Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 39,280
- 25,361
Ndugu zangu Watanzania,
Ni kishindo, ni gumzo mtaani, ni kila mtu na neno lake, ni kila mtu na uchambuzi wake, ni kila mtu na mtizamo wake. Nchi imesimama, nchi imetetemeka, nchi imepiga saluti kwa Rais Samia, Watanzania wanatetemeka. Lakini Taifa ni Salama na watanzania ni Salama salimini. Ni uteuzi na utenguzi wa aina yake uliofanywa na Rais wetu na Jemedari wetu mpendwa na kipenzi cha watanzania katika namna iliyozima habari zote kuanzia za michezo mpaka siasa, watu wamekesha macho mitandaoni utafikiri kengele au filimbi ya hatari imepigwa katikati ya makazi ya watu.Tangia uteuzi na utenguzi ulipotoka mitandaoni kwote kumetekwa na Rais Samia.
Kwa kweli Rais Samia ameisapraizi Tanzania Katika wakati ambao watanzania walikuwa wapo Bize na habari za Simba na Yanga lakini ghafla habari zikabadilika na kuzisahau kabisa habari hizo na kubakia na habari moja tu kuu ya Rais Samia na uteuzi pamoja na utenguzi. Ni mama wa Aina yake, ni Rais Wa maamuzi, Ni Rais wa mipango, mikakati, mbinu na medani za kivita. Ni Rais jasusi wa kiwango cha DUNIA, Ni komando wa siasa na mipango mikakati ya kisiasa. Ni Rais aliyeiva na kukamilika katika kila idara, ni Rais aliye mbele ya wakati.
Ni Mwenyekiti imara,hodari, shupavu na madhubuti sana.ni kiongozi na nusu,Rais Samia anabakia kuwa Rais Samia asiye na mfano wake.mpime katika mizani ya aina yoyote ile utamkuta anabakia kuwa yeye kama yeye Mwamba usio tikisika,field Marshall kutoka Tanzania, jasiri muongoza njia, simba wa nyika na shujaa wa Afrika. Ni nahodha imara anayeijuwa vyema bahari anayopita na aina ya mawimbi yake.
Taifa lipo katika mikono Salama ya Daktari Samia Suluhu Hasssan likiwa na afya njema na utulivu mkubwa sana. Huwezi ukatamani kuhama Tanzania ya Rais Samia. Uende wapi? Ukatafute nini kisichopatikana katika ardhi ya Rais Samia? Songa mbele Mama yetu na Rais wetu, Taifa lina imani kubwa sana na wewe.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.