Safi safi kamanda na zoezi hilo liendelee na hatutaki kusikia kinyoa hata mmoja amekufa


 
Ndugu yangu popiexo pamoja na dawa zote utakazoona zinafaa kuwapa kuku pia unatakiwa uzingatie lishe bora kwa kuku.na hapa naomba niweke vzr unatakiwa uhakikishe kuwa kuku mgonjwa ametengwa na wazima na anakula chakula cha kutosha pamoja na dawa.ili kujua Kama amekula ni lazima uangalie kifuko chake cha chakula na Kama ukiona hakina chakula basi umlishe Kama mtoto mpaka utakapojiridhisha kuwa ameshiba na umnyweshe dawa kiasi Fulani ili uwe na uhakika kuwa amekunywa dawa.uendelee kumfuatilia kwa ukaribu sana pale utakapoona kuna Shida umsaidie.usiweke tu chakula na dawa halafu uondoke.utakuta mizoga tu bandani. Siku njema
 
Nashukuru sana ndugu yangu.nitakupa mrejesho
 

Mama Timmy niliposoma hiyo green hapo juu, umenigusa sana, kama ni wimbo yaani huu umeweka wimbo niupendao! Asante sana! Wadau mtakaosoma hii post ya Mama Timmy, mjue kwamba hii ndiyo siri kubwa ya mafanikio kwenye kupambana na magonjwa. Mimi huko mwanzo niliwasimulia kuwa nilifunga JELA, Mama Timmy hapa ameongezea kuwa inapaswa kufungua WODI ya wagonjwa na pengine kuwe na ICU kabisa kwa ajili ya wale mahututi wanaohitaji ukaribu! Usione vyaelea vimeundwa jamani! Mama Timmy asantee!
 

Mheshimiwa Guta nimekuelewa, ili kujua tatizo linakoanzia hebu safari hii usitoe mayai tuone! Usisahau kuyachora mayai siku akianza kuatamia ili kuyagundua kirahisi mayai mapya! Kupima mayai husaidia sana kutambua iwapo chanzo cha kutokutotolewa ni nini! Mimi nilikuwa nayapima mayai baada ya siku 7, mayai ambayo hayakurutubishwa yalikuwa yanaonekana kabisa, yanakuwa clear kama lililotagwa siku hiyo hiyo. Pia baada ya wiki mbili niliyapima, mayai mazima yalionekana wazi, na siku moja au mbili kabla ya kutotoa niliyapima. Siku ya kutotolewa mayai yote niliyoyabakisha yalitotolewa yote. Nitaweka picha hapa jukwaani jinsi ya kupima mayai na picha za mayai yaliyopimwa ili tuelewane vizuri. Kwa kuazia ili tujue chanzo cha tatizo hebu safari hii usiwanyang'anye mayai tuone yatatotolewa au la!
 

[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]1. Clear when candled - probably infertile (or very early death) when candled at 8 days.
2. Fertile with red blood vessels - after 8 days.
3. Red or black staining - early death when candled at 8 days.
4. Embryo with red blood 'ring' - early death when candled at 8 days.
5. Dark outline with ill defined detail - late death (10-16 days).
6. Live embryo with bill in air sack - due to hatch in 24-48 hours.
7. Normal development of the air pocket according to number of days.
[/FONT]

Hivyo ndivyo yai likimulikwa na tochi (candling) linavyoonekana katika hatua mbali mbali za ukuaji wake.
 
Wadau nimewawekea Picha za mayai yanavyoonekana yakipimwa, inatumika tochi au mwanga wenye nguvu ya kutosha. Ukizitazama picha hizi kwa umakini kabisa utagundua kwamba yai lilikuwa linawekwa juu ya duara iliyotengenezwa kwa dole gumba na vidole vingine kisha tochi yenye nguvu iliwekwa chini ya yai na kuwashwa! Kuna baadhi ya picha utaona hadi kucha ya kidole gumba cha mkono wa mtu aliyekuwa anapima yai.

Huu ni mfano wa yai lisiloweza kutotolewa!



Yai baada ya masaa 24 baada ya kuatamia.



Siku ya 7




Day 8





Day 9






Day 10





Siku ya 11




Video



Siku ya 12




Siku ya 13








Siku ya 14 Kuna giza sana hakuna unachoweza kuona vizuri zaidi tu ni uwazi uliopo kushoto.





Siku ya 15




Video


Siku ya 16 Unaweza kuona vidole kwenye picha ya pili kulia!



video

Siku ya 17





Siku ya 18 Mayai haya karibu yanatotolewa, kunakuwa na uwazi mkubwa ndani ya yai kama pichani.
 
Jinsi ya kupima mayai (Candling Eggs)


Unaweza kutumia jagi kama hili au Box kisha ndani yake weka bulb kama hii au tochi, lakini epuka bulb za kawaida zinazotoa joto kali.


Kata kipande cha box kisha tengeneza tundu kiasi cha kutosha kufanya yai likae juu yake na lisipitilize!​


Hapa yai limeshakalishwa tayari na kufunika tundu.​


Hapa tochi au bulb imeshawashwa tayari!​
 
Wadau picha za kupima mayai nilizowaonyesha kwenye post namba 272 hapo juu, ndivyo inatakiwa yai lionekane hivyo unapopima siku husika. Hatua za kuzingatia zaidi ni wewe kuweza kutambua yai linavyoonekana siku ya 7 na jinsi linavyooneka siku ya 13/14 pia jinsi linavyopaswa kuonekana siku ya 17/18! Ukiona yai halieleweki eleweki na halifanani na hatua hizo ujue lina matatizo liondoe. Kwa mfano unaweza kukuta yai linaonyesha kama lina mawingu wingu tu ndani, au ukiligeuza na vitu vya ndani vinazunguka tu! Au halifanani au liko tofauti sana na hatua ambayo imefikiwa na mayai mengi. Ukiwa na mashaka na huna uhakika unaweza kuliwekea alama ili lisipototolewa itakupa uzoefu wa kujua yai baya au likitotolewa itakupa uzoefu kutambua yai zima. Ukiwa mfuatiliaji baada ya kupima mayai mara kadhaa unaweza kupata uzoefu na hatimae kuwa hodari wa kutambua yai litakalo totolewa na lile lililoharibika.

Yai ambalo halikurutubishwa ikifika siku ya 7 toka kuku aanze kuatamia huwa halionyeshi tofauti yoyote na yai jipya. Linakuwa clear kabisa nalo lapaswa kuondolewa; mayai kama haya ndiyo nilikuwa ninayakusanya na kuyahifadhi kisha nayatumia kumwekea kuku mwenye dalili za kuatamia yaani 'mayai feki' ili kusubiria siku ya kuwekea mayai ya kuatamia kuku wengi kwa pamoja.
 
Kubota nashukuru sana kwa shule.mimi hupenda zaidi kutumia tiba mbadala kwa kuku wa kienyeji kwani naamini hata zamani hizo ndo tiba zao.nikiona sipati matokeo mazuri ndo nageukia dawa za kizungu.kwa mfano nikiona kuku wangu ameharisha na sijaelewa nini shida nina chukua pilipili kichaa Sita na twanga nachanganya na jivu la kifuu cha nazi kikombe cha chai ktk lita tano za maji halafu kuku muhusika namnywesha na mengine naweka bandani nikiamini watakunywa na Kama alikuwepo mwingine mwenye shida hiyo atapata tiba.baada ya hapo ndo nachunguza ni ugonjwa gani ili nifuate dawa za kizungu sasa.na kwa hili nimepata mafanikio sana
 
Wakuu

@Kubota
@Mama Joe
@guta
@Mama timmy
@LiverpoolFC

Na wengine nawashukuru sana nimejifunza kitu kikubwa. Naachana na kufuga kitimoto nahamia kwenye ufugaji wa kuku wa Kienyeji. Kuna breed ya kuku Botswana wanahimili sana Magonjwa. Nikianza hii kazi nitajitahidi nipate na breed hiyo ya Kenya. Kuna kuku wa Singida na wale wa Usukumani ni wakubwa sana ila shida growth rate yao ni ndogo, nitafata maelekezo yenu ya lishe.
Kubota achana na mambo ya mikaa, utatuletea jangwa jitahidi upande miti pia

Mch Masa
 

mkuu Kubota ahsante sana, nitafanya kwa awamu ijayo nione matokeo yake nitajiandaa kuyapima. kuna kuku ambaye sikutoa mayai yake , nitaangalia imekuaje atakapofikia kutotoa, ila wasi wasi wangu kwa kuku huyu jana ameshinda nje kwa muda mrefu sana sijui ni kwa nini wakati chakula na kila kitu kiko karibu, ametoka saa mbili asubuhi amerudi ndani saa nane! sijui kama atatotoa vizuri. thanks.
 
Last edited by a moderator:
mama timmy ni kweli kwa kuozesha kinyesi ya n'gombe una wale funza na ni wazr sana kwa kuku,mi nlikua naweka mbolea ya kuku ktk ndoo kwa muda hata wiki 3 jioni moja na mwaga ndoo wanatoka wale wadudu hapo kuku inakua full shangwe.jf is the best .gud day
 
du uncle fanya mpango uwatenganishe una ambukiza sana huo ugonjwa ,nenda kwa wale wauza dawa uwaelezee hali halisi ya kuku wako kabla hujapata hasara.
 
Nashukuru sana ndugu yangu.
 

Aa mchungaji, fuga vyote kama eneo linakuruhusu, kuku hawana shida sana we ni kiasi cha kuangalia chakula bora cha kuku, na kuwa mwepesi wa kubaini magonjwa, hu hitaji muda mwingi sana kushindwa kufanya shughuli zingine.
 
Aa mchungaji, fuga vyote kama eneo linakuruhusu, kuku hawana shida sana we ni kiasi cha kuangalia chakula bora cha kuku, na kuwa mwepesi wa kubaini magonjwa, hu hitaji muda mwingi sana kushindwa kufanya shughuli zingine.

Mchungaji Masanilo Nashukuru kwa ushauri kuepuka jangwa nitajidhatiti kupanda miti na hata ikibidi naanzisha msitu wangu. Kuhusu kufuga vyote nguruwe na kuku hawa wa kienyeji inabidi uwe mwangalifu sana jinsi ya kutengeneza banda la nguruwe maana kuku huingia kwenye mabanda ya nguruwe kuokoteza mabaki ya pumba sasa nguruwe ni fundi sana wa kuwadaka kuku! Hadi nilipokuja kukuta manyoya bandani ndiyo niligundua kuwa nguruwe ni balaa!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…