Ujue ufisadi huu POLISI

Wakuu pia tusisahau kuwa LAST HOPE hakuitaji kwenda polisi.
Muelewe kuwa sheria za benki ni kama zinaiongoza nchi..Ama ukipenda..Zina act kama PROXIMATION ya kukuamulia maamuzi muhimu ambayo ni binafsi na yenye kuhitaji kutokuingiliwa.
Haimake sense kabisa kwenda polisi kuomba akaunti yako ifungwe!

Kwamba ni kweli ATM card yako imepotea ama la...Then ndio unahitaji kwenda polisi kuripoti ili na wao watoe tangazo.
Lakini benki ilitakiwa ifunge akaunti hiyo MARA MOJA!
Na mambo ya polisi ni baadaye.
NCHI IMEOZA HIYO INAHITAJI MABADILIKO MAKUBWA SANA.
Mambadilko hayo hatutaweza kuyapata kama hatutadai UHURU WETU SASA!
 
Polisi wa Tanzania hawapo kwa ajili ya kulinda usalama wa umma, kazi yao kubwa ni kuwalinda na kuwatetea mafisadi ambao kwao kuchunguzwa na kufichwa majina yao ilhali makabwela wakishukiwa tu basi watatangazwa kwa nguvu na mapolisi kuwaita wana habari ili waoneshe jinsi wanavyofanya kazi

Sijatoka nje ya mada kikubwa nenda kafunge akaunti yako



Polisi wa umma wakija, mafisadi watachekea selo
 
Ukifanyiwa hivyo we piga picha (simu zina kamera sikuhizi), record na simu yako, yani fanya lolote halafu lilete hapa... JF ndio chombo cha kurekebisha tabia na cha habari... watu wengi sana wanasoma JF, sasa tukiwa tunakuja na nondo kama number, picha, videos ni ushahidi tosha..... mpaka watanyooka tu hawa.....
 
Jamani ameshapata hela zake na report kapata bila kulipia shs 500,

Pole dada kwa yaliyokukuta.
 
Ujumbe wangu kwenu mapolisi: kama hamlipwi mishahara inayokidhi hiyo sio sababu ya kulazimisha rushwa. Badala yake muende mkaandamane!

Hivi kwa sheria za hapa Tanzania, kuna mahali imekatazwa ku-rekodi mazungumzo yangu na Polisi, mfano kwa kutumia simu? Je, kuna haja ya mimi kumfahamisha kwanza kwamba nina-rekodi hayo mazungumzo?
Ushahidi wa namna hii utakubalika mahakamani?




.

Siku nyingine pale pale omba kuongea na mkuu wa kituo, na unaenda ukiwa na namba ya askari....
 
Tunazungumzia kuhusu sheria hizo za benki za kumtaka mtu kwenda polisi kabla akaunti yake haijafungwa!
NI SHERIA ZA KITUMWA!
 
Siku nyingine pale pale omba kuongea na mkuu wa kituo, na unaenda ukiwa na namba ya askari....


In Tanzania it is not that simple my friend. Nimeshuhudia mkuu wa kituo akishirikiana na subordinate wake. Tena kawapa gari lake (sio la ofisi) kusaka 'wavunjaji' wa sheria. Mtaani pia watu wanakiri hivyo.



.
 


In Tanzania it is not that simple my friend. Nimeshuhudia mkuu wa kituo akishirikiana na subordinate wake. Tena kawapa gari lake kusaka 'wavunjaji' wa sheria. Mtaani pia watu wanakiri hivyo.



.

Ukiwa mgumu wote wananywea, mimi siku moja niliibiwa kwenye foleni nilienda front kwa wakati ule alikuwa Maji... nilikomaa mpaka nikamuona... niliongea sana siku hiyo na wakati huohuo aliitisha kikao cha wakuu wa vituo... cha dharura....


unapodai haki yako komaaaaa.... jilipue..... (usivunje sheria) wote watakaa pembeni kukusikiliza....

na siku nyingine nilikuwa nakimbia (najog) kwenye saa moja hivi usiku nilisimamishwa na hao maaskari wakaniambia si sheria kukimbia eneo lile (jangwani) nilipomuliza sbb akaniambia kaambiwa na mkuu wake, nikamwambia kuwa huo ujumbe ulikuwa ni wake na kama alikuwa amenikusudia mimi kama mwananchi nilimwambia akamweleze bosi wake kuwa sheria zote hupitia bungeni.... anakiomba msamaha... nikaondoka zangu
 


Mimi ni mmoja wao. Hata hivyo sidhani kwamba tunatakiwa kuacha kutii mamlaka au kuamini maelekezo wanayotoa.



.

Haukunielewa. Sikumaanisha kuacha kutii mamlaka. Nilimaanisha tunaogopa kuwaona wenye authority hata kwenye kudai haki yetu wenyewe. Ni haki yako ukiona maelezo ya aliyekuhudumia mwanzo hayaingii kichwani, kudai kumwona boss wake. Na huyo naye kama hakuingii kwenda kwa boss wake. Na kuendelea. Na si kwa mdomo tu. Maandishi. Wasipokujibu unakumbushia kwa boss wa juu yake na kutuma nakala kwa aliyekusumbua! Wenzetu ndivyo wanavyofanya. Sisi tunakubali kuonewa kirahisi. Kwa namna hii, hivi vipetty tyrants vitaendelea kutunyanyasa.
 
Ukiwa mgumu wote wananywea, mimi siku moja niliibiwa kwenye foleni nilienda front kwa wakati ule alikuwa Maji... nilikomaa mpaka nikamuona... niliongea sana siku hiyo na wakati huohuo aliitisha kikao cha wakuu wa vituo... cha dharura....


unapodai haki yako komaaaaa.... jilipue..... (usivunje sheria) wote watakaa pembeni kukusikiliza....

na siku nyingine nilikuwa nakimbia (najog) kwenye saa moja hivi usiku nilisimamishwa na hao maaskari wakaniambia si sheria kukimbia eneo lile (jangwani) nilipomuliza sbb akaniambia kaambiwa na mkuu wake, nikamwambia kuwa huo ujumbe ulikuwa ni wake na kama alikuwa amenikusudia mimi kama mwananchi nilimwambia akamweleze bosi wake kuwa sheria zote hupitia bungeni.... anakiomba msamaha... nikaondoka zangu

Mara nyingi hao wakuu wa vituo wanashirikiana na subordinates wao. Bila shaka. Lakini wakijua kuwa uko tayari kumruka hata yeye, watakumalizia uwaondolee kiwingu. Kama alivyosema, Mkuu, hapo juu, ukiwa mgumu wananywea. Usiwatukane lakini hakikisha wanajua kuwa unatarajia kwenda mbali kupata haki yako. Watakuachie maana bullies wote ni cowards.
 
Wananchi si tu kwamba hawajui haki zao...!
Bali hata viongozi wetu hawajali kwani na wao ni CORRUPT to the extent kwamba wanalindwa na corrupt polisi na wao wanawafumbia macho.

Ni system MBOVU inayohitaji mabadilko kwani polisi ni sawa na kumtrain jambazi na kumuingiza mtaani akanyanyase wananchi!

Kazi yao ni kupiga tu na kuomba rushwa na unyanyasaji wa kila aina!
Niliwaambia nitamlaumu mwalimu Nyerere kwani sheria zile zile za mkoloni alizokuwa akipingana nazo ndizo sheria hizo hizo zilitumika na bado zinaendelea kutumika dhidi ya MWAFRIKA!

Polisi wenyewe malipo yao ni finyu...Lakini pia wakumbuke licha ya kwamba cheki zao wanapopewa zina saini ya bosi wao...Bado wakumbuke ni jasho la mlipa kodi!

Huwezi kumyanyasa mtu anayekulipa kwa jasho lake!
Ni utumwa...Na wananchi wapewe elimu ya uraia na wajulishwe haki zao mara baada ya sheria hizo za MKOLONI zikibadilishwa!

Sheria zilizoachwa na baba wa taifa...Halafu zikatumiwa na MAFISADI kuturudisha chini ya mkoloni!
 
Pamoja na kupata pesa zake nafikiri hatutakoma kurekebishana hapa na kuwakemea wale tunaoona wanahatarisha haki ya watu. Itafika siku righteousness will roll down like waters and JUSTICE like a mighty spring!
 
Back
Top Bottom