ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
57,085
67,522
Naona Itifaki imezingatiwa.

VP Kwa VP.

MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango leo anatarajiwa kumpokea Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) mkoani Dar es Salaam.

Serikali kupitia kwa Msemaji wake mkuu, Gerson Msigwa imemkaribisha kiongozi huyo na imempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha diplomasia.

“Karibu Tanzania Mhe. Kamala Harris, Makamu wa Rais wa Marekani. Asante Mhe. Rais Dkt. @SuluhuSamia kwa kuimarisha diplomasia na uhusiano wetu na Mataifa makubwa Duniani. Tupo tayari kumpokea Makamu wa Rais wa Marekani…,” ameandika Msigwa katika ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa twitter.

Kamala Harris ambaye ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo nchini Marekani, anakuja nchini akitokea Ghana na akiondoka nchini anatarajiwa kwenda Zambia.

Baada ya kufika Ghana, Machi 26, mwaka huu, kupitia ukurasa wake wa twitter alieleza kuwa ni heshima kwake kuwa barani Afrika na kwamba nchi katika bara hilo ni muhimu kwa usalama wa dunia.

Alieleza kuwa akiwa barani humo anatarajia kukutana na viongozi, vijana na wajasiriamali wanapofanya kazi pamoja kuwekeza katika ubunifu barani humu.

“Safari yangu ya wiki moja barani Afrika ni kutambua kwamba nchi za Afrika ni muhimu kwa mafanikio ya dunia na ulinzi na mawazo na ubunifu wao vina manufaa kwa dunia,” ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter.

Katika ukurasa huo, ametoa orodha ya nyimbo 25 anazosikiliza akiwa kwenye ziara hiyo za wasanii wa Tanzania, Ghana na Zambia ukiwamo Mahaba wa Ali Kiba, Sawa wa Jay Melody, Single Again wa Harmonize, Utaniua wa Zuchu na Shetani wa Mbosso akiwashirikisha Alfa Kat na Costa Titc.

Rais Samia anatarajia kumpokea kiongozi huyo Ikulu Dar es Salaam kesho na baada ya mazungumzo yao, kiongozi huyo anatarajiwa kuweka shada la maua katika Makumbusho ya Taifa, kuashiria kuwakumbuka waathirika wa mabomu yaliyolipuliwa kwenye Ubalozi wa Marekani, Dar es Salaam mwaka 1998.

Pia kesho Kamala anatarajiwa kutembelea Taasisi ya Tanzania Startup Association, kukutana na wajasiriamali vijana na baadaye atashiriki futari iliyoandaliwa na Rais Samia katika Ikulu ya Magogoni.

Juzi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax alisema Kamala anakuja kwa mwaliko wa Rais Samia walipokutana Washington D.C Aprili mwaka jana wakati wa ziara yake ya kikazi nchini Marekani.

Pia alisema kiongozi huyo anakuja kutekeleza ahadi iliyotolewa Desemba mwaka jana na Rais wa Marekani, Joe Biden wakati wa mkutano wa kilele kati ya Marekani na viongozi wa Afrika.



Chanzo: HabariLeo
 
UVCCM - TAIFA
MACHI 29, 2023

UJIO WA KAMALA HARRIS MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI

Nchi ya Tanzania inakwenda kuandika historia isiyofutika kutokana na diplomasia imara iliyojengwa chini ya Uongozi madhubuti wa Rais Mhe. Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN

Kamala Harris anatembelea Tanzania akiwa ni makamu wa kwanza wa Rais mwanamke kuwahi kutokea nchini Marekani huku mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan akiwa mwanamke wa kwanza kuwa Rais nchini Tanzania.

#AlipoMamaVijanaTupo
#CCMImaraSerikaliMadhubuti #KulindaNaKujengaUjamaa
#KaziIendelee
IMG-20230329-WA0008.jpg
IMG-20230329-WA0174.jpg
 
Kiswahili sahihi ni Uwanja wa Ndege (Sio KIWANJA CHA NDEGE) halafu umepatia kwenye wa Julius Nyerere.
Watangazaji wengi wanakosea wanauita uwanja wa Mwl. Julius Nyerere (Ni Julius Nyerere sio Mwl)
 
HATUTAKI USHOGA, HATUTAKI USHOGA.


ZIARA YAKE YA GHANA, KAZUNGUMZIA SUALA LA MASHOGA.

HATUTAKI USHOGA ..

YEYE SAMIA KAMA ANAONA UONGOZI NI KAZI, AACHE, AACHE UONGOZI TUPATE MTU ATAKAYEPINGA USHOGA WAZI WAZI


UJUMBE HUU UMFIKIE SAMIA POPOTE ALIPO
 
Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, anawasili leo Tanzania kuanza ziara ya kihistoria ya siku tatu (Machi 29-31, 2023).

Ujio wa kiongozi huyo mkubwa wa Marekani nchini ni ishara ya mafanikio makubwa ya mageuzi ya diplomasia ya uchumi na ushirikiano wa kimataifa yanayofanywa na Tanzania tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani miaka miwili iliyopita.
 

Attachments

  • IMG-20230329-WA0005.jpg
    IMG-20230329-WA0005.jpg
    84.4 KB · Views: 5
  • VID-20230329-WA0003.mp4
    11.3 MB
Na Bwanku Bwanku.

Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, anawasili leo Tanzania kuanza ziara ya kihistoria ya siku tatu (Machi 29-31, 2023).

Ujio wa kiongozi huyo mkubwa wa Marekani nchini ni ishara ya mafanikio makubwa ya mageuzi ya diplomasia ya uchumi na ushirikiano wa kimataifa yanayofanywa na Tanzania tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani miaka miwili iliyopita. Baada ya kupokelewa Ikulu na Rais Samia Suluhu Hassan siku ya Alhamisi Machi 30, 2023 na kujadili masuala mbalimbali yanayogusa biashara, uwekezaji, utalii, elimu, afya na utunzaji mazingira, pia atashiriki matukio matatu nchini.

Kwa Mujibu wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Marekani imewekeza Tanzania kwenye miradi ya zaidi ya Trilioni 10 iliyotoa ajira zaidi ya 50,000 kwa Watanzania. Hivyo, ziara kama hii inafungua fursa zaidi za uwekezaji na biashara ili Taifa lipate maendeleo.

Bi. Kamala Harris akiwa kwenye ziara nchini Tanzania ataweka shada la maua katika Makumbusho ya Dar es Salaam kama ishara ya kuwakumbuka wahanga wa mabomu yaliyolipuliwa na Ubalozi wa Marekani mwaka 1998, kutembelea Taasisi ya Tanzania Startup Association ya Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukutana na Vijana Wajasiliamali na baadae kushiriki futari iliyoandaliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa heshima yake.


IMG-20230329-WA0009.jpg

FB_IMG_1680100237211.jpg
 
UVCCM - TAIFA
MACHI 29, 2023

UJIO WA KAMALA HARRIS MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI

Nchi ya Tanzania inakwenda kuandika historia isiyofutika kutokana na diplomasia imara iliyojengwa chini ya Uongozi madhubuti wa Rais Mhe. Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN

Kamala Harris anatembelea Tanzania akiwa ni makamu wa kwanza wa Rais mwanamke kuwahi kutokea nchini Marekani huku mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan akiwa mwanamke wa kwanza kuwa Rais nchini Tanzania.

#AlipoMamaVijanaTupo
#CCMImaraSerikaliMadhubuti #KulindaNaKujengaUjamaa
#KaziIendeleeView attachment 2569784View attachment 2569785
Apewe na kadi ya chama pendwa pia🤣😂
 
Maana mara ya kwanza nilisikia kuwa anakuja saa 4 usiku, sasa inasikika kuwa anakuja 5:40 usiku. Huku si kukesha huku? Maana hapo kumkaribisha, kumsalimia pamoja na kumfikisha na kumuelekeza malazi ifafika saa 8 usiku.

Poleni kwa mapambano viongozi wetu.
 
Back
Top Bottom