Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Makala nyingi za ufugaji wa samaki zinatukumbusha kuwa ni hatari sana kujenga bwawa la samaki ktkt au kando kidogo ya mkondo wa maji, kwa sababu maji yakifurika yatasomba samaki wote, pili maji ya mkondo yanaweza kuja na udongo mwingi na kufunika bwawa, au yakaja na wastes ambazo ni sumu. kumbuka chanzo cha maji huwezi kuki-control wewe, ni maji ya mvua ambayo ni kumba kumba.

Sasa, unaweza kuacha umbali mkubwa kati ya bwawa na mkondo mama, kisha ukachimba mfereji wa kuingiza maji ktk bwawa lako ambao unaweza kufunga na kufungua kadri uonavyo kina cha maji. Vinginevyo uniambie una nguvu kubwa ya kujenga tuta kubwa na lenye uwezo wa kuhimili msukumo wa maji.

Nina jirani yangu mmoja alikuwa na bwawa la zuri la maji ya mvua, mwaka jana umepiga ukame bwawa likakauka, Mchungaji wangu yuko kisere Mkuranga alikinga mkondo kama wewe, samaki pori ni wengi sana.
 
Nashukuru sana mkuu....umenipa tahadhali ya muhimu sana. be blessed!
 
Wakuu natamani kufuga samaki lakini sijui wapi nitapata wajenzi wa bwawa, kuna mtu ana habari zozote kuhusu hili jambo??? msaada tafadhali
 
kama upo DAR,kuna jamaa ,naweza kukupa namba ya simu watakuja kukufanyia kazi.

Kingolwira kuna fish farm unaweza pata ujuzi na mbegu bora pia, mdau hapo juu amedokeza mbegani bagamoyo, pia unaweza kujaribu ila nilidhani bagamoyo wako zaidi ktk salt water fishery
 
kama upo DAR,kuna jamaa ,naweza kukupa namba ya simu watakuja kukufanyia kazi.
Kingolwira kuna fish farm unaweza pata ujuzi na mbegu bora pia,
mdau hapo juu amedokeza mbegani bagamoyo,pia unaweza kujaribu ila nilidhani bagamoyo wako zaidi ktk salt water fishery

Mkuu shukrani zangu za dhati kwa hii info uliyonimegea. mimi nipo musoma nataka kuanzisha ufugaji kijiji kinaitwa Bwai, je hao waungwana wataweza kufika huku, naomba unipe namba zao. Nitawatafuta kingolwira
 
newmzalendo
unaweza kunisaidia makisio ya haraka ya kuanzisha na kuendesha mradi huu kwa bwawa la size ya kati-commercial, salt water?! Asante
 
Last edited by a moderator:
Kama upo Mara, nenda University of Nairobi nchini Kenya, wanayo mabwawa makubwa ya ufugaji wa samaki na wataalamu wapo watakusaidia.

Hata hivyo nimeambatanisha fish farming manual nadhani utapata mwanga jinsi ya kujenga bwawa, kuchagua mbegu bora na kufuga samaki.
 
Naomba nichangie mawili matatu,
Kabla hujaenda huko kwa watalaam, je eneo lako lina maji ya namna gani? Yanatiririka, yatakuwa ya kutuama, au ya kuleta kwa pampu/mfereji, je yamewahi kutokea mafuriko/au huwa yapo, ardhi ni mali ya nani/.Aina ya udongo uliopo ktk eneo lako.

Haya maswali lazima utaulizwa huko kwa watalaam. Nimeweka red kama tahadhali, nina rafiki yangu Isele Mkuranga, alipata mkondo mzuri wa maji bure, akafanya vitu vyake kitalaam,mavuno ya kwanza yakawaamsha waliolala,hawataki jamaa apanue biashara yake,kuuza hawataki, na wao kufuga hawawezi.
 
Kuna eneo la wazi kijjini nilipozaliwa ambalo lipo kwenye bonde, udongo ni wa clay type, wakati wa mvua panajaa maji na katikati ya bonde kwa kweli maji hayakauki hata wakati wa kiangazi (swampy area) bonde limeendelea hadi kuingia ndani ya ziwa victoria lakini maji ya ziwa mara chache sana hufurikia ndani ya bonde, mara ya mwisho ilitokea kwenye miaka ya 70s.

Ukubwa wa hili bonde ni hekari 70 mimi na plan kupata hekari 10 baada ya kuongea na uongozi wa kijiji. Nakushukuru sana kwa tahadhari hasa ya watu wenye fitina wasioweza kufanya chochote.

Ningependa kutumia wataalam wa hapa hapa kwetu badala ya kwenda nje ya nchi.
 
Kama upo Mara, nenda University of Nairobi nchini Kenya, wanayo mabwawa makubwa ya ufugaji wa samaki na wataalamu wapo watakusaidia.

Hata hivyo nimeambatanisha fish farming manual nadhani utapata mwanga jinsi ya kujenga bwawa, kuchagua mbegu bora na kufuga samaki

Ndugu mleta mada, Kenya mbali.

Tuna wataalam wazuri wa uvuvi hapa Tanzania. Hapo Musoma kuna watafiti wa uvuvi TAFIRI wana station yao SOTA-TARIME, na Mwanza pia kuna TAFIRI Mwanza based in Nyegezi. TAFIRI stands for Tanzania Fisheries Research Institute.
 
Kuna eneo la wazi kijjini nilipozaliwa ambalo lipo kwenye bonde, udongo ni wa clay type, wakati wa mvua panajaa maji na katikati ya bonde kwa kweli maji hayakauki hata wakati wa kiangazi (swampy area) bonde limeendelea hadi kuingia ndani ya ziwa victoria lakini maji ya ziwa mara chache sana hufurikia ndani ya bonde, mara ya mwisho ilitokea kwenye miaka ya 70s. Ukubwa wa hili bonde ni hekari 70 mimi na plan kupata hekari 10 baada ya kuongea na uongozi wa kijiji. Nakushukuru sana kwa tahadhari hasa ya watu wenye fitina wasioweza kufanya chochote.
Ningependa kutumia wataalam wa hapa hapa kwetu badala ya kwenda nje ya nchi.

Hizo eka kumi ukipewa zitakuwa karibu na ziwa au nje zaidi? Umesema masika maji ya mvua hujaa, je kiangazi maji utaingiza tokea ziwani au itakuwa static water fish farm?
 
Hizo eka kumi ukipewa zitakuwa karibu na ziwa au nje zaidi? Umesema masika maji ya mvua hujaa, je kiangazi maji
utaingiza tokea ziwani au itakuwa static water fish farm?

Malila nadhani ungem PM mkawasiliana na kumsaidia mkuu kwenye hio project yake. Najua wewe ni mtaalamu wa fani hiyo hivyo fanya kazi yako kwa kumsaidia vizuri na kumpa maelekezo yote juu ya ufugaji samaki wa aina mbali mbali na maeneo mbali mbali.
 
Naomba nichangie mawili matatu,
Kabla hujaenda huko kwa watalaam, je eneo lako lina maji ya namna gani? Yanatiririka, yatakuwa ya kutuama, au ya kuleta kwa pampu/mfereji, je yamewahi kutokea mafuriko/au huwa yapo, ardhi ni mali ya nani/.Aina ya udongo uliopo ktk eneo lako.

Haya maswali lazima utaulizwa huko kwa watalaam. Nimeweka red kama tahadhali, nina rafiki yangu Isele Mkuranga, alipata mkondo mzuri wa maji bure, akafanya vitu vyake kitalaam,mavuno ya kwanza yakawaamsha waliolala,hawataki jamaa apanue biashara yake,kuuza hawataki, na wao kufuga hawawezi.

He he hapo kwenye red baswahili bana ,wana roho za korosho /roho za kwanini ni kama joka la mdimu
 
Malila nadhani ungem PM mkawasiliana na kumsaidia mkuu kwenye hio project yake. Najua wewe ni mtaalamu wa fani hiyo hivyo fanya kazi yako kwa kumsaidia vizuri na kumpa maelekezo yote juu ya ufugaji samaki wa aina mbali mbali na maeneo mbali mbali.

Ni wazo zuri,
Huoni mjadala utamnufaisha mtu mmoja tu,nondo za hadharani ni tamu. Hata hivyo nitawasiliana na mdada mmoja wa huko Musoma ili amsaidie jamaa kiukaribu.
 
Halafu nimeshangaa kule Kyela kuna ziwa Nyasa, kuna mzungu anafanya biashara ya samaki wa mapambo anapata dola za uhakika, juzi nimeangalia Etv ya Afrika Kusini wanasema Lake Nyasa ndio ziwa pekee duniani lenye samaki wa aina mbalimbali zaidi ya aina 500 tofauti, ingekuwa makabila ziwa nyasa lina makabila 500 tofauti ya samaki.na kweli hilo ziwa lina samaki wa mapambo wazuri sana wa rangi mbalimbali, lakini wananchi bado tuko kwenye usingizi wa pono na mzungu yeye anajilia kiulaini sisi tumebaki kulalamika.

Nafikiri wizara inayohusika na uvuvi pia ingesaidia hawa wananchi wa wilaya ya Kyela ziwa Nyasa ni lulu ambayo imekaa tu, naamini wananchi wangewezeshwa kwa kuwa na vyombo vya kisasa vya uvuvi /kiwanda ule umasikini uliotopea unao wazunguka wananchi wa Kyela ungepungua,na isitoshe samaki wa hilo ziwa ni watamu hawana mfano
 
Ni wazo zuri,
Huoni mjadala utamnufaisha mtu mmoja tu,nondo za hadharani ni tamu. Hata hivyo nitawasiliana na mdada mmoja wa huko Musoma ili amsaidie jamaa kiukaribu.

Ni sahihi, ndio maana nikasema kama ni hayo maswali m PM, lakini otherwise weka nondo za ufugaji samaki humu!! maaana huyu anaonekana anataka fuga tilapia, lakini kuna wengine watataka fuga kambale, mwatiko n.k. Pia sio wote wapo kwenye Clay Soil, wengine wapo pwani kwenye Sand soil je nao hawawezi fuga samaki.

Tupe utaalaamu mkuuu.
 
Halafu nimeshangaa kule Kyela kuna ziwa Nyasa,kuna mzungu anafanya biashara ya samaki wa mapambo anapata dola za uhakika,juzi nimeangalia Etv ya Afrika Kusini wanasema Lake Nyasa ndio ziwa pekee duniani lenye samaki wa aina mbalimbali zaidi ya aina 500 tofauti,ingekuwa makabila ziwa nyasa lina makabila 500 tofauti ya samaki.na kweli hilo ziwa lina samaki wa mapambo wazuri sana wa rangi mbalimbali,lakini wananchi bado tuko kwenye usingizi wa pono na mzungu yeye anajilia kiulaini sisi tumebaki kulalamika .Nafikiri wizara inayohusika na uvuvi pia ingesaidia hawa wananchi wa wilaya ya Kyela ziwa Nyasa ni lulu ambayo imekaa tu,naamini wananchi wangewezeshwa kwa kuwa na vyombo vya kisasa vya uvuvi /kiwanda ule umasikini uliotopea unao wazunguka wananchi wa Kyela ungepungua,na isitoshe samaki wa hilo ziwa ni watamu hawana mfano

Kuna aina fulani tokea huko ililetwa Igowole Mfindi, inaitwa black barsa( spelling sijui) ni watamu balaa, na wanazaliana kwa speed ya kufa mtu. Kuna mtalaam mmoja anatokea kule Igowole, nilimuuliza kwa nini hawasambazi mbegu ile, aliniambia, wanaifahamu ile mbegu,pia zipo nyingine morogoro,kwa sasa wanazifanyia utafiti zaidi ili watoke na kitu sahihi, unajua tena kazi za utafiti zinachukua miaka.

Nyasa ni potential, sio kwa samaki tu, mengine tutazungumza siku nyingine.
 
Mimi mwenyewe nataka nitafute ardhi Kyela niwekeze kwaajili ya ufugaji samaki. Ukizingatia kule kuna mito mimgi kama Lufiryo, Kiwira, Songwe, Kiwira n.k. ni very potential area. Mbelele na Mbasa ni watamu sana na wale "furu" (Cichlids wa Lake Nyasa) usiseme!!
 
Back
Top Bottom