Mwanongwa
Senior Member
- Feb 15, 2023
- 169
- 198
Mwanajamii fuatilia huu mkasa kwa kina.
Kuna binti anaitwa Belith Adamu Mwangoka ambaye kwasasa ni Marehemu na amefariki leo hii majira ya saa kumi jioni katika hospitali ya Rufaa ya Kanda mkoani Mbeya.
FUATILIA KISA CHAKE HAPA HADI UMAUTI ULIPOMFIKA
Marehemu alifika Kituo cha afya Ruanda Mwanjelwa alikuja kufungua kadi ya mimba lakini hali aliyokuja nayo haikuwa nzuri akapewa barua kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa maarufu kama Mkoani.
Akawa hana uwezo wa kulipia gharama za matibabu nikamwambia mimi nitakusaidia hata ukilazwa nitakuletea chakula, mgonjwa akakubali tukachukua gari la wagonjwa tulipofika Mkoani alianza matibabu.
Nikaomba kibali cha kutibiwa kwa sosho walinipa lakini hakikusaidia kitu baada ya hapo nikaambiwa amepewa ya kitanda tu nikaanza kununua dawa wakamuanzishia uchungu akajifungua mtoto Njiti maana miezi ilikuwa haijatimia, lakini hali ilikuwa mbaya sana wakaniambia damu yake ni B Negative tutoe hela inatakiwa chupa mbili nikatoa wakamwongeza baada ya hapo wakamruhusu kutoka hospitali.
Nikawambia mbona hali bado analalamika kifua na tumbo limejaa wakamruhusu hivyohivyo akawa anatembea kwa shida sana tukarudi nyumbani kwangu.
Marehemu Belith Adamu MwangokaNilivyokaa naye siku 3 ya 4 nikarudi naye tena Kituo cha Afya Ruanda Mwanjelwa, nilipofika wakatupa tena barua ilikuwa usiku tukafika mkoani wakaniuliza mmekuja na usafiri gani nikawaambia Bajaj walishangaa maana mgonjwa alikuwa hawezi hata kutembea.
Basi Mkoani wakatupa huduma siku ya tatu wakatupa barua tukaenda Hospitali ya Rufaa ya Kanda kukawa hakuna huduma yoyote, nikiwafuata wananiambia mbona hamjamchukua vipimo wananiambia "kesho", jamani mgonjwa kazidiwa mtundikieni hata maji na tayari nilikuwa nimelipia wakawa wanamwangalia tu mpaka jana nikaenda huyu mgonjwa hali yake ilikuwa mbaya na sukari ilikuwa imeshuka mpaka 1 .
Mgonjwa mwenyewe akaniambia mama hawa wananiua tu ndio wakamtundikia maji moja, naenda jioni nikakuta wamemtoa nikawauliza mbona maji hayajaisha wakasema huoni sasa sasa hivi kafumbua macho.
Hospitali sasa hivi wanangalia mtu mwenye hela, kifo cha Belith wamechangia sana sio Mkoani sio Rufaa walikuwa wanamwambia maneno magumu sana ambayo yalikuwa yanampa wakati mgumu sana.
Hiyo ni simulizi ya mtoa huduma katika Kituo cha Afya cha Ruanda Mwanjelwa.
Marehemu alikuwa ameolewa na mwanaume mmoja ambaye kabila lake ni Msukuma na wakifanikiwa kupata mtoto mmoja ambapo jamaa alivyoona mkewe kabeba tena mimba ya pili akaamua kutoroka na mtoto wake mkubwa.
MTOTO ANAHITAJI MSAADA WA MAZIWA NA MAHITAJI MENGINE
Kuna binti anaitwa Belith Adamu Mwangoka ambaye kwasasa ni Marehemu na amefariki leo hii majira ya saa kumi jioni katika hospitali ya Rufaa ya Kanda mkoani Mbeya.
FUATILIA KISA CHAKE HAPA HADI UMAUTI ULIPOMFIKA
Marehemu alifika Kituo cha afya Ruanda Mwanjelwa alikuja kufungua kadi ya mimba lakini hali aliyokuja nayo haikuwa nzuri akapewa barua kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa maarufu kama Mkoani.
Akawa hana uwezo wa kulipia gharama za matibabu nikamwambia mimi nitakusaidia hata ukilazwa nitakuletea chakula, mgonjwa akakubali tukachukua gari la wagonjwa tulipofika Mkoani alianza matibabu.
Nikaomba kibali cha kutibiwa kwa sosho walinipa lakini hakikusaidia kitu baada ya hapo nikaambiwa amepewa ya kitanda tu nikaanza kununua dawa wakamuanzishia uchungu akajifungua mtoto Njiti maana miezi ilikuwa haijatimia, lakini hali ilikuwa mbaya sana wakaniambia damu yake ni B Negative tutoe hela inatakiwa chupa mbili nikatoa wakamwongeza baada ya hapo wakamruhusu kutoka hospitali.
Nikawambia mbona hali bado analalamika kifua na tumbo limejaa wakamruhusu hivyohivyo akawa anatembea kwa shida sana tukarudi nyumbani kwangu.
Marehemu Belith Adamu Mwangoka