Ujio mpya wa Ndugu Paul Makonda ndani ya CCM ni mfano wa Injili ya Mtume Paulo katika Biblia

Wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
5,432
11,101
Kipekee kabisa natumia fursa hii tena kuutazama uteuzi wa Paul Makonda kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM kama dhamira njema ya Rais SS Hassan kuisogeza CCM karibu na wananchi hasa katika kusimamia watendaji wa serikali ili CCM kupitia Serikali yake iweze kutimiza ahadi zake na malengo kwa wananchi, ilani ya CCM ni muhimu iende sambamba na usimamizi bora na utekelezaji tarajiwa.

Nikihuisha uteuzi wa ndugu Paul Makonda kama ujio wa mtume Paulo anaekuja kuongeza na kuimarisha imani ya Watanzania kwa CCM chini ya Rais SS Hassan hasa katika kusimamia utekelezaji madhubuti wa miradi mkakati kwa kuweka macho thabiti ya secretariat ya CCM.

Ndugu Paul Makonda naamini Utafanya vema kabisa katika kukemea viongozi wazembe katika usimamizi wa miradi ya maendeleo na utekelezaji wa ahadi ndani ya ilani ya chama pasipo kumuonea haya na kumuogopa awaye yeyote.

Mungu akawe pamoja nawe ndugu Makonda inshallah 👍👍👍

Na ikawe heri yenye mavuno kwa mamlaka ya uteuzi ukitendea vema nafasi hii nzuri.

Hii ndio CCM ambayo nitajivunia bila kupepesa macho.

Wadiz
 
Back
Top Bottom