Dx and Rx
JF-Expert Member
- Jul 16, 2017
- 1,303
- 3,085
Nilitaka kutoa pesa dirishani kwenye tawi moja la Bank ya NMB hapa kwenye huu mji wenye Elnino.
Nilipofika dirishani nikamkuta mhudumu nikampa ile karatasi(bank slip) niliyojaza ili nitoe hela.
Mhudumu akaingiza details na kuthibitisha taarifa then akakata hiyo slip kwenye maandishi ya kwa red pen na akaniambia nenda dirisha fulani.
Nilipofika kwenye hilo Dirisha nikampa huyo mhudumu niliyemkuta pale ile slip niliyotoka nayo dirisha la kwanza.
Baada ya kuiona na kuangalia details kwenye mfumo akaniambia nenda pale mapokezi ukapewe fomu ujaze(mimi nilikuwa sijui ni fomu ya aina gani)
Nilipofika mapokezi nikamwambia nimetoka kwenye dirisha fulani nilikuwa nataka kutoa hela ila nikaambiwa nije hapa, mhudumu wa mapokezi baada ya kunisikia hivyo akanipa fomu akaniambia jaza. Nikaisoma fomu nikagundua ni fomu ya kubadili status ya Bank Account.
Baada ya hapo nikarudi nikamwambia mimi nilitaka kutoa hela na wala sikutaka kubadili status, akanipa maelezo ambayo hata sikuyaelewa huku akisisitiza nijaze ile fomu ndipo nikapate huduma.
Nikasema ngoja nimuulize kwanza jamaa yangu ambaye alikuwa ananisubiri sehemu ili twende kusaka maokoto. Nikamtext jamaa fast na kumueleza scenario akaniambia "kimbia haraka, hao watakuumiza kwa makato", akaendelea kunisisitiza "ondoka fast jifanye unaongea na simu toka katoe ATM halafu uje twende"
Nikaamua kufuata ushauri wa jamaa yangu, nikaondoka.
Sasa nilitaka kutoa tena hela dirishani ila kwenye Tawi la hiyo Bank mkoa mwingine(maana nilisafiri kusaka maokoto)
Wakati naenda kwenye hili tawi la mkoa mwingine nilikuwa najua huenda wakanizingua tena na ikawa hivyo kweli.
Kwenye hili tawi mhudumu alipoangalia details baada ya kumpa slip, aliniuliza "umeangalia salio"? nikamwambia hapana(ila nilikuwa najua salio maana huwa nachukua risiti kila nikitoa hela ATM)
Akaniambia Account inasoma, nikamwambia inasoma nini, akaanza kutabasamu. Akasema salio lipo ila halioni kwenye computer, nikamwambia kwa hiyo haiwezekani kutoa, akasema ndio.
Nikamwambia mbona ATM natoa kama kawaida, akasema hapa dirishani haiwezekani. Halafu akaniambia nenda pale mapokezi wakakuangalizie Account na wakusaidie ili uweze kutoa.
Nikajisemea hawa mbona wananiwinda hivi, nikasepa nikaenda kutoa ATM kidogo kidogo ingawa huku napo nilipigwa limit sikuweza kutoa kiasi nilichotaka baada ya kuambiwa na system kuwa nimefikia kikomo cha kutoa kwa siku ATM.
Kabla ya kuandika huu uzi nimepitia nyuzi humu zinazohusu CHAP CHAP Account ya NMB, nimegundua kuwa haina makato mengi kama PERSONAL Account. Kubwa zaidi nimeona makato ya kila mwezi na ya minimum balance to maintain account. Naona lengo la kuwindwa ni kutaka niingizwe kwenye hayo makato na mengineo ambayo wanayajua wao.
Sasa sitaki niibadili kwanza kama wanavyonitaka, je, wanaweza kuibadili bila ridhaa yangu maana nimeona lazima nijazishwe ile fomu ambayo nitaweka details zangu kama NIN, Picha, Anwani n.k