Uhusiano wa Franco na Mobutu

Uhusiano wa Franco na Mobutu

mkuu
Wakuu habarini za muda huu,

View attachment 717548
View attachment 717549

Zimeanzishwa thread nyingi kuhusu Franco na Mobutu, historia ya Mobutu imeelezwa na ya Franco pia, leo naleta historia ya uhusiano wa watu hawa wenye majina makubwa Africa na ulimwenguni, mwanasiasa na gwiji la muziki.

View attachment 717532
View attachment 717529

KUNYONGWA KWA KINA EVARISTE KIMBA

Mnamo mwaka 1965 Mobutu anakua rais wa Zaire na kuagiza kunyongwa kwa watu zaidi ya 6 wengi wao wakiwa mawaziri wa serikali aliyoipindua katika eneo la matonge jijini Leopold Ville (Kinshasa) kwa kosa la uhaini, mamilioni ya watu wanashuhudia hadharani, mmoja wao ni Franco, baada ya hapo Franco akatunga nyimbo iitwayo Luvumbu Ndoki (Luvumbu mchawi) hii ni hadithi ya kikongo kuhusu Mfalme Luvumbu aliyeuwa ndugu zake wa karibu kwa ajili ya kujinufaisha.

Nyimbo hii inaonekana na mamlaka kama dhihaka kwa mobutu kutokana na kitendo chake cha kunyonga mawazili wale Franco anakamatwa na kuachiwa alafu anakimbilia Brazaville kwa miezi 6 mpaka pale mambo yalipokuwa shwari.

AUNTHENTICATION POLICY (Zairenisation)

Mnamo mwaka 1971 mobutu anabadili jina la Congo kuwa Zaire, sarafu kua Zaire, pamoja na miji kuitwa majina ya kiafrika, Leopoldville inakua Kinshasa, Elizabeth Ville inakua Kisangani na kadhalika, kutokana na sera ya uafrika mpaka majina ya watu yanabadilishwa.

Bendi ya Franco, Tp Ok jazz inaandamana na mobutu nchi nzima kueneza sera ya mobutu na kutoa album iitwayo belela unthenticite na congress ya mpira.

MALIPO YA KAZI

Mobutu anampa Franco eneo la ardhi pale Kinshasa, Franco anajenga night club iliyoitwa un Deux trois, pia Mobutu baada ya kubinafsisha kampuni za kigeni anampa Franco kampuni ya muziki iitwayo mazadi.

JACKY NA HELEINE(nyimbo za Franco)

Franco añatoa nyimbo mbili Jacky na heleine ambazo serikali iliziona hazina maadili na kumpa Franco kifungo cha miezi 6 jela, na bar yake kufungwa miezi 2, alivobisha kua hazina maadili mama yake alisikilizishwa, yote haya yalifanywa na Kengo wa Dondo aliyekua attorney general.

Mobutu anamtoa jela Franco baada ya week 3 na kumshusha cheo Kengo wa Dondo kua balozi wa Zaire nchini Ubelgiji, Franco anaimba nyimbo ya kumponda Kengo iitwayo trailleur (anasema fundi nguo akikinyanganya sindano utawachomaje watu? Yaani kengo kaporwa madaraka na Mobutu)

Franco anaimba lettre a mr le directeur general (barua kwa director general) nyimbo ambayo añawaponda viongozi wa serikali kwa rushwa na usimamizi mbovu, hii inachukuliwa na wengi kama diss song kwa Mobutu.

Mwka 1984 anaimba nyimbo ya kumsifu Mobutu iliyoitwa Candida na biso, wakati wa uchaguzi ambapo watu walitakiwa kujibu ndio au apana kama wanamtaka Mobutu, hakukua na wapinzani.

Mobutu alifadhili band nyingi kubwa za muziki nchini Zaire, ikiwemo TP OK JAZZ


KIFO CHA FRANCO

Franco anafariki jijini Ubelgiji mwka 1989, Mobutu akiwa Ufaransa ziarani,
Mobutu anatangaza siku 4 za maombolezo na radio zote kupiga nyimbo za Franco tu, mwili wa Franco unapelekwa Palais du people kuagwa
View attachment 717547

Mobutu aliporudi aliitembelea familia ya Franco pamoja na kaburi.

Kwa kiasi kikubwa Mobutu alimtumia Franco katika ku mobilize watu kwenye siasa zake na pia Franco alinufaika sana kwa kuendesha magari ya kifahari kama mercedes benz na kuishi vizuri, kuliko wanamuziki wengi wa Congo na nje ya Congo
asante sana
 
Mkuu Lucas Mobutu sina nia ya kukosoa bandiko lako but hapo kwenye wimbo Candidat Na Biso Mobutu naomba niongeze nyama kidogo kuhusu huu wimbo.

Baada ya kutoa wimbo wa kumtuhumu rais Mobutu kwa uongozi wake wa mkono wa chuma iliamriwa Frànco akamatwe atiwe jela,kisha Mobutu akampa options mbili either atumie kipaji chake kutunga wimbo mzuri utakaomfanya azidi kupendwa na wananchi wake au aendelee kukaa jela{tukumbuke huu wimbo wa kum-dis Mobutu ulipokelewa vizuri sana na masahabiki wa Frànco so nikama aliambiwa atafute kitu cha kuyafuta yale mawazo mabaya kwa wananchi kisha apandikize mazuri yanayomuhusu yeye}.

Ndipo alipotunga huu wimbo canditad na biso Mobutu na inasemekana Mobutu alipousikiliza kwa mara ya kwanza tu aliamuru Frànco atolewe jela upesi sana na apelekwe ikulu ambako ilifanyika sherehe ya kukata na shoka kwa muda wa siku tatu kisha Mobutu akataka ampe Frànco madaraka ya kisiasa ambapo aliyakataa akaomba apewe ruhusa ya kufanya shughuli zake za kimuziki kwa uhuru tu.

Copied.......
Katika watu walokula nchi Mobutu huko nafasi ya juu sana!
Hakuna starehe ambayo hakuifanya.
 
Najisikia furaha kuona kumbe bado tupo tunaopenda mziki wa kweli.

Sijawahi wala sintopenda vitu vya ajabu na makelele mengi eti nayo yanaitwa mziki.
 
Franco kawafundsha mziki wanamzki kama vile
tabu ley
Sam mangwana
mpongo love
simaro lutumba
madiluu system nk japokuwa baadaye tabu ley alihama band ya okk jazz na kuanzisha yake iitwayo orchestra afrisa international ambayo ilichuana na OK jazz
ktk band hiyo wakina Sam mangwana walijiengua okk jazz na kujiunga na orchestra afrisa,miaka ya 1987 band ya okk jazz ikaanza kuyumba hii n kutokana na Franco kuwa nje ya nchi mda mrefu pia afya yake kuzorota
mwaka 1987 Franco aliimba wimbo akimshirikisha Sam mangwana wimbo uitwao muongo na mulozi huu wimbo n kama walikuwa wanaagana Franco alitoa mawaidha mazito ktk wimbo huu miaka miwili baadae akafariki

Tabu ley na Sam Mangwana wamefundishwa Muziki na Franko?
 
11947465_10153397322963891_1756629325684420805_n.jpeg
 
Kama kumbukumbu zangu ziko vizuri ni kwamba UKIMWI uliingia Afrika miaka ya 80, sasa ikawaje UKIMWI huo huo ambao tunambiwa na watalaam huchukua miaka nane tangu kuambukizwa ndo dalili zake zionekane ukagharimu maisha ya Franco ndani ya miaka hiyo ya 80..Niko tayari kurekebishwa..Vinginevyo shukrani zimwendee aliyetuletea historia hii na pia wale wote ambao hawakusita kuchangia pale ambapo waliona wana cha kuchangia na wale pia waliouliza maswali yaliyopelekea historia hii kuongezewa nyama.
Naomba nifafanue kwa kadri ya ufahamu wangu HIV iko aina 2 yaani 1 au 2 ,HIV 1 ndio iko sana Africa na more virulent (kali)na HIV 2 iko kwa wenzetu ulaya.
HIV ya mwanzo 1970 -80 's ilikuwa kali na life span baada ya kuambukizwa ilikadiriwa kuwa miaka 5 baadae miaka inavyosonga technology ya dawa inavyogunduliwa HIV wanapoteza nguvu siku hz mtu anaweza survive 10 bila ya dawa na mpk 30yrs akitumia dawa na akafa kwa natural causes.
Kipindi kile ilikuwa anakufa akiwa amekonda sana lkn siku hz mtu anaondoka akiwa na mwili.
 
Saddam wa Kongo anafurahisha sana na hio bunduki yake hahah,wkt baba yake anatolewa madarakani na wakina kagame sijui alikua wapi huyu saddam au kazi yake ilikua ni kubaka wanawake tu?

Thnxs for the history mkuu.
Wakati mzee wake anatolewa madarakani alikuepo zaire

Baada ya baba yake kutoroshwa(hakukimbia) ,kongulu alibaki kinshasa akaongoza kikosi cha baadhi ya walinzi wa baba yake,dsp(division spicialle presidentielle) kuua wasaliti wa baba yake

Inasemekana alimuua waziri wa ulinzi aliyeitwa gen mayele kwa risasi,

Hakuishia hapo,hata baada ya kuikimbia kinshasa,alianzisha kundi la kuwateka walio msaliti baba yake
 
Wakati mzee wake anatolewa madarakani alikuepo zaire

Baada ya baba yake kutoroshwa(hakukimbia) ,kongulu alibaki kinshasa akaongoza kikosi cha baadhi ya walinzi wa baba yake,dsp(division spicialle presidentielle) kuua wasaliti wa baba yake

Inasemekana alimuua waziri wa ulinzi aliyeitwa gem mayele kwa risasi,

Hakuishia hapo,hata baada ya kuikimbia kinshasa,alianzisha kundi la kuwateka walio msaliti baba yake
Kumbe alikua Coward mkuu,i thought angeingia msituni kupambana na serikali iliyopo madarakani ya kabila ili warudi madarakani ye akaenda kuteka watu,no wonder alikua anabaka wanawake aisee.Anyway lesson learnt.
 
Kumbe alikua Coward mkuu,i thought angeingia msituni kupambana na serikali iliyopo madarakani ya kabila ili warudi madarakani ye akaenda kuteka watu,no wonder alikua anabaka wanawake aisee.Anyway lesson learnt.
Ilimbidi akimbie kwanza coz hakua amejipanga kuunda jeshi la msituni,lengo lake lilikua kui defend kinshasa,
Sasa wanajeshi wakubwa wakawa wameshaisaliti serikali,kwa kukimbia na kutoa mipango ya siri ya kijeshi hivo hakua na jinsi

But baàda ya kukimbia aliunda kikosi cha kuikomboa congo,but akafa mapema,nadhani asingekufa angesumbua sana serikali mpaka leo
 
Back
Top Bottom