Kwanini Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris anafanya ziara yake nchini Tanzania?

Maryam Malya

Senior Member
Nov 29, 2021
115
258
Leo Taifa la Tanzania litampokea Makamu wa Rais wa Marekani Bi Kamala Harris ambaye atafanya ziara ya siku tatu nchini ikiwa na lengo la kuimarisha Mahusiano baina ya Tanzania na Marekani.

Yapo masuala mbalimbali yaliyochagiza ujio wa Bi Kamala nchini Tanzania ikiwemo:

1: Kuimarika kwa Diplomasia na hili ni jambo kubwa ambalo Rais Samia amefanya juhudi kubwa katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani tangu aingie Madarakani.

2: Mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Marekani hususan katika nyanja mbalimbali za kukuza uchumi katika uwekezaji, Biashara, elimu, afya,pamoja na utunzaji wa Mazingira.

Ikumbukwe Marekani imesajili zaidi ya Miradi 266 katika kituo cha Uwekezaji nchini TIC yenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 4,778.6 na imetengeneza ajira 54,584 kwa Watanzania.

Na kadiri mahusiano yanavyozidi kusonga mbele ndivyo fursa mbalimbali zinavyozidi kufunguka kwa watanzania katika sekta mbalimbali.

Tukae Macho Watanzania huu ndo muda muafaka wa kumsaidia Rais Samia kuitangaza Tanzania yeye amefanya kwa nafasi yake kubwa zaidi kupitia Filamu ya Tanzania The Royal Tour sasa wameanza kuja viongozi wa juu, Shime shime tutumie hii fursa maana jicho lote lipo Tanzania mara baada ya Kamala kutangaza atazuru nchi yetu tujitangaze kwa mazuri zaidi na kutumia fursa hii kwani atakuja na ujumbe wa kutosha hivyo ni nafasi kubwa katika Sekta ya Utalii.

Vyombo vya Habari bila shaka ujio wa Bi Kamala ndio utakuwa kipaumbele kwa kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji ili wengine waone na waje kwa wingi.
 
Kwanini bibi tozo toka amekuwa Rais ameshaenda Marekani zaidi ya mara 10 na wakati hata mkoa wa Mara hajawahi kukanyaga miaka 2 sasa?
 
Leo huyu bibi Samia analo Yule mamawa USA anakazia sana ushoga. Sasa, Samia atakubali au atakataa. Kama akikubali atapata aibu kubwa kwa Watanzania. Hakikataa tu sanction inamutafuna. Bibi tozo Leo unalo.
 
Kilichomleta Ni ishu ya ushoga baada ya Uganda kupitishwa Sheria ya kuwakata mashoga na ushoga. Amekuja kutuliza Hali.

Mke wa Rais Biden alikuwa Kenya pia ishu ni hiyo hiyo , kutuzuia tusifuate mkumbo wa Uganda.

Sijui msimamo wa Rais wetu kuhusu ushoga.
 
Kilichomleta Ni ishu ya ushoga baada ya Uganda kupitishwa Sheria ya kuwakata mashoga na ushoga. Amekuja kutuliza Hali.

Mke wa Rais Biden alikuwa Kenya pia ishu ni hiyo hiyo , kutuzuia tusifuate mkumbo wa Uganda.

Sijui msimamo wa Rais wetu kuhusu ushoga.
Bibi tozo ana aibu sana
 
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom