Dialysis
JF-Expert Member
- Sep 22, 2021
- 325
- 677
Mama mjamzito ametoka Burundi kwenda Kwa mume wake Kenya Juzi tarehe 25/02/2022. Alivyofika Musoma alikamatwa na uhamiaji sehemu ainayoutwa Kurumuli (Barrier) . Alijitetea kwa uchungu Sana mpaka tulio kuwa kwenye gari lile tulipata huruma.
Mama alijitetea kuwa anaenda Kenya kujifungulia huko kwa mchumba aliyempa ujauzito, asingeweza kujifungulia kwao maana hana msaada na hata hivyo hajapata chakula tangu aanze Safari akitokea Burundi Kupita mpaka wa BURUNDI na NGARA na hata hivyo alijitetea kwenye mpaka huo na akasikilizwa.
Afisa wa uhamiaji Musoma hakutaka kabisa kusikiliza na hakujali hali ya mama yule. Alishikiliwa mpaka akapata labour pain (Uchungu) akakimbizwa Kituo cha AFYA NYASHO .
Mama hakuwa na chochote hata nguo hana, kibaya zaidi alipaswa kufanyiwa upasuaji kwa sababu alipata uchungu pingamizi.
Maafisa uhamiaji waliomleta wakatokomea na hata walipotafutwa hawakuwa na msaada, maana kituo hawakuwa na vifaa vya kama surgical gloves, Dawa za baada na kabla ya upasuaji, drip n.k
Watumishi wa kituo hiki walichanga pesa wakamsaidia. Leo yuko wodini hata chakula anapewa na wagonjwa wenzie. Hana nguo anatumia mashuka ya Kituo.
"Hivi uhamiaji pamoja na Sheria za nchi kwa Hali kama hiyo hawakuwa na chakufanya kuanzia kwenye ukamataji"?