Ujue ufisadi huu POLISI

Lasthope

Senior Member
Jun 5, 2008
149
6
Members hili limenisikitisha sana na sina pa kulisemea zaidi ya hapa.

Nilipoteza wallet yangu tarehe 21 ikiwa na id's zangu pamoja na ATM card yangu, sasa nikaenda bank niblock account yangu. Nikaambiwa haiwezekani hadi niende polisi nipewe lost report.

Hapo bank wakanipa form ya kunitambulisha huko polisi kama mteja wao. Nikaenda police pale Udsm mlimani, wakaandika maelezo yangu then nikaambiwa inabidi niende kituo cha magomeni au oysterbay nikalipie shilingi mia tano (500) kwa sababu wao hawana mhasibu pale, nipewe risiti niirudishe pale polisi ndio wanipe hiyo lost report ili nende bank kublock account yangu na kuanza process ya kupewa ATM mpya.

Kwa kuwa ilikuwa jioni definately nisingemkuta huyo mhasibu, nilivyoenda oysterbay nikaambiwa hawana risiti zimeisha niende magomeni, nikaenda magomeni nikaambiwa risiti zimeisha niende baada ya siku tatu au niende msimbazi, kumbuka siku zinapita sijablock account yangu, mchana huu nimeenda msimbazi, nimeambiwa risiti hakuna.

Sasa nikauliza inakuwaje kwenye ishu kama hii wananizungusha hivi na accaunt yangu inaweza kuibiwa wanasema there is nothing they can do. I am so mad hata sijui nfanyeje, tena bila aibu polisi huyo ananiambia rudi kule mlimani wabembeleze wape chochote wakuandikie lost report ndo hali ilivyo" can you imagine? Yani nimesumbuliwa wiki mbili ili nilipie tu sh 500 nimetembea vituo vyote hivyo vya polisi na hakuna nilichokipata, sasa jamani kwa hali hii mtu anafanyaje?

Je hii nchi haina kabisa utaratibu wa maana zaidi ya mlolongo mrefu usiokuwa na kichwa wala miguu ukitoa mianya ya rushwa? Na sasa ni lazima kuwe na process ndefu namna hii kwenye huduma ambayo ni haki yangu?
 
nchi imeliwa na mafisi,wewe kafunge account yako,kisha chukua kilicho chako.hiyo benk yako ni wendawazimu tena haifai kuwa benk ktk ulimwengu wa sasa.tanzania imeoza mpaka inatia kinyaaa.
pole kwa yaliyokukuta.huku kwetu mambo ni tofauti sana ukipoteza auukibiwa wewe unachofanya ni kupiga simu tu na unamaliza kila kitu widhini ya dakika tano tu.polisi report wanakupa reference namba tu.
 
Nenda kwa waandishi wa HABARI na mrekodi majibizano yote na ikibidi TAKURURU na wao watakupa hicho kitu kidogo. Na mwisho malizia kwa kubadilisha BANK kwani hilo bank unaotumia ni la KIJINGA na KI-COMUNIST. Hebu weka kabisa jina lao ili iwe fundisho kwa wengine na ikibidi waandishi wa habari wawafuate na kuwauliza utaratibu wao huo ukichukulia uzembe wa POLISI nchini. Bank gani hii yarabi???
 
he unashangaa, hapa Tz ukipoteza chochote, inabidi uende polisi. Ni kwa kuwa hatujulikani watanzania, labda vitambulisho vya uraia vitasaidia.
mimi nilipoteza driving licence, atm cards and medical cards,
benki moja walinifungulia (tunajuana). Nyingine ilibidi niende polisi, nilipoteza nusu siku, hadi ikafika jioni ambapo walikuwa wanafunga ilibidi nitoe 2000 ili wanipe ripiti blia risiti. Hapo nilishatoa 500 ya kawaida.
Ile medical insurance card ilibidi niwape 5000 wanipe cadi ingine (bila risiti0 kwani niona kurudi polisi sitaweza tena..
 
Pole na yaliyokukuta. Naona huu utaratibu wa kupata police report kabla benki haijablock account yako ipo katika kila benki tanzania.
 
Kwanza kabisa nampa pole sana mwenzetu aliyepotelewa na documents zake. Pamoja na hayo, mbali na lawama kulielekea jeshi letu la polisi, mimi nadhani pia wenzetu wa Financial institutions (mabenki) wanatakiwa wajue kwamba kazi yao kubwa ni kuhakikisha usalama wa amana za wateja wao unapewa kiwango na uzito wa hali ya juu. Kwa kweli binafsi kumwambia mteja karipoti Polisi wakati amepotelewa na kitu muhimu kama Debit Card ambayo ni muhimu kwa usalama wa amana yake, ni jambo la kushangaza. Nafikiri umefika wakati kwa mabenki yetu ku-abolish bank policies zisizokuwa na maana. I do not think, this person is a mad person going to his banker asking them to block any transaction relating to his debit card.

Once gain, natoa pole kwa mwenzetu huyu kwa usumbufu wote huu alioupata.

Thanks
 
Yaani Polisi wanaishiwa na risiti, stakabadhi zinazotumiwa kukusanya mapato ya serikali? Hawa wanaihujumu serikali isipate mapato yake.
 
Nenda kwa Kova moja kwa moja ... atawaamrisha mara moja utaona kama hutotetemekewa kama mfalme ... wakikuchezea chini we unapanda juu ... tena unajifanya hamnazo kabisa .. unagonga tu unaingia
 
This is disgusting...!

Kweli kabisa, haiwezikani kukakosekana kitabu cha risiti, huu ni uzembe wa hali ya juu kabisa.

Secondly, i think there is pervesive recklessness within our police, most of them are tuned to the conventional thinking that police is meant to fight thieves and not to assist civilians.

To my opinion, i know there are plenty of journalist/reporters with in JF, may i kindly request them to take this story and put it to their papers so as it may be well known by everyone. You can imagine if this is the situation in Dar es Salaam, what is the situation in other regions or Districts?

SHAME
 
Nchi imeoza hii nikisema mnabisha...

Last hope wewe ndiyo mwenye haki!
Hayo mabenki...Yalitakiwa yawe na rekodi zako kama namba ya simu nk...Hiyo ilitosha kufunga akaunti yako bila haja ya RB ya polisi!

Nyie viongozi mnafanya nini?
Ama busy kuuza nchi?

Huyu mtu anahitaji polisi wa kazi gani kabla akaunti yake kufungwa?
Ama mlikuwa mnataka kuona pesa zake zikipotea?

SHAME ON YOU!

Badilisheni taaratibu ili kuwe na uwezo wa kuverify information kama hizo!
Sasa mtu anataka akaunti ifungwe si ana nia nzuri?
Nafikiri kama ingekuwa imefungwa...Halafu akapiga simu akasema ifunguliwe..Then ndio labda mngemuuliza maswali ili kuhakikisha kuwa kabla haijafunguliwa...Aliyesema ifunguliwe ni mwenye akaunti na hata akitumia pesa hizo ni za kwake.

USHAURI WANGU...ACHANA NA POLISI WAO PIA NI WAZI WANATAKA RUSHWA!
WAFUNGULIE MASHTAKA BENKI!
MAKUBALIANO YENU MLIFANYA NA BENKI NA SI POLISI!
WALITAKIWA KUKUSIKILIZA NA KUFUNGA AKAUNTI YAKO MARA MOJA!
MASWALI MENGINE NI BAADAYE!
WALITAKIWA WAFANYE UDHIBITISHO KAMA AKAUNTI NI YAKO...NA BAADA YA HAPO WAFUNGE!
POLISI HANA HAKI NA AKAUNTI YAKO!
NI WEWE NA SI MWINGINE YEYOTE YULE!
JAMANI VIONGOZI....MMESHATURUDISHA UTUMWANI?
 
Pole sana Lasthope. Nimewahi kusikia tena story kama yako Dar-es-Salaam.
Huyo bwana alipofika Oysterbay alitizamwa kwa jicho la dharau na receptionist aliyekuwepo. Akaulizwa mia tano ya nini, halafu huyo dada akasonya.
Jamaa akasoma katikati ya mistari akaweka mezani 2000. Ilipokelewa ila bado alihudumiwa kwa kejeli nyingi tu. "Mnaturingishia vigari vyenu mnatuona sisi hatukwenda shule" - huyu ndugu maskini wala hakwenda na gari pale, yaani maudhi tu.

Hapa ndipo tulipofika wandugu. Pata picha hali ilivyo huku mikoani!

.
 
Nenda kwa Kova moja kwa moja ... atawaamrisha mara moja utaona kama hutotetemekewa kama mfalme ... wakikuchezea chini we unapanda juu ... tena unajifanya hamnazo kabisa .. unagonga tu unaingia
...Kweli kabisa hawa polisi wa ngazi za chini wameshalemaa na rushwa bora uanzie kwa mabosi wao tu....angalia mazee hako karisiti kasije kusababisha upoteze mihela yako kama wanaweka usiku funga akaunti tafuta benki nyingine...Mi nakwambia Tz imeoza
 
Nafikiri tatizo hapa ni policies za benki. There's got to be a way wakati mtu anafungua akaunti mpya ku verify kuwa ni yeye ndio mlengwa. Na in most cases ni kitu cha ku provide one or two forms of ID's cards basi. Kama debit card imeibiwa ni jukumu la benki ku i supsend ile account temporary mara tu baada ya kupata taarifa kutoka kwa mwenye account. Vinginevyo kama mteja katoa taarifa kuhusu upotevu wa kadi zake na kuomba benki i block account yake na benki ikafanya otherwise..halafu kukawa na transcations..na uchunguzi ukaonyesha kuwa hizo transactions sio za yule mwenye account..basi benki inakuwa liable kum reimburse mteja kile kiasi kilichopotea.
Hivi kwanza benki zetu zina Bima ya serikali?
 
dawa yao n kwenda na recorder na hela za moto! ....napo inategemea kama takuru watafanya kazi yao ipasavyo. poor Tanzania.
 
Sheria Za Benki Za Makaburu Zimegeuka Sheria Za Nchi Halafu Mnasema Tuko Huru?
Kuzitoa pesa zako ama kupata haki yako kama MTEJA...Kweli hadi UENDE POLISI?
HILI SWALA LIANGALIWE NA WATANZANIA MUIBADILI NCHI...KWANI IMEUZWA NA NYIE PIA MMEUZWA MKIWA NDANI!
 
Kwanza kabisa nampa pole sana mwenzetu aliyepotelewa na documents zake. Pamoja na hayo, mbali na lawama kulielekea jeshi letu la polisi, mimi nadhani pia wenzetu wa Financial institutions (mabenki) wanatakiwa wajue kwamba kazi yao kubwa ni kuhakikisha usalama wa amana za wateja wao unapewa kiwango na uzito wa hali ya juu. Kwa kweli binafsi kumwambia mteja karipoti Polisi wakati amepotelewa na kitu muhimu kama Debit Card ambayo ni muhimu kwa usalama wa amana yake, ni jambo la kushangaza. Nafikiri umefika wakati kwa mabenki yetu ku-abolish bank policies zisizokuwa na maana. I do not think, this person is a mad person going to his banker asking them to block any transaction relating to his debit card.

Once gain, natoa pole kwa mwenzetu huyu kwa usumbufu wote huu alioupata.

Thanks


Another Mwanakijiji!!!!!!!!!!
 
Nenda kwa Kova moja kwa moja ... atawaamrisha mara moja utaona kama hutotetemekewa kama mfalme ... wakikuchezea chini we unapanda juu ... tena unajifanya hamnazo kabisa .. unagonga tu unaingia

Nadhani kwa walio karibu wamshawishi kama Kova naye ajiunge JF, nadhani na yeye atafaidika sana kama ambavyo ataweza kutupatia msaada
 
Hiyo ndio Tanzania, yaani kila tukio ni dili la mtu sasa hapo police wakishapata issue kama hiyo kwao ni dili. Mi nafikiri hapa ni kuwa na usalama wa Taifa strong sio TAKUKURU, yaani wajifanye watu wenye matatizo wanaenda Police na ofisi mbali mbali za umma, kujifanya wanataka huduma wakizunguushwa tu next day mtu anapewa transafer Tandahimba na kuambiwa kuwa jana alimzunguusha mtu kwa kutaka chochote ndio sababu ya transfer. yaani huo uwe utaratibu, ILA PANATAKA HAWA JAMAA WAWE FAIR hasa maana wanaweza anzisha visasi. Hapa ni vita dhidi ya Tabia na mtazamo ikifanyika hivyo mwaka mmoja mfulizo nchi itakuwa na amani na rushwa itapungua sana. na tutakuwa na utamaduni wa kuwajibika. Ila la muhimu pia na hawa mafisadi watunga sera waache wizi wawalipe watu pesa ya kutosha kuishi kwa mwezi mzima.
 
Pole sana ndugu, pia ninaomba jina la benki, ili nijihadhari nayo kabisa, itawasaidia na wengine pia
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom