Ujio wa Makamu wa Rais wa Warekani sio bahati mbaya

Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,402
942
Haya mambo hayatokei kwa bahati mbaya! Rais Samia Suluhu amerudisha sana heshima ya Tanzania kwenye diplomasia na sasa imerejea mahali pake, Serikali ya awamu ya tano ilififisha mahusiano kati ya Tanzania na nchi nyingi lakini Rais Samia Suluhu alipoingia madarakani amefanikiwa kuimarisha diplomasia iliyoanzishwa na watangulizi wake na sasa Tanzania tunaendelea kunufaika kupitia uhusiano huu.

Ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris nchini itaimarisha na kufungua zaidi fursa za biashara na uwekezaji.


FsPCPmVWcAMtPUk
 
..kwasababu Tz inaongozwa na mwanamke.

..Kamala Harris naye ni mwanamke.

..ndio maana ktk ziara yake lazima atembelee nchi ya Afrika inayoongozwa na mwanamke ili kunogesha na kuhalalisha ziara hiyo kwa vyombo vya habari vya Marekani.
 
Marekani sio taifa la kuamini,wapo kimasilahi zaidi,kuja Kwa Kamala ni vizuri Kwa taifa ila tutegemee kuendelea kunyonywa mahala fulani
Mimi nachokiona watanzania tutanufaika zaidi na ziara hii maana lazima Marekani aongeze uwekezaji Tanzania na hii itasaidia kutuinua kiuchumi na kuzalisha ajira nyingi zaidi maana

hadi sasa watanzania Zaidi ya 50,000 wamepata ajira za moja kwa moja kupitia uwekezaji wa TZS trilioni 10.97 uwekezaji huo uliofanywa na marekani
 
..kwasababu Tz inaongozwa na mwanamke.

..Kamala Harris naye ni mwanamke.

..ndio maana ktk ziara yake lazima atembelee nchi ya Afrika inayoongozwa na mwanamke ili kunogesha na kuhalalisha ziara hiyo kwa vyombo vya habari vya Marekani.
Hiyo inaweza kuwa sababu lakini sababu kubwa ni Rais Samia Suluhu ameboresha sera ya uwekezaji na kwakua Marekani ni muwekezaji mkubwa katika nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania lazima atembelee Tanzania nchi inayovutia zaidi kwa uwekezaji ukilinganisha na nchi nyingine Afrika
 
Makamu wa Rais wa nchi mnayodai ina-promote uchafu anakaribishwaje nchini? Au amekuja kinguvu?
Hta kama wanapromote ni huko kwao lakini huku kwetu hayo mambo hatuna na Rais wetu hawezi kuruhusu huo upuuzi sisi tunachoangalia ni jinsi Tanzania itakavyonufaika na kibiashara na uwekezaji baada ya ziara hii

Rais Samia Suluhu ni akili kubwa
 
Yule jamaa yeye alikuwa anapenda marafiki zake wawe ni cuba,urusi,china na N.korea tu!!akiambiwa dunia ya sasa huwezi taka kuongoza watu kama miaka ile ya 1945,ana kuwa mkali!!ila MUMGU NI FUNDI
 
Hta kama wanapromote ni huko kwao lakini huku kwetu hayo mambo hatuna na Rais wetu hawezi kuruhusu huo upuuzi sisi tunachoangalia ni jinsi Tanzania itakavyonufaika na kibiashara na uwekezaji baada ya ziara hii

Rais Samia Suluhu ni akili kubwa
... kwa maana hiyo wanaosema serikali hachukui hatua thabiti na za wazi kuonesha clearly kwa vitendo kwamba inapinga hayo mambo wanakosea? Kinyume chake ni as if serikali ina-support!
 
... kwa maana hiyo wanaosema serikali hachukui hatua thabiti na za wazi kuonesha clearly kwa vitendo kwamba inapinga hayo mambo wanakosea? Kinyume chake ni as if serikali ina-support!
Kinachotakiwa hapa ni kuingia barabarani na mabango ya NO NO LGBTQ ili ayaone Kwa amani na utulivy tu kwani uko shida gani.
 
as if serikali ina-support!
Kuna jamaa Jana alielezea kwamba alikua anafanya kazi kwenye taasisi fulani au tuiite taasisi B na kwenye hio taasisi B akakutana na hao jamaa (mashoga) wakiwa wamewekewa utaratibu wao maalum kwamba kila mwisho wa mwezi apart from salary payment kuna pesa walikua wanapewa pamoja na zawadi pia kutoka watu wa Marekani na wanaambiwa km kuna wenzao (mashoga) pia wawaambie wajiunge nao wapatiwe pesa na zawadi, akasema alipohoji kwanini wanafanya hivyo alipewa barua 2 moja ni ya hao wafadhiri na ya pili ni ya Wizara ya Afya ikitoa kibari kwamba hao watu wapatiwe hizo huduma km ilivyoelekezwa, kwa hio usiseme Serikali haijui au Serikali hai-support
 
Back
Top Bottom