Uhuru wa Habari Tanzania: Kati ya Waparaji na Wakunaji Wazuri, Nani Watamsaidia Zaidi Rais Samia?. Tunakuomba Mama, Usiwaparure Waparaji!.

Wanabodi,
Hii ni makala ya Jumapili hii
View attachment 2216032View attachment 2216034
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa"

Siku ya Mei 3 kila mwaka ni Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari. Nchini Tanzania, siku hii imeadhimishwa Kitaifa jijini Arusha, mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa JMT, Rais Mama Samia Suluhu Hassan, japo alisema mengi, Mimi kubwa lililonigusa ni hili...(nanukuu)

"Ukinikuna vizuri, mimi nakukuna huku nnakupapasa na kukupuliza ufuu...ufuu... Lakini "Ukinipara..., Nakuparura!", (mwisho wa kunukuu).

Naomba kuianza makala ya leo kwa kumkuna vizuri Rais Samia, Kwa pongezi kwa yeye Rais Samia, ndiye Rais wa kwanza wa Tanzania kuwa mgeni rasmi Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari kwa hapa nchini kwetu Tanzania.

Nimekuwa newsroom kwa zaidi ya miaka 30, hii ndio mara ya kwanza kwa event yetu wanahabari kuhutubiwa na Rais wa nchi. Kiukweli kabisa, Rais Samia, ametuheshimisha sana wanahabari!, asante sana Mama, kutuheshimisha sisi wanahabari, na sisi kwa upande wetu, tunakuahidi kufuata kanuni ya reciprocity, "ukipendwa, pendeka", "ukiaminiwa, jiaminishe" na "ukiheshimiwa, jiheshimishe".

Hivyo kwa jinsi Rais Samia alivyotuheshimisha sisi wanahabari, automatically na sisi wanahabari, tutamuheshimu, tutamkuna vizuri, sio ili atupapase na kutupuliza ufuu..., ufuu, no!, tutamkuna vizuri vile viwasho vinavyotokea sehemu za ngozi laini, vinavyohitaji ukunaji mzuri, ila kukitokea miwasho sehemu za ngozi ngumu, kama kwenye magaga, hakuna budi, ni lazima tutampara.

Kwa vile Rais Samia amethibitisha kuwa na yeye ana ngozi ngumu, ukitokea muwasho kwenye sehemu za ngozi ngumu kama kwenye magaga, hata ukune vipi, muwasho huo hauwezi kukunika ni lazima kumpara, hivyo ikitokea katika kumkuna, badala ya kumkuna vizuri, tukajikuta tumempara, tunamuomba sana Mama yetu, Mama Samia, asituparure!.

Pongezi zangu ziziishie kwa Rais Samia kutuhutubia, bali pongezi kwa vyama vyote vya Habari vikiongozwa na Jukwaa la Wahariri, TEF, MCT, MISA-Tan, TAMWA, TMF, UTPC na waandishi wenyewe wa habari.

Pongezi mahsus kwa Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile na Mwenyekiti mstaafu Absolom Kibanda, for their personal initiatives hadi...
Tena nilifurahi sana Rais Samia alipozungumzia SMS za Kibanda!.

Pongezi za tatu ni kwa Mama Samia, kuikuza lugha yetu adhimu ya Kiswahili kwa kutuongezea misamiati mipya from time to time.
Alianza na neno "Kudemka", likaja neno "mkinizingua, tutazinguana", sasa ni neno "kupara".

Kukuna na Kupara.
Kukuna: ni kujikuna mahali panapokuwasha,
Kupara: Kuchuna magamba ya samaki, Kupara samaki.

Kwenye kujikuna, mtu hawezi kujikuna mwenyewe mgongoni, hivyo mtu ukiwashwa mgongoni ni lazima umuombe mtu mwingine akukune, ili na siku yeye akiwashwa mgongoni na wewe pia utamkuna Kwa kanuni ya "Scratch my back, and I'll scratch yours".

Kwenye kukuna kuna kumkuna na Kukuna, kuna kumkuna mtu vizuri, anayekunwa vizuri, anajisikia Raha, na ukimkuna mtu vibaya, kwa makucha makali kama unapara samaki, anayekunwa anajisikia karaha, na huko ndiko alikokusema Mama, ukimpara, anakuparura!.

Mama Samia katuasa sisi waandishi, tukimkuna vizuri, na yeye atatukuna vizuri, ila tukimpara atatuparua!.

Kila kazi ina kanuni zake, yaani rules of engagement, miongoni mwa kazi za dakitari ni kutibu, katika kutibu, sometimes dakitari anatoa dozi ya kidonge kichungu au kukudunga sindano yanye maumivu ili upone.

Kazi ya media ni kuhabarisha, kuelimisha, kuburudisha, kukosoa na kuwajibika kwa jamii. Media haiwajibiki kukuna vizuri tuu bali kwenye yale ya kustahili kumkuna vizuri, tutamkuna vizuri, Rais Samia hadi kusikia Raha, ila yale yanayostahili kumpara, media hatuna jinsi, ni lazima tuu tutampara, kwa jinsi ile ile ya dakitari kutoa kidonge kichungu au kumdunga sindano mgojwa ili apone, hivyo ni wajibu wa media, kumkuna rais panapostahili kukunwa, na kumpara pale panapostahili kuparwa, Ila kwenye kupara, hatutampara kwa kisu kikali kama kumpara samaki, tutatumia lugha ya heshima,na unyenyekevu mkubwa.

Kati ya media itakayo andika habari za kumkuna vizuri tuu Rais, na media itakayoandika habari za kumpara rais, ni habari gani zitamsaidia zaidi Rais Samia na kulisaidia Taifa?.

Kati ya mtu anayekusifu tuu wakati wote na yule anayekusifu ukifanya mazuri, lakini ukikosea anakukosoa na kukushauri, ni yupi atakusaidia zaidi?.

Huku kukuna na Kupara, kwa lugha nyingine, wakunaji wazuri ni zile media na wale waandishi ambao kazi yao siku zote itakuwa ni kusifu tuu na kumwandika vizuri bila kumkosoa, halafu wapara ni zile media au waandishi watakao mwandika vibaya au kumkosoa. Enzi za JPM, niliwahi kuileta hoja hii
Hivyo sasa kwa vile Rais Samia nae kaja na hoja kama hii hii, naomba tuutumie utaratibu ule ule

Rais Samia nae ni binadamu na sio malaika, hivyo, kama binadamu ni haki yake kukosea, kwasababu nobody's perfect, the only perfect being is God!, hivyo Rais Samia kama Binadamu, kuna mahali anaweza kukosea au amefanya ndivyo sivyo, tupaseme sio kwa kubeza au kukejeli, bali kufanyike kwa heshima, kwa lugha ya staha na unyenyekevu kwa lengo la kutoa ushauri wa kusaidia, the right thing to do, hivyo ukosoaji kwa rais, ufanyike constructively kwa nia njema ya kujenga na sio kubomoa, yaani tufanye "a constructive criticism" in good faith kwaa nia ya kumsaidia rais wetu kuwa rais bora zaidi na kulisaidia taifa letu kusonga mbele na sio kurudi nyuma kwa sababu kwa mujibu wa katiba yetu, rais hawezi kukosea ndio maana hawezi kushitakiwa.

Rais ana sehemu mbili, rais ni taasisi ya presidential institution hivyo rais kama taasisi hawezi kufanya kosa lolote ni perfect being kila kauli yake ni sheria, inafuatiwa na utekelezaji tuu, lakini hiyo institution inashikiliwa na kuongozwa mtu ambaye ni binadamu tuu kama sisi anayeitwa Samia Suluhu Hassan, huyu ni binadamu wa kawaida kama sisi wengine wote, she is a human being, anaweza kukosea. Katika kumkosoa rais, tumkosoe kwa heshima in such a way tusije kujikuta tunakosa uzalendo, badala ya kumkosoa, tunamuaibisha na kujikuta tunajiabisha sisi kama taifa.

Enzi za JPM, kuna Mwandishi wa JF, Ben Saanane, alifanya IJ ya Ph.D ya mtu fulani. Ph.D za UDSM, zinasomewa kwa aina mbili, by thesis, or dissertation. Ph.D by thesis unaweza kuifanyia popote, lakini Ph.D by dissemination iliyochunguzwa imefanywa Full Time, ila hakuna wakati wowote mhitimu huyo alichukua likizo, hivyo Ben Saanane, akaichukua Ph.D yake hiyo, akaichambua jinsi ilivyo fanyiwa plagiarism. Ben Saanane just vanished into thin air!.

Azory Gwanda, Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mwananchi, aliandika makala jinsi watu wanavyoyeyuka kwenye familia mbalimbali huko Rufiki (Mkiru), mara na yeye siku moja, akafuatwa nyumbani kwake, akachukuliwa na gari jeupe Totara Landcruiser ya mkonga, akapotea jumla!.

Kuna siku kuna mwanasiasa fulani, aliitwa msaliti, mzungumzaji akasema wasaliti wa aina hii hawawezi wakaachwa kusurvive tuu!. Hazikupita siku mbili, yule mwanasiasa alimiminiwa pyu pyu za kutosha!, hivyo mtu mwenye kauli yenye mamlaka akisema ukinipara nitakuparura, itategemea utaparurwaje, kwa mtindo wa Ben Saanane, Azory Gwanda, kwenye viroba, au ki Lissulissu Kwa pyu pyu!, ndio maana tunamuomba Mama, haya ya kumparurana haya...

Naomba kauli hii ya Rais Samia, isitugawe sisi media na social media kugawanyika katika kambi mbili kuu, kambi ya kukuna ni kukuna tuu, na kambi ya Kupara, ni kupara tuu.

Kambi ya kukuna na kusifia, wao kazi yao ni kusifia tuu, hata kukifanyika mabaya au maovu kiasi gani, wao watasifu tuu!.

Kambi ya Kupara, ni kuponda na kukosoa tuu, nao kazi yao ni kuponda, kupinga na kukashifu kila kinachofanywa na Rais Samia na serikali yake, hata kiwe kizuri vipi, wao wataponda, watakosoa, watakashifu, wata tukana , watadhalilisha na kubagaza, mfano kazi nzuri ya Filamu ya Royal Tour, kuna watu wanasifu, na kuna watu wanaponda.

Na kundi la tatu ambalo ni dogo, hili lina watu very objective, wao Rais Samia na serikali yake, wakifanya mazuri, watampongeza, na wakifanya mabaya, watamkosoa kwa kutumia constructive criticism, ambao ni ukosoaji unaofanyika kwa nia njema, sio kwa lengo la kubeza, kukashifu, kudhalilisha au kubagaza, bali ni ukosoaji unaofanyika kwa nia njema kwa lengo la kusaidia, kutoa angalizo, kurekebisha na kutoa ushauri wa namna bora zaidi ya kufanya mambo. Ukosoaji wa aina hii, ni ukosoaji mzuri, na ndio unaomsaidia Rais Samia na serikali yake kuliko wale wanaomsifia tuu au wanao mpondea tuu.

Maadam Rais wetu Mama Samia, amekiri kwa kinywa chake kuwa ana ngozi ngumu na kuonyesha kwa dhamira, maneno na matendo, hivyo kwa niaba ya waandishi wenzangu wa habari, tunamuomba sana rais wetu Mama Samia, kama atafutahia kukunwa vizuri, tunamuomba pia atuvumilie tukimpara na tunamuomba asituparure waparaji, kupara pia ni jukumu muhimu la media, kama daktari kutoa dozi chungu na kudunga sindano.

Wasalaam

Paskali
kabla sijaenda mbali wewe kaka mayala tuambiye mparaji at mparulaji?
 
Kuwaogopa waparaji ni kielelezo cha mtu asiependa challenges, anataka kufanya kazi kwa mazoea, na haya mazoea ndio yanaturudisha mikononi mwa wapigaji.
Naunga mkono hoja, maadam Mama ameishasema ana ngozi ngumu, it's good sisi media kujua preference yake ni kukunwa vizuri, ametoa promise ya zawadi ya media hizo na waandishi watakao mkuna vizuri, nao watakuwa vizuri, watapapaswa na kupulizwa ufuu...ufuu. Hivyo sasa kwenye news rooms, ni mashindano ya kukuna vizuri.

Tatizo ninaloliona ni ikitokea muwasho kwenye magaga, hata ukune vizuri vipi, haitasaidia, kwenye magaga ni lazima kusugua gaga, hivyo ni lazima umpare, baada ya kujua ukimpara atakuparura, jee kuna waandishi watathubutu kumpara?.
P
 
Bado sana kuwa katili. Yaan si character yake kabisa
Mkuu Detective J , asante for this
Hili pia lina thread yake
P
 
Wanabodi,
Hii ni makala ya Jumapili hii
View attachment 2216032View attachment 2216034

Kati ya mtu anayekusifu tuu wakati wote na yule anayekusifu ukifanya mazuri, lakini ukikosea anakukosoa na kukushauri, ni yupi atakusaidia zaidi?.

Na kundi la tatu ambalo ni dogo, hili lina watu very objective, wao Rais Samia na serikali yake, wakifanya mazuri, watampongeza, na wakifanya mabaya, watamkosoa kwa kutumia constructive criticism, ambao ni ukosoaji unaofanyika kwa nia njema, sio kwa lengo la kubeza, kukashifu, kudhalilisha au kubagaza, bali ni ukosoaji unaofanyika kwa nia njema kwa lengo la kusaidia, kutoa angalizo, kurekebisha na kutoa ushauri wa namna bora zaidi ya kufanya mambo. Ukosoaji wa aina hii, ni ukosoaji mzuri, na ndio unaomsaidia Rais Samia na serikali yake kuliko wale wanaomsifia tuu au wanao mpondea tuu.

Maadam Rais wetu Mama Samia, amekiri kwa kinywa chake kuwa ana ngozi ngumu na kuonyesha kwa dhamira, maneno na matendo, hivyo tunamuomba sana rais wetu Mama Samia, kama atafurahia kukunwa vizuri, tunamuomba pia atuvumilie tukimpara na tunamuomba asituparure waparaji, kupara pia ni jukumu muhimu la media, kama daktari kutoa dozi chungu na kudunga sindano.

Wasalaam

Paskali
Dr. Bashiru Ali Kakurwa, amempara mtu, sasa watu wamemshukia na kutaka awajibishwe, hivyo wanasubiri kwa hamu aparuliwe!. Tunamuomba Mama, kwa vile alikiri kwa kinywa chake kuwa ana ngozi ngumu, tunamuomba huu ndio wakati wa kuthibitisha ana ngozi ngumu, Dr. Bashiru, kampara, tunamuomba asimparure!.
P
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom