Uingereza: Waandamamaji wapanda juu ya paa la nyumba ya Waziri Mkuu. Hapa Tanzania hata Dp world wauziwe nchi hamuwezi kuthubutu

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
1,126
4,169
Wanaharakati wamefunika sehemu ya mbele ya jengo hilo kwa kitambaa cheusi

1691081110174.png
Wanaharakati wamepanda juu ya paa la nyumba ya waziri mkuu katika eneo bunge lake la NorthYorkshire kupinga vibali vipya 100 vya mafuta na gesi ya Bahari ya Kaskazini.

Wanaharakati hao wa Greenpeaceiwalisema walikuwa wamefunika "kitambaa cheusi cha mafuta" upandemmoja wa nyumba ya bw sunak Kirby Sigston, karibu na Northallerton.

Ofisi ya Bw Sunakilithibitisha kuwa yeye na familia yake hawakuwapo kwenye nyumba hiyo wakati watukio hilo. Wanaharakati wanne walitumia ngazi kulifikiapaa kabla ya kutandaza kitamba kwenye jengo la makazi ya waziri mkuu, kuonyeshahisia zao juu ya athari za kibali hicho.

Watu hao wanne walishukasaa saba na robo mchana kwa saa za Uingereza na mara moja wakawekwa ndani yagari la polisi. Bw Sunak na familia yake wakolikizoni huko California.

Mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje wa chama cha Conservative katika bungee la Uingereza Alicia Kearns alisema hatua hiyo "haikubaliki".

Alisema nyumba za familia za wanasiasa hazipaswi "kushambuliwa". Mmoja wa waandamanaji hao, Philip Evans, aliiambia BBC: "Tuko hapa kumletea waziri mkuu madhara makubwa ya hali mpya ya kuchimba visima katika Bahari ya Kaskazini."

Bw Evans alikataa kusema jinsi wanaharakati hao walivyoweza kuifikia nyumba hiyo.
 
Waandamananji wana PPE za kujilinda unafikiri hao ni raia wa kuambiwa mkataba ni mbovu lakini tumtetee mwenzetu.
Hao itakuwa ni watu wa mfumo. Hata sisi siku kundi hilo likiamua kuandamana ndo tutakuwa na Uhuru wa kweli
 
Back
Top Bottom