Hata Mie nimeanza kufuga kwa kuku kuchi 2 na dume lake 1 sasa Nina vifaranga vya kuku kuchi 13 vya mwezi 1 matarajio yangu hadi mwezi wa sita mtakua nao wengi kwa kuuza biashara
Mkuu vipi unaendelea je na ufugaji wa kuchi, nikihitaji mayai kwa ajili ya kutotolesha nitapata?
 
Mkuu tupe update nataka nami nijikite huko
 
Hesabu yako sijaielewa!,hiyo million 3 umeipataje,hiyo laki moja ni ndogo sana ila mwanzoni itamudu lkn kadiri kuku wanavyo zidi kuongezeka garama za uendeshaji nazo zinaongezeka na usizani ni rahisi kama uliyo andindika kuku wanakula mno hasa wakiwa wengi (competition of food) na gharama kubwa ya uendeshaji wa mradi wa kuku ni chakula.Kwaushauri hebu achana na matarajio makubwa makubwa badae utakuja kuwa mfugaji makubwa sana kama ukiacha kufuga kwa hisia
 
Umeongea point Sana .. mkuu kuku wana lipa lakin si kwa mahesabu ya uyo bwana me na fuga huu mwaka watano wakienyeji pure Ila sijawi waza Ayo mahesabu
 
Kuna binadamu hawana huruma kabisaa mwaka 2017 mwisho december nilinunua kuku kutoka mbeya jumla majike na majogoo kama 70 ila mpaka hivi hela hawajaongeza kabisaa zaidi naona wamebakia 30 kila siku mfanyakazi anasema wanaumwa na kufaaaaa
 
Ni mradi mzuri kama mfugaji ukiweza kukabiliana na magonjwa lakini pia uweze kumudu gharama za chakula. Chakula jifunze kutengeneza mwenyewe ambacho kitakuwa na virutubisho vyote. Tumia malighafi zinazopatikana ktk mazingira yako kutengeneza chakula.
 
Its very simple to do business calculation on imagination...karibu watu wote duniani wanatembea na miradi kichwani - shida inakuja kuuhamisha huo mradi toka Logical way of thinking into reality hapo ndipo kwenye mtego mkuu - na hapo ndipo wanapopatikana Matajiri na Maskini ambao wametajwa hata katika vitabu vitakatifu.

Ukifanikiwa kuuhamishia mradi wako toka kichwani into reality na ukafanya kazi basi wewe ni TAJIRI.

Nakutakia mafanikio mema, kujaribu si ujinga........ kumbuka kuwachanja hao kuku wako maana wanaweza kufa wote in just 24 hrs...
 
Nyongeza kwa wachangiaji wengine walotangulia ....
Jifunze kustawisha Azolla, mbegu zipo kilo ni sh/. 15,000/= Pia vitabu vya mafunzo ya kuzalisha fodder vipo soft copy Tsh. 10,000/=
 
Toka January Hadi Leo miezi imepita leta mrejesho ,nipo tayari kukupa ushauri utakao kusaidia Ila tupe changamoto ulizokutana nazo
 
Safi sana, mimi nimeanza kufuga kuku 6, jogoo mmoja mitetea 5, sasa hivi wote wanataga nnatarajia mda siyo mrefu nitakuwa na vifaranga siyo chini ya 60, ambao nitawachukua kutoka kwa mama yao, baada ya hapo kazi yangu itakuwa kula mayai na nyama wakipungua nazalisha wengine, sifanyi kwa ajili ya biashara, ila nimegundua kufuga wanyama/ndege inakufanya uwe active sana, furaha na stress vyote vyako, kuna kuku mmoja namkubali sana sana sijui kama nitakuja kumla kwa kweli, actually hawa kuku wote nilioanza nao sitawala
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…