Uhamiaji Musoma, huyu mama kutoka Burundi angefariki damu yake ingewalilia

Huelewi kitu ,Tuliza kichwa Kwanza.

Uhamiaji wa Kwanza ilikuaje wakamuruhusu kuvuka mpaka?(Burundi -Ngara)

2.Umejua chanzo cha uchungu huo?

3.Uhamiaji hawezi kuwa na Sheria zinaweza kusaidia kwa watu kama hao?

4.Passport atatoa wapi hata hela ya chakula nyumbani imeshindikana.
Uhamiaji wanafuata sheria siyo huruma. Ingekuwa huruma, basi nchi yetu ingejaa watu wasiyo na vibali vya kuingia.

Uhamiaji wamepewa kazi na taratibu zake, tuwaache wafanye kazi. Kama hana hela basi abaki huko kwao.

Kwani hana ndugu? Huenda huyu mama alipita njia za panya na kupandia basi njiani.
 
Ukisika uongo ndiyo huu. Nafikiri wewe ni CHADEMA.
Weka siasa pembeni. Issue hapo sio ukwel au uongo, issue happ ni kwann uwamiaji wamemtelekeza huyo mama hospital?

Aya hapo wanasubiria akitoka hospital ndio waje kumkamata tena baada ya kumtelekeza?
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Mimi naona uhamiaji inalaumiwa bure. Je, huyo mama alikuwa na passport ya Africa Mashariki akakataliwa kuendelea na safari? Tukitunga sheria lazima tuzifuate. Hatuwezi kuchagua sheria ipi ifuatwe na ipi isifuatwe. Huyu mama angekuwa na makaratasi yanayotakiwa angeendelea na safari. Kwanza unajuaje ni kweli anaenda Kenya. Unajuaje ni Mrundi. Kwa nini hakuwa na passport? Je huko Kenya angeingiaje bila passport? Si angeisha kurudishwa mpakani. Kama alipata uchungu na kwenda Nyasho Clinic, si ni afadhali kuliko kupatia uchungu ndani ya gari ambapo huduma ya ukunga hakuna?
Hata Kama huyo Mama ni mtuhumiwa wa kutokua na vibali,bado anabaki chini ya uhamiaji kwa hali yoyote ile kuliko mnamkamata alafu mnamtelekeza bila ya msaada wowote ule kutokana na hali yake ya ujauzito!

Kwa hiyo Sasa uhamiaji ndiyo wamesha maliza kazi yao!?
 
Uhamiaji wanafuata sheria siyo huruma. Ingekuwa huruma, basi nchi yetu ingejaa watu wasiyo na vubali vya kuingia. Uhamiaji wamepewa kazi na taratibu zake, tuwaache wafanye kazi. Kama hana hela basi abaki huko kwao. Kwani hana ndugu? Huenda huyu mama alipita njia za panya na kupandia basi njiani.
Sijakataa!Point ni hii kwenye situation kama hii ,Uhamiaji wanachakusaidia?

Walikuwa sahihi Kwa vyovyote vile lakini kwanini hakuna utaratibu wa kimatibabu mhanga wao?

Mbona huwa wanakamata na kuwarudisha kwao Kwa gaharama za ofisi tena wakiwa escort ambaye analipwa per derm ,Iweje wakose fungu la kusaidia?

Read between the line acha mihemuko
 
Uhamiaji wanafuata sheria siyo huruma. Ingekuwa huruma, basi nchi yetu ingejaa watu wasiyo na vibali vya kuingia. Uhamiaji wamepewa kazi na taratibu zake, tuwaache wafanye kazi. Kama hana hela basi abaki huko kwao. Kwani hana ndugu? Huenda huyu mama alipita njia za panya na kupandia basi njiani.
Mkuu ilitakiwa uje na pingu umfunge kwenye kitanda alichokuwa anajifungulia Sasa wewe ukala winga
 
Binadamu tuoaswa kuwa na huruma, hata jamaa alikuwa na makosa bado alipaswa ahudumiwe kulingana na afya aliyonayo. Ueledi katika majeshi yetu haya ni mdogo mno inatakiwa kifanyika reformation ya maana. Kakwambia anaenda Kenya kujifungulia kwa mchumba wake wewe unakomaa utafikiri kaua.

Huwa wakivaa hayo magandwa wanajona ni wamemaliza maisha

Inabidi tushinikiE reformation ya majeshi haya
 
Kiongozi kwasasa dunia ni kama Kijiji na wewe CCM ,hushindwi kupata ukweli kutoka MUSOMA .Mganga mkuu yupo ,Mganga mfawidhi yupo.Unaweza kupata maelezo kutkea huko.Kwanini uniite muongo bila kupata ukweli U au uongo upande wa pili?
Mpuuzi mpuuze.
 
Kuna ofisi moja ya uhamiaji wakiwakamata watu wa namna hiyo (wasio raia) huwapiga sana na kuwanyang'anya fedha zao wanazokuwa wamezipata katika kufanya kazi aidha wakiwa wanarudi nchini kwao au wakiwa wameingia nchini kwetu katika utafutaji.
Sasa ninapofanyia kazi ni karibu na ofisi hiyo Sasa wakiwa wanawapiga wanatoa kilio cha uchungu sana utakuta mtu anapigwa zaidi ya masaa matatu roho yangu huwa inaugua sana kwa kusikia vilio vile.
Baada ya kuwapiga huwapora fedha zao na kuwaachia warudi nchini kwao huku hawana nauli wala hela ya chakula, uhamiaji fuateni taratibu zenu za kazi tafadhari

Kama raia unayo haki ya kuripoti matukio kinyume na utaratibu wa Kazi kwa mamlaka husika
 
Huelewi kitu ,Tuliza kichwa Kwanza.

Uhamiaji wa Kwanza ilikuaje wakamuruhusu kuvuka mpaka?(Burundi -Ngara)

2.Umejua chanzo cha uchungu huo?

3.Uhamiaji hawezi kuwa na Sheria zinaweza kusaidia kwa watu kama hao?

4.Passport atatoa wapi hata hela ya chakula nyumbani imeshindikana.

Hakuna Uhamiaji wa hivyo aruhusu mtu aingia nchini bila kibali huyo alipita njia ya panya.
 
0
Mama mjamzito ametoka Burundi kwenda Kwa mume wake Kenya Juzi tarehe 25/02/2022.Alivyofika Musoma alikamatwa na uhamiaji sehemu ainayoutwa Kurumuli(Barrier) .Alijitetea kwa uchungu Sana mpaka tulio kuwa kwenye gari lile tulipata huruma.

Mama alijitetea kuwa anaenda Kenya kujifungulia huko kwa mchumba aliyempa ujauzito ,asingeweza kujifungulia kwao maana hana msaada na hata hivyo hajapata chakula tangu aanze Safari akitokea Burundi Kupita mpaka wa BURUNDI na NGARA na hata hivyo alijitetea kwenye mpaka huo na akasikilizwa.

Afisa wa uhamiaji Musoma hakutaka kabisa kusikiliza na hakujali hali ya mama yule.Alishikiliwa mpaka akapata labour pain(Uchungu) akakimbizwa Kituo cha AFYA NYASHO .

Mama hakuwa na chochote hata nguo hana ,kibaya zaidi alipaswa kufanyiwa upasuaji kwa sababu alipata uchungu pingamizi.

Maafisa uhamiaji waliomleta wakatokomea na hata walipotafutwa hawakuwa na msaada ,maana kituo hawakuwa na vifaa vya kama surgical gloves,Dawa za baada na kabla ya upasuaji,drip n.k

Watumishi wa kituo hiki walichanga pesa wakamsaidia.Leo yuko wodini hata chakula anapewa na wagonjwa wenzie.Hana nguo anatumia mashuka ya Kituo.

"Hivi uhamiaji pamoja na Sheria za nchi kwa Hali kama hiyo hawakuwa na chakufanya kuanzia kwenye ukamataji"???
Laana hii inatajwa kwenye Isaya 50:11
 
Kuzaliwa Tanzania kama wazazi wako wote si watanzania hakukufanyi kuwa raia wa TANZANIA.

Ni either mmoja wa mzazi wako awe Mtanzania au wote au mmoja wa wazazi wako aliukana utaifa wake wa awali.
 
hakuna uhamiaji wasumbufu kama wa tz ,nimegundua hilo wakuu sijui wanamatatizo gani .sasa huyo mama serious she is not a threat to the nation, kwanin umhangaishe .doesn't make any sense .

very inhumane and barbaric shame on them.
 
Kenya angekufa! Hamna huruma huko.
Na huyo aliyekuwa anamfuata pia angemkataa kweupeee

Kipo kisa cha msichana mmoja mrwanda alizaa na mkenya aliuekuwa anafanya kazi

rwanda basi jamaa aliporejea kwao kenya alimtelekeza yule mrwanda na watoto
 
Back
Top Bottom