote wakuandikie lost report ndo hali ilivyo" can you imagine? Yani nimesumbuliwa wiki mbili ili nilipie tu sh 500 nimetembea vituo vyote hivyo vya polisi na hakuna nilichokipata, sasa jamani kwa hali hii mtu anafanyaje? Je hii nchi haina kabisa utaratibu wa maana zaidi ya mlolongo mrefu usiokuwa na kichwa wala miguu ukitoa mianya ya rushwa? Na sasa ni lazima kuwe na process ndefu namna hii kwenye huduma ambayo ni haki yangu?

Pole sana ndugu yetu. Hiyo ni Dar es salaam sasa ingekuwaje kama mambo hayo yangekukuta mikoani?.
Tanzania tunahitaji kubadilika ili tuweze kwenda sambamba na nchi zingine. Lakini ungekuwa na jina zito ama unatokea katika familia yenye jina kubwa hapa Tanzania basi ungesaidiwa palepale kituoni mlimani.
 
Mtambo....ELEWA KITU KIMOJA!
LAST HOPE HAKUHITAJI MSAADA WA POLISI KUFUNGA AKAUNTI YAKE.
 
Members hili limenisikitisha sana na sina pa kulisemea zaidi ya hapa. nilipoteza wallet yangu8 tarehe 21 ikiwa na id's zangu pamoja na ATM card yangu, sasa nikaenda bank niblock account yangu. Nikaambiwa haiwezekani hadi niende polisi nipewe lost report. Hapo bank wakanipa form ya kunitambulisha huko polisi kama mteja wao. Nikaenda police pale Udsm mlimani , wakaandika maelezo yangu then nikaambiwa inabidi niende kituo cha magomeni au oysterbay nikalipie shilingi mia tano (500) kwa sababu wao hawana mhasibu pale, nipewe risiti niirudishe pale polisi ndio wanipe hiyo lost report ili nende bank kublock account yangu na kuanza process ya kupewa ATM mpya. Kwa kuwa ilikuwa jioni definately nisingemkuta huyo mhasibu, nilivyoenda oysterbay nikaambiwa hawana risiti zimeisha niende magomeni, nikaenda magomeni nikaambiwa risiti zimeisha niende baada ya siku tatu au niende msimbazi, kumbuka siku zinapita sijablock account yangu, mchana huu nimeenda msimbazi, nimeambiwa risiti hakuna. Sasa nikauliza inakuwaje kwenye ishu kama hii wananizungusha hivi na accaunt yangu inaweza kuibiwa wanasema there is nothing they can do. I am so mad hata sijui nfanyeje, tena bila aibu polisi huyo ananiambia rudi kule mlimani wabembeleze wape chochote wakuandikie lost report ndo hali ilivyo" can you imagine? Yani nimesumbuliwa wiki mbili ili nilipie tu sh 500 nimetembea vituo vyote hivyo vya polisi na hakuna nilichokipata, sasa jamani kwa hali hii mtu anafanyaje? Je hii nchi haina kabisa utaratibu wa maana zaidi ya mlolongo mrefu usiokuwa na kichwa wala miguu ukitoa mianya ya rushwa? Na sasa ni lazima kuwe na process ndefu namna hii kwenye huduma ambayo ni haki yangu?

Kwanza karibu sana JF. Jibu la swali lako ni kwamba ndiyo maana wengi wanaleta mapendekezo yao hapa JF, lakini je hali hiyo ndiyo unaijua leo, mbona mambo hayo ni ya siku nyingi? Pole sana.
 
Lasthope:
Mimi nilitoa shs 10,000/= Oyster Bay ili nipate ripoti ya polisi baada ya kupoteza kitambulisho cha kazi. Huo mzunguko ulioambiwa nami niliambiwa vile vile.
 
Kwanza karibu sana JF. Jibu la swali lako ni kwamba ndiyo maana wengi wanaleta mapendekezo yao hapa JF, lakini je hali hiyo ndiyo unaijua leo, mbona mambo hayo ni ya siku nyingi? Pole sana.

Sasa kama ni ya siku nyingi nifanyeje? nikubali kutoa rushwa? yanaweza kuwa ya siku nyingi lakini sijakutana nayo. je inawezerkana vituo vyote hivyo vya polisi wote wanataka rushwa/ ama ni kweli risiti books zimeisha? na kama ni kweli risiti zimeisha je inawezekanaje jambo hili serikalini au zina printiwa ulaya hazi iwe muda mrefu hivyo?
 
...Kweli kabisa hawa polisi wa ngazi za chini wameshalemaa na rushwa bora uanzie kwa mabosi wao tu....angalia mazee hako karisiti kasije kusababisha upoteze mihela yako kama wanaweka usiku funga akaunti tafuta benki nyingine...Mi nakwambia Tz imeoza[/QUOTE

Naenda tena bank asubuhi hii na polisi huko chuo niplead nao, nikishindwa ntakomba kila kilicho changu hapo bank na kuondoka nacho na kufunga hiyo account. Ni NBC kWA FAIDA YA WALE WANAOTAKA KUJUA.
 
Pole sana mkuu.
Lakini hapo hukujua tu yalikuwa mazingira ya rushwa kwa vile wewe ulikuwa umekomaa ndo maana wakaamua kukuzungusha lakini hapo ungenunua HAKI yako kwa 5000/= mbona ungeshughulikuwa faster tatizo mkono wako ulikuwa mfupi.
Hii ndo BONGO bwana wanadai kila mtu anakula kutokana na ulefu wa kamba.Mshahara wenyewe wanao lipwa ni kima cha mbuzi wataacha kukuzungusha ili usitoe rushwa hii thubutu.Lazima upigwa danadana mpaka unazama mfukoni unanunua HAKI tatizo mishahara midogo sana serikalini.
 
Shauri yenu, nyi endeleeni kusema uozo wa nchi yetu, mnazidi kuwaogopesha wabeba maboksi kurudi home.

Mwanakijiji aliyekuwa ana mpango wa kurudi mnazidi kumuogopesha..hivyo inabidi mseme taratibu...maana kwa mwendo huu vijana wetu makini akina YourNaME, Mwafrika wa Kike, Nyani Ngabu, Joka Kuu, Fundi Mchundo, StevD et al...hawatataka kurudi kwa kuogopa kadhia kama hizi! Maana wamezoea maisha ya suluba huko ughaibuni lakini yanayoheshimu utu wa mtu! Bongo ni suluba tuu na utu hauheshimiwi!

Hiyo ndiyo bongo bana, kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yako....shauri yako kama kamba yako inaishia pasipo na nyasi au nyasi kavu ambazo haziliwi!

Masanja,
 
...Kweli kabisa hawa polisi wa ngazi za chini wameshalemaa na rushwa bora uanzie kwa mabosi wao tu....angalia mazee hako karisiti kasije kusababisha upoteze mihela yako kama wanaweka usiku funga akaunti tafuta benki nyingine...Mi nakwambia Tz imeoza[/QUOTE

Naenda tena bank asubuhi hii na polisi huko chuo niplead nao, nikishindwa ntakomba kila kilicho changu hapo bank na kuondoka nacho na kufunga hiyo account. Ni NBC kWA FAIDA YA WALE WANAOTAKA KUJUA.

Mkuu pole sana ndugu yangu, ngoja tuzidi kupambana hapa kwenye Keyboard...atleast for now...ipo siku kitaeleweka. But to me my worst BANK IS CRDB. Yaana wanaukiritimba sijawahi kuona hapa duniani!
 
Pole sana mkuu.
Lakini hapo hukujua tu yalikuwa mazingira ya rushwa kwa vile wewe ulikuwa umekomaa ndo maana wakaamua kukuzungusha lakini hapo ungenunua HAKI yako kwa 5000/= mbona ungeshughulikuwa faster tatizo mkono wako ulikuwa mfupi.
Hii ndo BONGO bwana wanadai kila mtu anakula kutokana na ulefu wa kamba.Mshahara wenyewe wanao lipwa ni kima cha mbuzi wataacha kukuzungusha ili usitoe rushwa hii thubutu.Lazima upigwa danadana mpaka unazama mfukoni unanunua HAKI tatizo mishahara midogo sana serikalini.

Pole ndugu kwa yalo kukuta,. ila si benki pekee, mie nili ibiwa simu, nilikuwa mteja wa celtel, nilivo enda kuomba line hiyo hiyo, nikaambiwa nipeleke hiyo polisi report, nilizungushwa hivo hivo hadi kule central, ila masikini mie sikuwa najua kwamba walitaka kitu kidogo nilijua sincerely hizo risiti hawana, hivi kumbe huwa zipo isipokuwa wanataka kitu kidogo?

Kwa mwendo huu bado safari ni ndefu sana!
 
Suala la kublock account linatakiwa lifanywe as soon as unapogundua kuwa umepoteza kadi bank card yako, you dont even need to go to the bank, kila bank ina namba ya simu maalum kwa ajili hiyo ambayo inafanya kazi 24 hrs kila siku, utaulizwa tu accounts details na of course neno la siri. Mhh- dont get too excited kama upo bongo,sorry- hii ni kwa wenzetu 'walioendelea' na kustaraabika, its not a rocket science- our banks can also do this but they just dont care!
 
Banki Zote Zina Huduma Ya Masaa 24 Ya Simu Kwanini Hukutafuta Namba Yao Ya Simu Uwapigie ? Pia Kama Umeshindwa Hiyo Benki Karibu Zote Unaweza Kuaccesss Account Yako Online Je Katika Hiyo Yako Hakuna Sehemu Yoyote Ya Kureport Tatizo Lako ?

Hata Wewe Umekosea Kuna Njia Hukufuata Unaonekana Ulikuwa Na Haraka Sana
 
Halafu Hapo Sioni Suala Lolote La Ufisadi Unalidhalilisha Jeshi Letu La Polisi Unavyojaribu Kuliweka Katika Mazingira Haya Bwana
 
Pole sana .
Hapo ufisadi ni kwenye hiyo bank yako.Wange block kwanza halafu ndiyo uendelee na mambo ya polisi
 
Halafu Hapo Sioni Suala Lolote La Ufisadi Unalidhalilisha Jeshi Letu La Polisi Unavyojaribu Kuliweka Katika Mazingira Haya Bwana

SHY jeshi hili letu lilisha laanika mbona unaishi ugaibuni nini??KUna kero kibao Polisi pale rushwa ndo usiseme watu tunanua HAKI zetu pale mpaka RAIS anajua haya alafu wewe unasema wamelidhalilisha jeshi why????? kwa nini? HApo ni rushwa mtindo mdogo ni kweli vituo vyote viishiwe risiti za serikali kulipia??tena zile za njano?Inaingia akilini kweli risiti ziishe Buguruni au Oysterbay?Wewe upo wapi bwana??
 
Shauri yenu, nyi endeleeni kusema uozo wa nchi yetu, mnazidi kuwaogopesha wabeba maboksi kurudi home.

Mwanakijiji aliyekuwa ana mpango wa kurudi mnazidi kumuogopesha..hivyo inabidi mseme taratibu...maana kwa mwendo huu vijana wetu makini akina YourNaME, Mwafrika wa Kike, Nyani Ngabu, Joka Kuu, Fundi Mchundo, StevD et al...hawatataka kurudi kwa kuogopa kadhia kama hizi!

Masanja!
Nashukuru kwa kuniita kijana.
Nakumbuka hapo zamani kidogo wakati NBC ndiyo benki pekee ya maana, nilishuhudia jamaa akikaripa baada ya kuambiwa aende akalete lost report ya polisi. Akadai kwenda kwa meneja ambaye akarudia wimbo ule ule. Jamaa akawaambia kama mchezo wenyewe ndio huo, anafunga account yake! Nadhani wali'freeze' account yake.

Sisi watanzania tumezoea vitu viwili:

1) kununua haki yetu. Kiasi cha kwamba hatuoni taabu kukata kitu kidogo ili tuipate.

2) Kuogopa authority. Tunakubali kuendeshwa na madesk officers, receptionists hata mesenja! Kwa nini huyu bwana baada ya kuona upuuzi hu hakudai kuwaona wakubwa zaidi? Huko polisi angepanda ngazi hadi kwa Mwema. Hapo ndipo jamaa watakapo shika adabu. Hauwezi kuzungushwa vituo vyote hivyo kwa ajili ya risiti!

Nashauri lolote litakalotokea aandike barua ya kulalamika kwa Kova, nakala Mwema na Katibu Mkuu, Mambo ya Ndani. Akiona wanapuuzia aitie kwenye magazeti na mlolongo mzima wa ishu. Aandike nyingine kwa meneja wa benki yake, nakala kwa CEO, akitoa sababu za KUFUNGA akaunti yake.

Upuuzi huu ni kama ule wa PF3. Inabidi wabadilike na kuwajali wateja.
 
pole sana kwa yote yaliokukuta why usimpigie kamanda wa kandaa maaluumu ukamwelezea jinsi vijana wake wanavyofanya kazi kizembe awaajipishe, namba yake ni Kamanda Seleman Kova 0754094224
 
kamanda alilisifia sana jeshi lake wiki iliopita ktk vyombo vya habari sasa hili ni la kusikitisha kwa jeshi letu tunalolitegeme kutusaidia halafu wana fanya mauzauza JE! TUTAFIKA....!
 
Back
Top Bottom