Ujio wa Makamu wa Rais wa Warekani sio bahati mbaya

Haya mambo hayatokei kwa bahati mbaya! Rais Samia Suluhu amerudisha sana heshima ya Tanzania kwenye diplomasia na sasa imerejea mahali pake, Serikali ya awamu ya tano ilififisha mahusiano kati ya Tanzania na nchi nyingi lakini Rais Samia Suluhu alipoingia madarakani amefanikiwa kuimarisha diplomasia iliyoanzishwa na watangulizi wake na sasa Tanzania tunaendelea kunufaika kupitia uhusiano huu.

Ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris nchini itaimarisha na kufungua zaidi fursa za biashara na uwekezaji.

FsPCPmVWcAMtPUk
Usisahau sasa mahusiano ystaboreshwa ikiwa ni pamoja na haki za LGBTQ. Usisahau Kamara Harisd ni muumini wa LGBTQ!
 
Mtakuja kushangaa ule mpango wao wa kujenga kambi ya kijeshi Kigamboni unaendelezwa wana kigamboni jiandaeni kwa fidia maana wakisema wanaendeleza Plan mtafukuzwa anytime
Mzee baba unazungumziaje ndoa za kulana vijambio? Na hasa ukihusianisha na ujio wa Kamala Harris.
 
Usisahau sasa mahusiano ystaboreshwa ikiwa ni pamoja na haki za LGBTQ. Usisahau Kamara Harisd ni muumini wa LGBTQ!
Hilo suala hatuwezi kulikubali maana sisi tunachokiangali ni uhusiano wa kibiashara na uwekezaji pamoja na kuimarisha uchumi wa taifa letu hayo mengine yaishie uko uko kwao hatuwezi kujivika laana hiyo
 
Alipokuja Oboma wakati wa Kikwete 2013 tulipata nn said ya Obama kutuambia tu tukubali mapenz ya jinsia moja.Alipokuja Bush tulipata nn? Anakuja Kamala kusisitiza ushoga ndio maana mama hataki kupinga.Tafakali ndugu yangu .Acha kuandika vitu visivyo na maana.
Nimetafakari na nimeona ujio huu utaimarisha zaidi uhusiano wa kibishara, uwekezaji na utalii na sio vingine hilo suala la ushoga halikubaliki kwa nchi yetu na Rais Samia Suluhu analikemea wazi kabisa
 
Hilo suala hatuwezi kulikubali maana sisi tunachokiangali ni uhusiano wa kibiashara na uwekezaji pamoja na kuimarisha uchumi wa taifa letu hayo mengine yaishie uko uko kwao hatuwezi kujivika laana hiyo
Kwa kifupi wewe ni muumini wa msemo wa "Baniani mbaya, kiatu chake dawa"! Ahahahahaha!!!
 
Mimi nachokiona watanzania tutanufaika zaidi na ziara hii maana lazima Marekani aongeze uwekezaji Tanzania na hii itasaidia kutuinua kiuchumi na kuzalisha ajira nyingi zaidi maana

hadi sasa watanzania Zaidi ya 50,000 wamepata ajira za moja kwa moja kupitia uwekezaji wa TZS trilioni 10.97 uwekezaji huo uliofanywa na marekani
Uwekezaji gani huo ambao haujulikani bwashee..USA ni wahuni tu wanaojipenyeza kupitia demokrasia.
 
Tanzania Kwa Marekani ni jicho la mbali ndio maana ilikuwa nchi ya kwanza kuweka ubalozi baada ya uhuru
 
Marekani ameshasaidia Taifa lipi la mfano likainuka? Waanze na Haiti! Taifa la kinafiki linaloangamiza dunia kwa sera mbovu zinazolazimishwa na ubabe wao.

Kama hata sisi binadamu tulivyo na maadui ili watutie adabu tumrudie Mungu, ndivyo Marekani nao lazima kuwe na akina Putin kuwapunguza upunguani wao.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
China
 
Haya mambo hayatokei kwa bahati mbaya! Rais Samia Suluhu amerudisha sana heshima ya Tanzania kwenye diplomasia na sasa imerejea mahali pake, Serikali ya awamu ya tano ilififisha mahusiano kati ya Tanzania na nchi nyingi lakini Rais Samia Suluhu alipoingia madarakani amefanikiwa kuimarisha diplomasia iliyoanzishwa na watangulizi wake na sasa Tanzania tunaendelea kunufaika kupitia uhusiano huu.

Ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris nchini itaimarisha na kufungua zaidi fursa za biashara na uwekezaji.

FsPCPmVWcAMtPUk
Nini nchi ilifanikiwa ujio wa hao washenzi?,vyandarua?

Tumieni akili kidogo mungu aliyowazawadia kupambanua mambo,

Ndani ya muda mchache rais hayati Magufuli amefanya Makubwa bila ziara za hao LBGTQ
 
Nini nchi ilifanikiwa ujio wa hao washenzi?,vyandarua?

Tumieni akili kidogo mungu aliyowazawadia kupambanua mambo,

Ndani ya muda mchache rais hayati Magufuli amefanya Makubwa bila ziara za hao LBGTQ
Acha kukaza ubongo mzee Rais Samia Suluhu amefanya maendeleo mengi sana tena kwa kipindi cha miaka 2 tu imagine akifikisha miaka 5 au zaidi itakuaje

Asilimia kubwa ya nchi za Afrika zinapata msaada na mikopo kutoka Marekani kwahiyo mikopo na misaada haiepukiki kwa ajili ya maendeleo lakini pia Mwendazake alikua anakopa sana ila kwa siri
 
Ziara zote za viongozi wa Marekani lazima ziwe na maslahi fulani kwa walipa kodi wa taifa hilo.

Kazi iko huku kwetu ambako viongozi wengi hawaonekani kuwa na malengo yoyote ya kuwafaidisha wananchi wao katika majukumu yao ya kawaida achilia mbali wakifanya ziara huko ughaibuni.
 
Back
Top Bottom