Uhusiano wa Franco na Mobutu

Uhusiano wa Franco na Mobutu

Mimi huwa zinanichanganya hizi Congo mbili, Brazzaville na Congo Kinshasa, hebu nipeni itofauti hapo, hawa wanamuziki kina Koffi, Werrason n.k wanaishi Congo ipi? Kabila anaongoza Congo ipi? Congo ipi ni maarufu kuliko nyingine na kwa nini?
wanamzk hao woote n wa Congo DRC
brazavile haina exposure kuzid DRC
 
Nakumbuka huu wimbo wa candinda nabiso mobutu, huwa nasisimka kabisa , maana inchini Zaire kulikua na sintofahamu kabisa kama mzee angeshinda uchaguzi , huu wimbo aliupigia Belgique Mobutu akatuma ndege kwenda mfuata Franco na jamaa akashinda uchaguzi kilaini Franco - Candidat na Biso Mobutu Song Lyrics, Music Video
Mobutu alifuja hela za nchi mno
hadi anakufa alikuwa na Pesa cash dola billion 3 za marekan achana na asset nyingne
hadi juz juz serikali ya uswiss ambalo kulikuwa na akaunt ya Mobutu waliamua kuwagawia hizo hela familia ya mobutu
 
mkuu ID yako imenikumbusha mwanamzk wa okk jazz alieitwa simaro lutumba masiya
alicharaza wimbo matata unaitwa Maya
Ile album ya Maya wenyewe wanaita "Album des albums" ilipigwa na OK Jazz tawi la Kinshasa wakati Franco na OK Jazz bendi kubwa wako ulaya. Kitu ile ilipotua mikononi mwa Franco ilibidi aite bendi nzima waisikilize na akawaambia anataka wajitume. Simaro ana nyimbo nyingi kali-bahati mbaya au nzuri-ni mtu muungwana sana, hajitutumui lakini vigongo vyake Luambo alivikubali hadi kumpa Chef D'Orchestre, Vice President na baada ya kufariki Franco akawa President of OK Jazz na Vice wake akiwa Josky Kiambukuta. Wanamuziki wenzake walimheshimu sana ndio maana familia ya Luambo ilipo mvua u-president, yeye aliamua kutoak OK Jazz na wanamuziki wote waliobaki wakaiacha bendi hapo hapo pamoja na Josky ambae familia walitaka awe President. Leo hii anapiga 80 years na anastaafu muziki baada ya miaka 60.
 
Siongo Bavon Marie Marie alifariki 1970. Alipata ajali baada ya kuto kuelewana na Kaka yake. Kwa uhakika wa kifo cha huyu bwana muulizeni Papa Chimanga Assosa wa Bana Marquiz (rafiki yake marehemu Bavon) mwanamuziki wa Zamani wa Negro Success kupitia RTD FM kipindi cha Kavasha Time yuko kila Jumamosi na Mtangazaji Nguli Mbazigwa Hassan. Hapo pia utapata taarifa nyingi na muziki wa zamani wa DRC. Si kweli kwamba Bavon alitaka kujiua.
hebu nifafanulie kidgo mkuu kuhusu sintofaham hiyo please
 
mke wa kwanza wa Mobutu aliejulikana kama Marie Antoine alifark mwaka 1977 kutokana na kipigo kutoka kwa Mobutu alikimbizwa hospital nchini uswiss lkn alifariki
watoto wawili wa Mobutu walikufa kwa ngoma
mmoja mwaka 1994(huyu ndie mtoto wake wa kwanza alizaliwa 1955)
meingine anaitwa kongulu Mobutu alifariki mjini Monaco 1998 huyu alizaliwa 1975 na alikuwa askari ktk kikosi cha kumlinda Mobutu alikuwa anabaka msichana yoyote amtakae hakukuwa na wa kumuuliza,akiamua anaenda shule anatafuta mwanafunz yyote anaenda kumla,mwishow ukimwi ulimmaliza
 
Ile album ya Maya wenyewe wanaita "Album des albums" ilipigwa na OK Jazz tawi la Kinshasa wakati Franco na OK Jazz bendi kubwa wako ulaya. Kitu ile ilipotua mikononi mwa Franco ilibidi aite bendi nzima waisikilize na akawaambia anataka wajitume. Simaro ana nyimbo nyingi kali-bahati mbaya au nzuri-ni mtu muungwana sana, hajitutumui lakini vigongo vyake Luambo alivikubali hadi kumpa Chef D'Orchestre, Vice President na baada ya kufariki Franco akawa President of OK Jazz na Vice wake akiwa Josky Kiambukuta. Wanamuziki wenzake walimheshimu sana ndio maana familia ya Luambo ilipo mvua u-president, yeye aliamua kutoak OK Jazz na wanamuziki wote waliobaki wakaiacha bendi hapo hapo pamoja na Josky ambae familia walitaka awe President. Leo hii anapiga 80 years na anastaafu muziki baada ya miaka 60.
aisee story nzuri sana hii
mzee simaro lutumba yy hakuangaika na sketi ndio maana ukimwi ulimuepuka
Franco aliwacharaza mademu mno
Sam mangwama pia nampenda mno sijui yupo wapi now
 
Madilu System alikuwa mwanamuziki wa Afrisa International ya Tabou Ley, ilipofika safari ya kwenda ulaya akachujwa kwa mizengwe akiwa Airport. Akaona enough is enough akaomba kujiunga na OK Jazz na Franco hakuwa na hiyana. Akawa mwimbaji pamoja na waimbaji vinara wa OK Jazz- Josky, Ntessa na wengineo. Alifanya hivyo kwa miaka takribani 2/3. Ilipotokea safari ya ulaya dakika ya mwisho akapata namba. Franco wakati huo ndo amemaliza project yake ya "Lisanga ya Banganga" ambayo ilitoa santuri si chini ya 6 akiwa na Tabou Ley, Mavatiku Vissi na Josky Kiambukuta. Akiwa huko ulaya akapata idea ya wimbo wa Non au "Libala oh Libala 1982/83. Akamjaribu Madilu kama ataweza kuuimba. Baada ya kuelekezana ndo mwimbo ule ukasukwa na madilu akapiga duet na Franco na pia kuimba solo vipande vingine. Sauti ya Madilu ikapaa na OK Jazz wakaonekana wamekuja vipya-Franco akanogewa ndo akawa anatunga nyimbo za style ile (pamoja na Mamouu, Mario etc). Hapo Madilu ndipo alipopanda chati hadi kufikia 1986 Josky na Ntessa wakazira kwani waliona Franco macho yake yako kwa Madillu tu. Wakatoka OK Jazz wakatoa nyimbo kama Selengina. Ntessa alirudi kwa style ya Collaboration na OK Jazz (Album kama mbili), Josky alijiunga tena na kuongoza kikosi cha waimbaji wa OK Jazz. Baada ya kutokuelewana kati ya Familia ya Franco (Dada Yake) na Papa Simaro Lutumba 1993 Familia wakamvua Simaro uongozi, ndipo wanamuziki wote wakaiacha OK Jazz wengi wao wakianzisha Bana OK chini ya uongozi wa Simaro. Madilu akaamua kwenda solo, lakini akahakikisha mdundo wake na karibu nyimbo zake zinafuata beat ya OK Jazz na Solo ya Luambo. Alijitahidi pia akajenga bendi yake Bana Syste ambayo ukisikiliza album zake utaona role model wake ni Luambo. Si tu alitembelea nyota ya Franco bali aliishi muziki wa Odemba (style ya OK Jazz). Mwenyewe alidai kila anapoingia studio-anamuona Luambo kazini akimwongoza. Ndogo ndogo inasema mama wa Madilu ni dada wa mke wa Simaro (Maman Kelani).
 
Kama kumbukumbu zangu ziko vizuri ni kwamba UKIMWI uliingia Afrika miaka ya 80, sasa ikawaje UKIMWI huo huo ambao tunambiwa na watalaam huchukua miaka nane tangu kuambukizwa ndo dalili zake zionekane ukagharimu maisha ya Franco ndani ya miaka hiyo ya 80..Niko tayari kurekebishwa..Vinginevyo shukrani zimwendee aliyetuletea historia hii na pia wale wote ambao hawakusita kuchangia pale ambapo waliona wana cha kuchangia na wale pia waliouliza maswali yaliyopelekea historia hii kuongezewa nyama.
 
Back
Top Bottom