No. 10 Downing; Makazi ya Waziri Mkuu yenye ushawishi mkubwa duniani

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
NO. 10 DOWNING; MAKAZI YA WAZIRI MKUU YENYE USHAWISHI MKUBWA DUNIANI.

Na. Comred Mbwana Allyamtu (CMCA)
Tuesday-22/02/2022
Marangu, Kilimanjaro, Tanzania

Katika jiji la London kuna kitongoji maarufu kinaitwa Westminster, ndani ya kitongoji hicho kuna mtaa maarufu uitwao Downing Street, mtaa huu upo kwenye Barabara ya Downing, ndani ya barabara hii kuna jengo maarufu duniani liitwalo "No10 Downing" wengi hupaitwa "Namba 10 Downing street", hapa No 10 Downing street ndipo ilipo nyumba au makazi na ofisi ya Waziri mkuu wa Uingereza.

Hapa Namba 10 Downing Street, kama nilivyosema awali ndio makazi na ofisi rasmi za mawaziri wakuu wa Uingereza tangu mwaka 1735, ikulu hiyo inashika namba mbili duniani kwa ikulu zenye ushawishi duniani, ikiwa nyuma ya Ikulu ya White House ya Marekani, hii Inamaana kwamba No 10 Downing street ni jengo la pili duniani kwa muhimu wa kisiasa ulimwenguni, hii ni kutokana na nafasi ya taifa la Uingereza duniani.

Lakini linashika namba moja duniani kwa kuwa makazi ya Waziri mkuu yenye ushawishi mkubwa, nafasi ya pili ikishikwa na makazi ya Waziri mkuu wa Japan yaitwayo "Sōri Daijin Kantei" au "Kantei (官邸)", kisha makazi ya waziri mkuu wa India yaitwayo "7 Lok Kalyan Marg", alafu Canada, Israel, Italy na Australia.

Jengo hilo la No 10 Downing street limetumika na mawaziri wakuu 77 kwa zaidi ya miaka 275 mpaka sasa, Baadhi ya mawaziri wakuu mashuhuri wa kisiasa na kihistoria nchini Uingereza wameishi na kufanya kazi katika makazi ya Nambari 10, wakiwemo Robert Walpole, Pitt Jr, Benjamin Disraeli, William Gladstone, David Lloyd George, Winston Churchill na Margaret Thatcher.

Ikulu ya Nambari 10 ndio makazi rasmi ya Waziri Mkuu wa Uingereza, pia ndio ofisi ya shughuri zote za waziri mkuu, Jengo hilo ni kubwa zaidi kuliko linavyoonekana kwa mbele, ukifika kwenye jengo hilo kwa mbele utakutana na mlango mweusi, kwenye huu mlango mweusi najua wengi hawaelezi maana hasa ya mlango huo kuwa na rangi nyeusi, Je unafahamu maana ya rangi nyeusi ya mlango huo?

OK iko hivi...

Rangi nyeusi ya mlango wa mbele wa jengo la 10 Downing street inamaanisha (most important decisions affecting Britain pass "black door") yani ni kwamba geti hilo ndipo mahala ambapo maamuzi magumu ambayo hufanywa ima yawe mabaya au mazuri yatapitia lango hilo kuja kwa umma, waingereza wana msemo kuwa lango hilo limebadirika rangi na kuwa jeusi kutokana na kupitisha mambo mazito ya Uingereza yani "Dark hell gate".

Hivyo basi rangi nyeusi ya mlango huo huashiria kuwa hapo ndio mahali ambapo mambo yote magumu na mapesi hupita, japo hakuna uhusiano wa mambo hayo na rangi hiyo nyeusi (nadhani ni utamaduni wa utani wa Uingereza)

Ukiachilia geti hilo, jengo hilo lina takriban vyumba 100, kutilia ndani makazi binafsi ya Waziri mkuu, pia kuna vyumba maalumu kwajili ya matumizi ya waziri mkuu yapo ghorofa ya tatu hapo ndipo Waziri mkuu na familia yake huishi kwa kipindi chote awepo kwenye jengo hilo, ghorofa zingine zinazo baki zina ofisi na kumbi za mikutano, maeneo ya mapokezi, vyumba vya ofisi ambapo waziri mkuu anafanya kazi, na mawaziri wa serikali, pia kuna sehemu maalum ambapo viongozi wa kigeni hukutana.

Kwa nyuma ya jengo hilo kuna ua wa ndani na bustani ya ½ ekari (0.2 ha), ambapo bustani hiyo utazama eneo la St James's Park, Nambari 10 Downing street ina ukubwa wa eneo la takribani ½ km² sawa na mita 500, kwa upande wa kulia kuna lango jekundu la siri (red door) ambalo hutumiwa kwenda Buckingham Palace, makazi rasmi ya mfalme wa Uingereza au makao ya Mfalme wa Uingereza, njia ya mbele pia hutumiwa na waziri mkuu kwenda na kurudi kutoka Palace of Westminster, bunge la Uingereza mahali ambapo Waziri mkuu ni kiongozi wa shughuri za bunge.

Jengo la Downing Street iliunganishwa na jengo kubwa na la kifahari nyuma yake mwanzoni mwa karne ya 18, na kuifanya Ikulu hiyo kueenea upande wa kushoto wa mlango wa mbele, na imechukua sehemu kubwa ya 12 Downing Street na 11 Downing Street mkabala na makazi rasmi ya waziri wa fedha na gavana wa benk kuu na Chansela wa Hazina.

Chimbuko la jengo la 10 Downing Street...

Eneo la Downing Street miaka mingi huko nyuma halikuwa likifahamika kwa jina hilo ila makazi ambayo Downing Street ipo ilikuwa ni makazi ya Warumi wa kale, Anglo-Saxon na Norman, Warumi walikuja Uingereza kwa mara ya kwanza chini ya kaisari Julius Caesar mwaka wa 55 KK, Wakaweka makao yao makuu katika moja wapo ya kisiwa kwenye mto Londinium, Warumi walichagua Kisiwa cha Thorney, karibu na makutano ya mto Thames kama mahali pa makazi yao rasmi.

Makazi haya ya Warumi, na yale ya Anglo-Saxons na Normans waliyo yaanzisha hayakufanikiwa sana, Eneo hilo lilikumbwa na ugonjwa wa tauni, pia kuanguka kwa utawala wa kiroma ulifanya eneo hilo kutoendelea, baadae Mfalme wa Uingereza Mercian wa mwaka 785 akapendekeza kuhamisha makazi ya wasaidizi wake (mabunyenye) eneo la kuta za mto thames.

Baadae Mfalme Canute aliyetawala Uingereza kuanzia mwaka 1017 hadi 1035 alijenga jumba katika eneo hilo la Downing ya leo, lakini jumba hilo lilitumika kama eneo la mfalme binafsi, eneo hilo liliendelea kubakia hivyo hata kipindi cha Edward the Confessor alitawala Uingereza mwaka 1042 hadi 1066 na William Mshindi aliyetawala Uingereza mwaka 1066 hadi 1087 walidumisha utamaduni wa kutumia jumba hilo lilojengwa ilipo Downing leo.

Kipindi hicho ndio eneo la Westminster lilianziashwa kama eneo la utawala na kitovu cha serikali, kipindi hicho ndio jengo la Whitehall lilijengwa, jengo hili la Whitehall ndio lilitumiwa na Chief lord of the Royal kama makazi rasimi, ikumbukwe kwamba kabla ya cheo cha uwaziri mkuu kuanzishwa msaidizi mkuu wa mfalme na jemedari mkuu alitumia jina la cheo cha Chief Lord of the Royal, huyu ndio alikuwa kama Waziri mkuu wa sasa, hivyo jengo la Whitehall na St James’s Park yalitumika kwa matumizi ya malords.

Ujenzi wa eneo la Downing Street...

Jengo la kwanza lilojengwa kwenye kitongoji ambacho baadae kilikuja kuitwa Downing Street ilikuwa ni kiwanda cha bia cha Axe kilichomilikiwa na ukoo wa Abbey of Abingdon katika miaka ya 1500.

mfalme Henry VIII aliyetawala Uingereza mwaka 1509 hadi 1547 ndie hasa aliye anzisha ujenzi kwenye mtaa wa Downing (japo ilikuwa aijaitwa jina hilo, kwanza aliipanua jengo la Whitehall Palace, akaweka Mbuga ya St James's, japo eneo hilo baadae liliharibiwa na moto mnamo mwaka 1698.

Baadae nyumba ya kwanza ikajengwa kwenye kiwanja ambapo Ikulu ya Downing ipo sasa, nyumba hiyo alizawadiwa Sir Thomas Knyvet mnamo mwaka 1581 na Malkia Elizabeth I aliyetawala Uingereza mwaka 1558 hadi 1603, huyu Thomas Knyvet alikuwa mmoja ya watu waliopendwa zaidi na Malkia Elizabeth l na pia alikuwa mbunge wa Thetford aliteuliwa kuwa Chief Lord of Westminster aliishi kwenye jengo hilo mpaka mwaka 1605 alipo uwawa kwa kupigwa risasi na Mfalme James I aliyetawala Uingereza mwaka 1603 hadi 1625 kwa tuhuma ya kutaka kuasi, baada ya kuuwawa kwa Thomas Knyvet jengo hilo akapatiwa mpwa wao, Elizabeth Hampden ambaye aliendelea kuishi hapo kwa miaka 40 iliyofuata.

Kufatia kuibuka kwa machafuko ya kisiasa katika karne ya 17 baada ya wabunge kumpinga Mfalme Charles I aliyetawala 1625 hadi 1649 ambapo maasi hayo yaliongozwa na Oliver Cromwell, nyumba ile iliuzwa kwa mkataba wa kulipia Kodi na kununuliwa na bwana mmoja aliyeitwa George Downing.

Hapa sasa ndio Jina Downing likaanza kutumika rasmi, ilikuwaje?

Ilikuwa hivi...

Ilipo jengo la ikulu ya leo ya No 10 Downing Street ilianza toka mwaka 1682 ambapo bwana George Downing tajiri na mfanyabiashara mkubwa jijini London kipindi hicho alinunua nyumba na kiwanja Mali ya familia ya Knyvet na kuanza kujenga majengo kwajili ya kupangisha (estate apartments), mwanzo akajenga nyumba 6 zenye kupendeza, kufatia hilo mtaa huo ukapewa Jina la Downing kufatia Jina la mmiliki wa nyumba hizo.

Pakazoeleka eneo hilo kuwa ni Downing, kurejelea Jina la tajiri George Downing, Mnamo mwaka 1682 akamuajiri muhandisi Sir Christopher Wren kujenga nyumba ya ghorofa na kubomoa nyumba tatu za chini, Kati ya mwaka 1682 na 1684 nyumba hiyo ya ghorofa ikakamilika na kuwa nyumba ya kwanza ya ghorofa 3 kujengwa eneo hilo maana awali zilikuwa nyumba za chini na ghorofa 2 tu, hivyo jengo hilo ndio likawa jengo la kwanza kubwa na la kuvutia, jengo hilo ndio baadae likaja kuwa No 10 Downing.

Lakini kwa kipindi hicho lilijulikana kama No 5 Downing, baadae zikajengwa nyumba 20 mahali hapo na kuifanya nyumba hiyo kubwa kubadilishiwa namba na kuitwa namba 10, mmiliki wa nyumba hizo alijenga kwajili ya kuzipangisha, na alipangisha watu maarufu jijini London kama Yarmouth aliishi Nambari 10 kati ya mwaka 1688 na 1689, na kufuatiwa na Lord Lansdowne aliyeishi 10 Downing kutoka mwaka 1692 hadi 1696 na Earl wa Grantham kutoka mwaka 1699 hadi 1703, Mkazi wa mwisho kama mtu binafsi (mpangaji) kwenye jengo la 10 Downing alikuwa Bw Henones aliyeishi hapo mwaka 1730, baada ya hapo jengo hilo likanunuliwa na serikali ya mfalme George ll kufatia malalamiko ya mwanae kuwa eneo hilo mlango wake unaangalia dirisha ya chumba chake cha kulala hivyo kumfanya kupoteza utulivu.

Baada ya Mfalme George II kununua jengo hilo akaligawa kwa Sir Robert Walpole, ambaye alishikilia cheo cha Bwana wa Kwanza wa Hazina (first Lord of the Treasury) na Waziri Mkuu wa kwanza wa Uingereza, ikumbukwe kwamba Sir Robert Walpole Ndio mtu wa kwanza kuanza kutumia cheo cha Waziri mkuu wa Uingereza na ni kipindi cha mfalme George ll ndio nafasi ya uwaziri mkuu ilianzishwa kutoka ile ya awali ya kuitwa Chief Lord of the Royal.

Ila kuna kitu nataka uelewe hapa...

Licha ya Sir Robert Walpole kutambulika kama ndiye waziri mkuu wa kwanza wa Uingereza, hakuwahi kutumia cheo au jina la Waziri mkuu badala yake alikuwa akiitwa "First Lord of the treasury", rasimi cheo cha waziri mkuu kilianza kutumika rasmi na kutambulika kikatiba mnamo mwaka 1905 wakati wa utawala wa Waziri mkuu Henry Campbell-Bannerman.

Huko mwanzo wasaidizi na kemedari mkuu wa mfalme waliitwa Chief Lord of the Royal, nafasi hii ilianzishwa na mfalme John l mwaka 1250, baadae miaka ya 1470 wakabadirisha nafasi hiyo na kuwa first Lord of the Treasury na kisha Waziri mkuu (prime minister).

Turejee kwenye jengo la No.10 Downing.......

Mfalme George ll baada ya kumpatia Sir Robert Walpole jengo hilo kama zawadi lakini Walpole alikataa kupewa jengo hilo kama zawadi ya kibinafsi badala yake alimwomba mfalme alifanye jengo hilo kama makazi rasmi ya first lord of the treasury, toka hapo mpaka sasa utamaduni huo umeendelea mpaka sasa wa jengo la No 10 Downing kuwa makazi rasimi ya mawaziri wakuu wa Uingereza mpaka sasa, pia Jina Downing limebakia kuenzi muasisi wa jengo hilo na mtaa huo mpaka sasa.

Sir Robert Walpole alianza kuishi kwenye jengo la 10 Downing tarehe 22 Septemba 1735, alipo hamia hapo Walpole alianza kulifanyia mabadiriko jengo hilo kwa kuajiri mbunifu William Kent ambaye alianza kulikarabata na kupata muunekano unaoonekana mpaka hivi leo.

William Kent ilifanya kazi kubwa kwenye ukarabati wa jengo hilo, kwanza alianza na kuziunganisha ghorofa 2, kisha Lango kuu la kuingilia akalielekeza lilielekea kwenye Barabara ya mtaa wa Downing badala ya kuelekea kwenye jango la Walinzi wa mfalme wajulikanao kama walinzi wa Farasi, na pia Barabara ya Downing ikawa ndio njia kuu ya kupita kwenye jengo la No 10 Downing Street, Nyuma ya jengo hilo la Downing, Kent alijenga vyumba vipya vya kupokelea wageni muhimu, na akajenga ngazi isiyo ya kawaida, yenye pande 3, ambayo ngazi hiyo bado ni moja ya kivutio cha jengo hilo.

Toka hapo mpaka leo jengo la No.10 Downing ndani ya mtaa wa Downing Street umekuwa makazi rasmi ya mawaziri wakuu wa Uingereza, japo kuna mawaziri wakuu wanne waligoma kuishi kwenye jengo hilo.

Maboresho na Huduma za jengo la No.10 Downing Street..........

Jengo la 10 Downing liliunganishwa na huduma ya maji moto na mfumo wa maji mwaka 1877 chini ya waziri mkuu Benjamin Disraeli.

Jengo la 10 Downing Street liliunganishwa na umeme rasimi mwaka 1894 na kwa mara ya kwanza ikaunganishwa na huduma ya simu mwezi uiliofuata ya mwaka 1894 chini ya waziri mkuu William Gladstone.

Mwaka 1902 kwa mara ya kwanza Waziri mkuu wa Uingereza akaanza kutumi gari rasimi na kupewa Dereva rasimi wa kumuendesha, toka hapo Waziri mkuu atapaswa kuchagua kampuni ya gari itakayo tumiwa kwa kipindi chake cha uwaziri mkuu ila sharti tu kampuni hiyo iwe ya Kiingereza kati ya kampuni hizi Wolseleys, Humbers, Rovers, Daimlers au Jaguars.

Mwaka 1937 jengo la 10 Downing likawekewa mfumo wa kuingiza joto (central heating).

Mwaka 1963 jengo la Downing likafanyiwa ukarabati mkubwa wa maboresho ya mifumo ya utambuzi na ya kisasa zaidi.

Mwaka 1982 jengo la 10 Downing likaunganishwa na mfumo wa mawasilano na ikulu ya White house chini ya Waziri mkuu Margaret Thatcher.

Mwaka 1982 jengo la Downing likawekewa compute ya kwanza (micro-computer) na kufungiwa mfumo wa kuchapisha nyaraka unaojiongoza (microfilm reader) kwa mara ya kwamza.

Mwaka 1983 jengo la Downing lilifanyiwa ukarabati na watumishi wote kuunganishwa na mfumo wa computer.

Mwaka 1990 mfumo wa kuendesha vikao kwa njia ya video uliunganishw kwa mara ya kwanza.

Mwaka 2005 kwa mara ya kwanza makazi ya Waziri mkuu 10 Downing iliweka hadharani e-mail account ambayo inaruhusiwa kwa raia wa Uingereza kuwasiliana na Waziri mkuu wao.

Mwaka 2008 jengo la 10 Downing wakaanzisha online TV station, inayoitwa Number10 TV.

Hii ndio No. 10 Downing Street, Makazi ya Waziri mkuu yenye ushawishi mkubwa duniani...
.
Kwa kupata makala Zaidi wasiliana na Mimi WhatsApp 0679555526 uungwe group la Maktaba Kuu kwa gharama ya Tsh 3000/=.

Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copyrights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu

Kwa Tanzania
+255679555526 (WhatsApp).
+255765026057.
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com

Copyright 2022, All Rights Reserved.

Maktaba Kuu.View attachment 2130994
FB_IMG_1645803436625.jpg
View attachment 2130996View attachment 2130995View attachment 2130997View attachment 2130998
 
Huwa nikiona waziri mkuu anaingia kwenye hako kamlango najua anaingia ofisini tu kumbe ndio makazi rasmi,hebu tuwekee na picha ya ndani huko kwenye mabustani isije kuwa imekaa kama Kotaz
 
Hilitembele UK mwaka 2011 niliishi mjini unaitwa Hereford ,ila kuna siku wenyeji wangu walinipeleka hapo mahali pia hospitality aliyofia Rais. Wa kwanza wa TZ haiko mbali na hapo!!! Kiukweli ni pazuri
 
Ilipo jengo la ikulu ya leo ya No 10 Downing Street ilianza toka mwaka 1682 ambapo bwana George Downing tajiri na mfanyabiashara mkubwa jijini London
... asante sana. Sikuwahi kuwaza Downing lilikuwa jina la mtu. Kumbe na sisi tunaweza kuenzi wa kwetu; pale Tandale pana eneo linaitwa kwa Bibi Nyau, miaka 100 ijayo patakuwa mtaa mkubwa sana; aenziwe asisahaulike.
 
Back
Top Bottom