Ufisadi wa Kifo Vipimo vya UKIMWI

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,098
ili kupata uhakika. Watu wengi wameharibiwa maisha yao kwa majibu ambayo yalikuwa si ya kweli
~+~+~+~+~+~+~+~+~+~+~+~+~+~+~+~+~+~+~+~+~+~+~+~+~+~+

Italian man returns from woodland exile after HIV 'mistake'

Tom Kington in Rome
Wednesday August 8, 2007
The Guardian

Alberto Zabbialini dropped into an internet cafe on Sunday and did what millions do at their computers every day, idly keying his name into a search engine. But the 28-year-old mechanic had more reason than most to be curious after he had fled his home three months earlier in a suicidal mood to carve out a hermit's life on berries and river water in the Ligurian woods, driven by the belief he had contracted HIV.

What he found online was shocking: reams of articles about him pointing out medical tests he had taken actually showed he was in perfect health, desperate appeals from his family and from celebrities to come home, and news of a police dragnet which gripped Italy's attention.
"Is this true I'm not ill? Don't lie to me," were his first words when he rang his mother Francesca from a call box.

"I said to him 10 times, 'I swear, you're fine, just come home,'" she told journalists and camera crews crowding her doorstep on Monday as she hugged tightly the pale, thin son she had almost given up for dead.

Shorn of the long beard he was sporting when he arrived back in the hamlet of Castrezzone di Muscoline near Lake Garda, Alberto was tight-lipped as to whether fear, shame or embarrassment had driven him into the hills.

What is known is that he underwent a series of medical tests after feeling unwell on his return from a foreign holiday earlier this year. Whether he misread the results or was initially misdiagnosed is unclear, but he panicked and took off on his moped on May 10, stopping only to phone his parents to tell them to "take care" of his girlfriend, Simona.

With €1,000 (£680) in his pocket and his mobile phone switched off, Alberto abandoned his moped 140 miles from home in Vado Ligure, where it was later found by police, before marching into the sparsely inhabited wooded slopes running down to the Mediterranean west of Genoa.

"For the first month I ate what I could find, figs and cherries," said Alberto, adding that he had drunk stream water and slept on a bed of leaves and branches. At one point he heard his uncle roaming the woods and yelling through a megaphone that the tests had put him in the clear. "But it was the first days and I thought he was lying so I hid myself. I wanted to end it."

By this time a national police manhunt was under way and Gianluigi Buffon, goalkeeper at Alberto's favourite football team Juventus had published a personal appeal in the pages of sports daily La Gazzetta dello Sport for Alberto to come home. Alberto's doctor also published his mobile phone number, urging Alberto to call in. "It was just a mundane infection," said the doctor.

"The worst day was when I was called to identify a corpse found in those woods," said his father, Angelo. An autopsy later showed the body to be that of a missing pensioner.

Asked why he was so pale after his outdoor sojourn, Alberto said he had stayed under cover of the woods, venturing out only when he discovered a path leading to a motorway service station where he purchased sandwiches without once being recognised.

Three months on and 10kg lighter, Alberto's curiosity to know what the world was saying about him won out. "I came down from my wood to an internet point, put in my name and clicked to find a stream of articles which said I was not ill. At 8pm I called home to find out the truth."

Cast by the Italian media as an all-Italian family boy plagued by angst, Alberto lived up to his role on Monday, smiling as his mother kissed him after a celebratory roast chicken dinner at the family house he still lives in.

"When you leave you turn your back, and that is easy," said his father, who employs Alberto in a local car workshop. "But when you return you need to show your face, and that is much more difficult. Alberto managed this and that makes me proud of him," he said. "Us Zabbialinis are capable of eating a lion, but in the face of illness ..."
 
Ufisadi wa kifo

na Asha Bani na Julieth Mkireri

BAADA ya taifa kutikiswa na ufisadi wa kutisha wa uporaji fedha za umma uliosababisha kuyumba kwa uchumi, mtiririko wa matukio hayo umegeuka, na sasa umeanza kutishia uhai wa Watanzania.

Taarifa za karibuni zilizothibitishwa na viongozi wa juu serikalini zinasema kuwa mamilioni ya Watanzania waliopima maambukizi ya virusi vya ukimwi majibu yao si sahihi kwa sababu vifaa vilivyotumika kuwapima havikuwa na ubora unastahili.

Wakati serikali ikitangaza hatari hiyo, taarifa nyingine kutoka ndani ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASCO) zimeeleza kuwa zaidi ya Watanzania milioni 15 wanaotumia maji yanayosambazwa kutoka mtambo wa Ruvu Chini wako hatarini kupoteza maisha baada ya baadhi ya wafanyakazi wa mtambo huo kutangaza azma yao ya kuweka sumu katika mitambo inayosambaza maji kwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Kitisho hiki, pia kimethibitishwa na Menejimenti ya DAWASCO iliyokiri kupokea barua ya wafanyakazi wa mtambo huo, inayomtaka Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof. Mark Mwandosya kuwarudisha kazini katika kipindi cha wiki moja wenzao waliofukuzwa kwa tuhuma za kukiuka taratibu za kazi, kabla hawajatia sumu kwenye mitambo inayosambaza maji hayo.

Matukio haya mawili makubwa yalitokea mwishoni mwa wiki hii.

Tukio la kwanza, serikali imekiri kuwa mashine za kupima maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) zinazofahamika kitaalamu kwa majina ya ‘Capillus na Cyflow CD4’ hazina ubora unaotakikana, hivyo waliopima majibu yao si sahihi.

Kauli hiyo ya serikali ilitolewa jana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Prof. David Mwakyusa kwa waandishi wa habari ikiwa ni siku chache baada ya kupokea majibu ya tume iliyochunguza vifaa hivyo.

Prof. Mwakyusa alilazimika kuunda tume hiyo baada ya mzabuni aliyeleta vifaa hivyo kuituhumu wizara yake kuwa ilipokea rushwa ili vifaa hivyo vionekane batili na zabuni hiyo itolewe kwa mtu mwingine.

Akitoa taarifa ya uchunguzi uliofanywa na Chuo Kikuu cha Sayansi za Afya Muhimbili (MUHAS), alisema umebaini kuwa vifaa hivyo havina ubora, hivyo kuwapo kwa uwezekano mkubwa kwa wagonjwa waliopimwa ukimwi na VVU kwa kutumia vifaa hivyo au waliopima CD4, kupewa majibu yasiyo sahihi.

Prof. Mwakyusa alisema baada ya kupokea taarifa ya uchunguzi uliofanywa na MUHAS aliamua kuunda tume ya kuchunguza tuhuma hizo kwa uzito wake kuwa kama ni za kweli, basi maisha ya maelfu ya Watanzania wanaougua ugonjwa huo yalikuwa hatarini.

Aliwataja wajumbe wa tume hiyo kuwa ni Profesa Philip Hiza, Mganga Mkuu wa Serikali mstaafu, Profesa Raphael Lema, Consultant Pathologist mstaafu, Dk. Juma Madati, Mkemia Mkuu wa Serikali mstaafu.

Alisema tume aliyoiunda ilianza kazi kwa kuzifanyia kazi tuhuma zilizotolewa na mzabuni wa vifaa hivyo, Roland Gohde, aliyeingiza vifaa hivyo nchini kwa kushirikiana na mtoto wake, Wolfang Gohde pamoja na Mtanzania mmoja aliyetajwa kwa jina la Dk. Mbawala mkazi wa Dar es Salaam.

Prof Mwakyusa alisema taarifa ya tume hiyo ilionyesha kuwa, vifaa hivyo havikuwa feki bali viliharibika baada ya kuwekwa sehemu yenye joto kwa muda mrefu.

Aidha, tume hiyo pia ilibaini kuwa historia ya Prof. Gohde ilionyesha kuwa ni mstaafu wa Chuo Kikuu cha Muster cha nchini Ujerumani ni mshauri wa Kampuni ya Partec inayotengeneza kifaa cha Cyflow na pia ndiye aliyeleta vifaa hivyo hapa nchini wakati akiwa hana utaalamu wa kutengeza kifaa hicho.

Kwamba historia hiyo ilionyesha wazi kuwa Prof. Gohde hakuwa na sifa ya kuwa mshauri wa kampuni hiyo kwa sababu si mtaalamu wa vifaa hivyo, hivyo hakuwa na sifa ya kuvileta.

Alisema ripoti ya tume hiyo ilibainisha kuwa, tuhuma ilizotupiwa wizara za kucheleweshwa kwa makusudi kwa vifaa hivyo hadi vikaharibika si za kweli kwa sababu viliagizwa nchini kwa jina la Katibu Mkuu aliyepita (hakumtaja jina) na si wizara.

“Hata hivyo, tume ilichunguza na kuona kuwa kuna ukweli ndani yake, vifaa hivyo vilicheleweshwa mara mbili, lakini ni kutokana na kuingizwa nchini kwa jina la mtu binafsi na si kiofisi ndiyo vilicheleweshwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa zaidi ya miezi miwili jambo lililosababisha viharibike.

“Kutokana na hilo, taarifa za ujio wa vifaa hivyo zilichelewa kutolewa tangu vilipoingia uwanja wa ndege, kwenda wizarani hadi kufika katika bohari la serikali la kuhifadhi dawa (MSD) ambalo ndiyo ‘Clearing agent’ wa wizara,” alisema Prof Mwakyusa.

Alisema ucheleweshwaji wa pili ulichukua miezi saba baada ya mashine kufikishwa MUHAS ambako zilikaa bila kuchunguzwa kwa kukosa vitendanishi hadi vilipowasilishwa vikiwa vimechelewa.

Alikanusha uzembe huo kufanywa na wataalamu wa MUHAS na kueleza kuwa lilikuwa jukumu la wasambazaji wa vifaa na Bodi ya Maabara ya Umma (PHLB) iliyokuwa na jukumu la kuleta vitendanishi.

“Hata hivyo, baada ya vitendanishi kuwasili, iligundulika kwamba vifaa hivyo vilikuwa na kasoro ambayo ilibidi Mhandisi wa Partec aitwe kutoka Nairobi Kenya kuja kuvirekebisha, jambo lililochangia ucheleweshwaji kuvichunguza,” aliendelea kufafanua Prof Mwakyusa.

Sababu nyingine ya kuchelewesha kufanyika kwa utafiti wa vifaa hivyo iliyotolewa na Prof. Mwakyusa ni uchunguzi wake kuchukua wiki sita kukamilika na kwamba mwakilishi wa Kampuni ya Partec, Dk. Mbawala, aliwaudhi wanasayansi kwa sababu ya kutojiamini hali iliyomfanya kwenda kila wakati katika maabara vilikohifadhiwa vifaa hivyo.

“Kwenda kwenda kila mara MUHAS wakati uchunguzi ukiendelea, jambo hilo liliwaudhi wanasayansi hao kwa kuwa si utaratibu wala kanuni zinazozingatiwa katika kufanya uchunguzi huo,” alisema Prof Mwakyusa.

Aliendelea kueleza kuwa, tume iligundua kuwa kulikuwa na vitendanishi vya aina tatu ambavyo ni Calibration beads vilivyoisha muda wake tangu Oktoba mwaka 2005, Dilution Buffer vilivyoisha muda tangu Desemba 2005 na Easy Count CD4PE vilivyoisha muda wake tangu Februari 2006.

Kwamba uchunguzi kwa kutumia vitendanishi ulikamilika Septemba 30 mwaka 2005 jambo linaloonyesha kuwa vilikuwa bado ndani ya muda ila vifaa havikuwa salama.

Alisema matokeo ya tume hiyo pia yalibaini udhaifu kwa Patrec ambao ni wazalishaji wa vifaa hivyo kuwa hawakuwa makini katika kufuatilia usafirishaji na utunzaji wake kutoka vilipotumwa hadi kuwasili maabara ya uchunguzi.

Alieleza wasiwasi na mshangao kwa nchi zinazotengeneza vifaa hivyo kupenda kuingiza vifaa hivyo kwa wingi katika nchi zinazoendelea.

“Mimi nashangaa kwa nini vipimo hivi viwepo katika nchi zinazoendelea kwa wingi - Nigeria, Ghana, Uganda na Sudan na si katika nchi zilizoendelea za bara la Ulaya. Hapa kuna walakini kidogo,” alisema.

Alisema kutokana na shaka iliyojionyesha kuhusu vifaa hivyo, serikali imepiga marufuku uingizwaji wake hapa nchini na kuongeza kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wanaoviingiza kinyume cha taratibu.

Wakati hali ikiwa hivyo katika Wizara ya Afya, huko Dawasco nako, tishio hilo la wafanyakazi lililofikishwa mezani kwa Waziri Mwandosya, linakuja wakati taifa likipita katika kipindi kigumu cha kukabiliana na kashfa mbili kubwa zilizogharimu uchumi wa taifa, Richmond na EPA.

Wafanyakazi walioandika barua pasipo kuweka majina yao wanasema kufukuzwa kwa wenzao hao hakukuwa kwa utaratibu maalumu, bali kulitokana na mipango iliyopangwa na Mkurugenzi Mkuu wa DAWASCO makao makuu, akishirikiana na Meneja wa Mtambo huo.

Katika barua hiyo, walieleza kuwa, iwapo waziri hataizingatia atashuhudia matokeo ya kuwapoteza Watanzania wengi wasio na hatia kutokana na utendaji mbovu wa meneja wa mtambo pamoja na mkurugenzi wake.

Katika barua hiyo, wafanyakazi hao walidai kuwa, baada ya wenzao kufukuzwa wamekuwa wakifuatilia jambo hilo na kubaini kuwa ni njama za Mkurugenzi Mkuu wa DAWASCO za kutaka kuwaondoa wafanyakazi wote wa zamani wenye ajira ya kudumu.

Kwa mujibu wa wafanyakazi hao, habari walizonazo zinaeleza kuwa mameneja waliopewa kazi hiyo wameahidiwa kulipwa zawadi ya shilingi milioni tano kama akiikamilisha kazi hiyo.

“Kilichobaki ni kulipiza kisasi, tunajua ndugu zetu watakufa, lakini kwa hili heri lawama kuliko fedheha. Vyombo vya habari vitaripoti ni lazima tuweke sumu, hatuna mzaha vinginevyo wenzetu warudishwe kazini,” inasomeka sehemu ya barua hiyo.

Akizungumza na maofisa kutoka DAWASCO makao makuu waliokuwa wameambatana na makachero kadhaa wa polisi, Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini, Joseph Bamwezaki alisema alikuwa hana taarifa juu ya barua hiyo.

Naye Meneja wa DAWASCO makao makuu, Elias Kasitila alisema kuwa, mkurugenzi wake amepata barua hiyo juzi na kwamba siku hiyo hiyo walimuomba ofisa upelelezi kwenda naye eneo la tukio ili kuona ni jinsi gani wataimarisha ulinzi kuokoa maisha ya Watanzania.

Meneja uhusiano wa DAWASCO, Badra Masoud alieleza kuwa, taarifa hizo zimekwishaufikia uongozi wa juu wa mamlaka hiyo na umekwishawasiliana na vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kuhakikisha jambo hilo halitokei.

“Inatisha, lakini inasikitisha, wameamua kuua hata ndugu zao, wamefukuzwa baada ya kubainika wana makosa makubwa. Wanakiuka taratibu za kazi, wanaiibia DAWASCO maji. Sisi tumeripoti kwa vyombo vya ulinzi na usalama, kila kitu kiko chini ya utaratibu, wateja wetu wasiwe na wasiwasi,” alisema Masood.

Source: Tanzania Daima 16/03/2008
 
Kutoka Tanzania Daima~Sauti ya Watu

Maoni ya Wasomaji

Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 13 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Mimi nashindwa kuielewa hii inayoitwa serikali ya tanzania. Unajua kuna kipindi mtu unawaza na unaona ni bora kufanya mapinduzi ya nchi, kila siku amani amani kitu gani amani kama watu wanakufa bila kujaliwa.
tatizo la serikali hii kila mtu anataka kuchukuwa chake mapema hivi inaingia akilini kweli waziri kuwaita waandishi wa habari bila aibu kana kwamba anatangaza ukombozi anasema vifaa vilivyotumika kupimia ukimwi si sahihi na je baada ya kutamka hivyo mhusika aliyeuza vifaa hivyo kwa serikali amekamatwa na kushtakiwa tuache longolongo katika vitu vinavyohusu maisha ya watu.
Kikwete ana kazi ngumu sana namuonea huruma sana kwa kuwa amezungukwa na mafisadi kila upande kama utaandu wa buibui naye hajui hata afanyeje?
Bora ningezaliwa Iraq ama Pakistan kuliko tanzania ambapo tunauwawa na viongozi wetu kwa ajili ya manufaa yao.

na mzalendo- Ngara, Tanzania, - 16.03.08 @ 12:09 | #2434

hii tena kali!!yani kila kukicha kunaibuka ufisadi mwingine,ndo maana ip akasema mafisadi ni kama magaidi wametambaa nchi nzima,yani sasa si amini mfanyakazi yoyote wa serikali,mpaka huu mwaka uishe mbona tutajua mengi,kikwete songa mbele watataja mpaka mwisho,kweli fari moja huanzisha nyengine

na mzalendo - 16.03.08 @ 12:26 | #2438

Haitoshi kutuambia kwamba vifaa vilivyotumika vilikua havina ubora.Tuambieni watu wangapi wamepewa damu kwa kutumia vifaa hivyo,na muwaite watu wote waliopewa damu muwapime tena acheni mashairi yenu ,fanyeni kazi kisayansi

na abdulla, uk, - 16.03.08 @ 13:25 | #2449

MAFISADI WA SAKATA LA EPA WANARUDISHA FEDHA WALIZOWATAPELI WATANZANIA-WANAPETA BAADA YA KUPATA MITAJI NA WANARUDISHA MKOPO WA UTAPELI BILA RIBA!!,SASA HAWA WA WIZARA YA AFYA MTAWASHAURI WAFANYE NINI?.Kama kawaida wameshakurupuka na kuunda tume ya wazee waliotufikisha ktk hali hii tuliyo nayo ya ufisadi,ubinafsi nk,halafu mnatudanganya mna nia njema!.
Hata waziri mwenyewe tuna shaka nawe sana katika utendaji wako kwani wengi wanakufahamu toka ukiwa Muhimbili na hata kabla hujawa Prof.-JASIRI HAACHI ASILI,SIE TUNAWATAZAMA-IKO SIKU UKWELI UTADHIHIRIKA!.
Na hao watishia kuweka sumu nao ni kundi hilohilo la MAFISADI WADOGOWADOGO!,KAMA MTU NI SAFI HUWEZI HATA KUFIKIRIA KUTISHIA KUWEKA SUMU.
Nashauri wasifikiriwe hata kurudishwa kazini na kama sumu na waiweke!,pia inabidi SERIKALI IINGIE DAWASCO KWA NGUVU KUBWA NA MTU MWENYE MSIMAMO NA UFUATILIAJI KAMA MH.MAGUFULI AWASHUGHULIKIE HAWA DAWASCO KWANI NI KERO KUBWA SANA.

na Juma Masumbwi, Mwenge-DSM, - 16.03.08 @ 13:39 | #2451

Hawa DAWASCO wasituletee mchezo!! Ingawa hao viongozi wao wamejikosha kwenda polisi, Mwandosya tunahitaji kuona busara zako ili tupate uhakika kati ya uongozi wa DAWASCO na hao wafanyakazi ni nani mwenye haki. Wananchi tunataka kujua kama hao wafanyakazi walijiunganishia maji kweli na kama ni kweli je utaratibu wa kutoa adhabu ulifuatwa na je adhabu waliyopewa inaendana na kosa walilofanya? Pia tufaham kama hao viongozi wa DAWASCO kweli walihongwa ili watimize uovu huo uliodaiwa na wafanyakazi wao au la?

na emmanuel, songea, - 16.03.08 @ 13:56 | #2452

MIMI NASOMA ITALY NA ZAIDI YA MARA TATU NILISHA WAHI KAA NA MARAFIKI ZANGU PAMOJA NA MAPROFFESSOR TOFAUTI KATIKA MAZUNGUMZO WA KIITALIANO NA KIRUSIA NA WENGI WAO WALINIAMBIA KWAMBA SERIKALI ZA KIAFRICA HAZINA ''AKILI'' WAKIZIMWAGIA SIFA SERIKALI ZA ZIMBABWE,LIBYA NA SOUTH AFRICA,NILIKATISHA MAZUNGUMZO HAYO KWA KUONA NIDHARAU HIYO, ILA BAADA YA KUKAA WEEK MOJA NAKUFIKIRI WHY THEY SAYED THAT NILIENDA MUULIZA PROF MMOJA AND HE TOLD ME,,, WE DONT HAVE OUR PERSONNAL DECISION'''' HADI TUAMBIWE NA NCHI ZA MAGHARIBI CHA KUFANYA,, SASA KAMA MNA UWEZO WA KUZIKAGUA HIZO MASHINE NA KUGUNDUA NI MBOVU NA HAZINA VIWANGO,,,,,HIVYO MNAO UWEZO MKUBWA KABISA WA KUTENGENEZA ZA KWENU WENYEWE ZENYE VIWANGO VINAVYOKIDHI MAZINGIRA YETU,,,,, WHY? MWAAGIZA TOKA NJE??? NYIE MWONENI TU MUGABE FALA LAKINI BAADA YA MIAKA KADHAA MTAWAONA WAZIMBABWE WATAVYO USHIKA UCHUMI WAO NA KUSIMAMA KAMA WAO NA KUFANYA WANACHOKITAKA KWA MANUFAA YAO,,,,,, HIVI WEWE WAZIRI MWAKUSYA UNATEGEMEA MZUNGU ATAKUPA MASHINE BORA ILI USIFE THEN MADINI NA RASLIMALI ZAKO ATAZIIBAJE BASI??? IF U REALLY GOT UA BRAINS U FAKE CCM LEADERS USE IT!!!!!

na PEMBE, Italy, - 16.03.08 @ 14:21 | #2453

Hii ndo bongo yenye watawala wasio na bongo!nani shamba la mwendawazimu unaloweza kuvuna hata kama hukupanda, mradi tu unanafasi ya kufanya "procurement."
Hapa ina maana wapo watu waliopimwa nakuambiwa kwamba hawana ukimwi kumbe laa. Pili,wapo walioongezewa damu kwa upotovu wa vipimo 'fake'na kujikuta wameongezwa damu yenye vijiini vya ukimwi.Lakini pia wako waliopimwa na kuendelea kujamiiana na wenzi wao bila ya kinga kwavile vipimo vilionyesha ni 'negative.'
Tunaitaka serikali kupitia wizara husika itoe fidia kwa wote walioathiriwa na vipimo hivi kwa kupewa majibu 'fake'na kwavile viongozi wa nchi hii ni vigumu kujiuzulu tunaomba iundwe kamati ya Bunge kuchunguza sakata hili ili jamaa hawa waweze kuwajibishwa na kamati hiyo.
Sakata hili lilishawahi kuripotiwa sana na gazeti la Rai ila kwavile watanzania ni wagumu kuelewa nani wepesi wa kuashau ndo maana sasa tumefikishwa hapa na wakuu wa wizara, na kwakuwa kila kitu nchi hii ni siasa viongozi wetu walibisha na sasa sisi tulowaweka madarakani tunaathirika.Dawa pekee ni 2010.


na Brown. M,, Nzega, Tanzania, - 16.03.08 @ 15:46 | #2457

KAKA PEMBE ITALY NAKUUNGA MKONO,ILI TAMKO LINATISHA, NASHINDWA KUELEWA HATA HUYO WAZIRI KWA NINI AMEAMUA KULIWEKA WAZI, JE WALIOAMBIWA WANA UKIMWI???HAWANA?? WALIOMBIWA HAWANA WANAO?? JAMANI MUWE WAANGALIFU NA TAARIFA ZINGINE, HII LAWAMA NI PAMOJA NA GAZETI HILI LA TANZANIA DAIMA, MNAUA WATU KWA HILI TANGAZO, MAANA HATA HABARI YENYEWE INA MASWALI MENGI SANA,AMBAYO MLIPASWA KUULIZA??JE NINI KINAFANYIKA SASA??WATU WASIPIME TENA?? I AM TOTALLY DEVALUING YOU GUYS.

HILO SIO LA KULICHEKEA NENDENI TENA KAMUULIZENI HUYO WAZIRI MPUMBAVU.JE WATU SASA WASIPIME?? NA JE NI WATANZANIA WOTE?? MNALETA UTANI NA UKIMWI........SERIKALI,MWAKYUSA ,TANZANIA DAIMA WOTE MNAMAKOSA.HII TAARIFA SIO YA KICHUNGUZI WALA HAIJAPIMWA KUWA ITOLEWE AU LA MMEFANYA HIVYO HILI WATU WANUNUE MAGAZETI, WALA HAIJALENGA KUMSAIDIA RAIA ANAYEIPATA HABARI HII NA ALIYEATHIRIKA.

PEMBE KWELI KAKA, HII MIJITU INAYOTAKA TUIYONE SMART SANA, NDIYO MIJINGA SANA.

na Imani Martini, USA, - 16.03.08 @ 16:08 | #2462

KWELI HALI SIO NZURI KAMA TUMEFIKA HAPA AFYA ZETU WA KUZILINDA NI NANI KAMA SIO SERIKALI HAYA YA MUHIMBILI SI TOFAUTI NA YA VETA ( MAMLAKA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI ) JAKAYA TUME INATAKIWA LAKINI ISIWE YA WAZEE TUTAONA MENGI NA KUOKOA PESA ZA WANANCHI

na john lema - 16.03.08 @ 17:51 | #2476

Hivi nchi hii inakwenda wapi, kila kona ni mafisadi wamejaa.Serikarini,mahospitalini,mashuleni nk.Hii imekuwa ni hatari kubwa kama vifaa vya kupimia HIV ni feki. hebu tujiulize ni wagonjwa wangapi wameongezewa damu, na kama vifaa havifai, tunauhakika gani na usalama wa damu hiyo. Ama kweli kikulacho ki nguoni Mwako.
Kameta USA.

na Kameta, Marekani, - 16.03.08 @ 19:08 | #2485

Wafanyakazi wa DAWASCO siyo watu waungwana kama ilivyo menejiment ya DAWASCO.
Kuwauwa watanzania mamilioni kwa maslahi ya mshahara ambao unatokana na hao mamilioni wanaotarajiwa kuuawa ni uhuni wa kigaidi.
Dawasco kutumia hoja dhaifu kuwafukuza wafanyakazi wake ni aina ya uhuni wa waajiri wababe ambao hawana chembe ya utu.
Je serikali ilimuasign DAWASCO kuwa msimamizi wa maji dar kwa uzoefu upi?? Ninaamini kuwa ili at;east upate tenda kubwa serikalini basi uwe na business inayoexist three years in bonus sasa hawa dawasco wametoka wapi na walisajiliwa lini??

Serikali isipuuzie vitisho vya wwafanyakazi maana inaonesha kuna moto mkali chinichini unawaka.

na Msanii, Afrika, - 16.03.08 @ 19:39 | #2487

nafikiri wakati sasa umefikia wakati wa kuisafisha wizara ya afya,mana juzi tu hapa waziri anabishana na watu wake wa chini,waziri anasema vifaa vya muhimbili havina ubora na vimechakaa kesho yake watu wa muhimbili wanasema hayo mambo ya zabuni yalifanyika wizarani,sasa hapa kuna mkono wa rushwa na waziri anajua au km hajui kuna haja ya kumtoa,hivi wabongo wenzangu hawa wazungu ndio wameitengeneza ngoma ili kutumaliza na wachukue rasilimali zetu kiulaini huko mbeleni,mnategemea leo watawapa vifaa bora vya kupimia hiyo ngoma,unafikiri wao wanapenda kuona sisi tunapambana na ngoma,hawapendi basi tu wafanyeje unajua sasa naona kuna kitu lazima tufanye wabongo ili kuitoa hii serikali mana kila kukicha kuna jipya wamefanya ufiasdi kwenye madini na mambo mengine sasa wameona haitoshi wanakuja kwenye afya zetu,tena kwa gonjwa ambalo mpk sasa halina tiba lazima tutakwisha,mana najua baada ya watu kuambiwa hawana ngoma,basi wakawa wanapiga roast,au watoto wa mjini wanaita buzz kwenda buzz unafikiri hapa km majibu yalikua si sahihi si mtu mamilioni wameshapata tayari,hii serikali ina mambo mengi ya ajabu.

na mstari wa mbele, calif/usa, - 16.03.08 @ 19:57 | #2490

Tanzania inavuna mapato ya rushwa,tangu kwenye vyama vya siasa hadi uteuzi, mambo ya kujuana na kulindana.Thamani ya Mtanzania ni katika kura yake kwa ajili ya wakubwa na watoto wao.Mfano no hao watoto wa wakubwa waliojazana BoT na sehemu nyingine za wateule za kulindana mapato yake ni kuvuruga ufanisi.Tunashangaa kitu gani.Angalia kila fani ni urithi tupu, katika serikali, siasa, polisi, hospitali kila mahali, tuna haki ya kumlilia Mwalimu Nyerere.

na ngadaya, italy, - 16.03.08 @ 20:10 | #2492
 
Yaani hapa tumekwisha. Hapo ndo mtu umejinyima ngono miaka yote hadi utakapofunga ndoa, unapata mchumba mnaenda kupima mnaambiwa wote mambo safi! Mnarudia baada ya miezi 3 mnaambiwa bado mambo mswano, kumbe vipimo ni feki. Mnaoana na maisha yanaendelea, huko katikati hata mkipata shida yoyote hamuwazi UKIMWI kwa kuwa mmeambiwa "negative". Jamani tunauana bila huruma! Ufisadi umefikia kiwango hiki?

Kumbe basi ndio maana hata wale watu ambao wana wasiwasi sana kuwa huenda wanayo HIV kutokana na lifestyle yao ilivyokuwa, wanapoenda kupima wanaambiwa "NEGATIVE", hata wenyewe wanajishangaa "Negative mimi? Kweli miujiza ipo!" Kumbe masikini wamefisadiwa tu, vipimo ni feki?

Nina kisa cha kweli, huyo jamaa yangu kama anasoma hii forum atakumbuka kwa uchungu. Alikuwa na "nyumba ndogo" yake kule Chang'ombe, ikawa imeugua sana muda mrefu. Basi yule mama akamwambia jamaa anaomba akapimwe tu kama ni ukimwi ajue moja, na kwanza siku hizi kuna dawa za kupunguza makali. Akampeleka Kinondoni Hospital kwa Dr Mvungi, akapimwa pale akaambiwa "Negative". Yule mama hakuridhika, aliporuhusiwa pale akaenda Mwananyamala, akapata pia jibu hilohilo. Akatibiwa shida alizokuwa nazo kipindi hicho akarudi nyumbani. Siku moja (baada ya miezi kama 2 hivi) jamaa akanipigia simu kuwa "shemeji" anaumwa sana yuko kwa Dr Mvungi, basi nilipotoka mahangaikoni nikapitia kumuona. Alikuwa amebanwa kifua vibaya sana, walimwekea Oxygen na madaktari walisema kaishiwa damu pia. Walichukua vipimo kadhaa, na mgonjwa aliomba tena mbele yetu kuwa kipimo cha HIV kirudiwe. Tulishangaa sana, jibu likarudi kesho yake "HIV positive". Jamaa hakukubali, akauliza mbona mara ya mwisho mlisema NEGATIVE na hata Mwananyamala wakasema hivyohivyo? Yule mtaalamu alijieleza sana, akadai wametumia kipimo tofauti na awali. Tukauliza kwa nini hukutumia hicho toka mwanzo? Yaani majibu yake hayakuturidhisha kabisa, tukachukua mgonjwa wetu tukaenda Muhimbili, akalazwa kwenye ile wanaita "Fast Track". Huko jibu likawa lilelile "HIV positive" na tena wakasema CD4 zimeshuka sana, na hata ini lake na figo vilikuwa vimepungua uwezo sana, visingeweza kuhimili madawa ya ARV. Alifariki baada ya wiki moja pale Muhimbili.

Sasa leo nimesoma habari hii nikamkumbuka, nikahisi inawezekana nae alikuwa mmojawapo wa wahanga wa hivi vipimo feki. Yaani mafisadi kila kona jamani! Toba yarabi!
 
Prof. Mwakyusa now defends Capillus HIV rapid test kit

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam


THE Minister for Health and Social Welfare, Prof. David Mwakyusa, has made a U-turn regarding the controversial HIV rapid test kit Capillus, saying it will now continue being used in the country after being approved by a ministerial team of experts.

Prof. Mwakyusa, whose ministry last year announced the phasing out of the Capillus kit due to tough storage requirements, this time confidently asserted that the required cold chain storage facilities are available to transport and distribute the test kit to health centres across the country.

He was presenting over the weekend a summary of the findings of a three-man team assigned to investigate the defunct HIV rapid test algorithm crafted in 2002 and the controversy surrounding disqualification of the Cyflow CD4 counting machine after a flawed laboratory examination in 2001.

The ministerial probe team was made up of Professors Philip Hiza, Raphael Lema and Dr Juma Madati.

Prof. Mwakyusa also accused the local agents of the Cyflow machine’s German manufacturers of negligence which led to poor laboratory test results of the CD4 counting machine at the Muhimbili University for Health and Allied Sciences.

But he also noted that even the World Health Organization had voiced reservations about the machine, saying no organized or coordinated independent multi-site evaluation had been carried out on the instrument while ’’field experience has shown that Cyflow has not overcome technical challenges related to robustness of the equipment or reproducibility of results.’’

The minister also said Cyflow, which is widely used in poor countries because of its perceived effectiveness and use of cheap reagents compared to the US-made Facs Count machine, has been dismissed by WHO experts because of its functioning.

’’Furthermore, the expert group noted that the one parameter Cyflow counter may not be appropriate in monitoring TB co-infected patients,’’ he stated.

’’The decision by the government not to accept Cyflow was a result of the laboratory test results done by MUHAS, elsewhere in the world and the WHO position,’’ Prof. Mwakyusa said.

He also strongly defended the ministry’s continued utilization of Capillus, and blamed the local representatives of the rival SD Bioline HIV rapid test kit, Tega International Communications and Supplies Limited, of delaying the evaluation of their kit so that it should be allowed for use in the country.

He said even though the SD Bioline test kit was endorsed by the Private Health Laboratories Board (PHLB), this did not necessarily mean that the South Korean-made kit was automatically the winner of any government tender to supply such gadgets.

’’SD Africa was informed that registration of their kits by PHLB did not mean that it was going to be purchased by the government. Instead they were advised to contest a tender once it was announced,’’ the minister said.

A draft copy of the ministerial probe team’s report back in October 2006 had the three authors rejecting any further purchases of Capillus and Determine HIV rapid test kits, giving various reasons including non-fulfillment of any of the four conditions stipulated by the PHLB.

According to Prof. Mwakyusa, the probe team had established that some officials from the ministry, PHLB and the National Aids Control Programme had been communicating directly with SD Bioline manufacturers Standard Diagnostics Inc. of Korea without following proper official channels.

He described this as a major weakness.
 
KWA mara nyingine tena, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Profesa David Mwakyusa amewashangaza wanasayansi duniani kwa kukubali kunaswa na mtego wa mafisadi na kutangaza ripoti ya uongo kuhusu kipimo cha Capillus na mashine ya kupima chembechembe za damu (CD 4) inayojulikana kama Cyflow.
 

Attachments

  • ExecutiveSummary27.3.doc
    452.5 KB · Views: 402
  • REPORT WRITE UP24.10.06.doc
    105.5 KB · Views: 294
KWA mara nyingine tena, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Profesa David Mwakyusa amewashangaza wanasayansi duniani kwa kukubali kunaswa na mtego wa mafisadi na kutangaza ripoti ya uongo kuhusu kipimo cha Capillus na mashine ya kupima chembechembe za damu (CD 4) inayojulikana kama Cyflow.

Karibu sana JF ndugu PAMOJA

kwa hiyo ripoti ni ya Uongo!!!.............then Ukweli ni upi??
 
Nami nasema tupo pamoja ndugu pamoja so njoo barazani ukae mkekani then tupe somo
 
Sasambua yakhe si kila mmoja anaweza kuona ndani ya kapu la mwali weka vitu hadharani!....
 
KWA mara nyingine tena, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Profesa David Mwakyusa amewashangaza wanasayansi duniani kwa kukubali kunaswa na mtego wa mafisadi na kutangaza ripoti ya uongo kuhusu kipimo cha Capillus na mashine ya kupima chembechembe za damu (CD 4) inayojulikana kama Cyflow.

Sasa Pamoja si utuonyeshe uongo wenyewe basi?Mbona unaleta habari nusunusu na kutuchanganya?Lete mistari yote halafu tutachagua mchele na kukuachia pumba!
 
Wakuu someni hizo attached files nadhani ndio nia ya huyu mgeni wetu ambaye laabda ndio kwanza kajifunza kurusha mawe..
Hapa chini nitanukuu kipande cha report hiyo:-

One of the first chorus of disapproval came from the Rai weekly newspaper (see Annex 2.60.1), whose issue dated 31/08/2006 blazed a front page headline: "Corruption of MoHSW is Shaking the World–Muhimbili is Involved in This".
It quoted Dr.Roland Godhe, an International Director of Partec as having informed the scientific world and the international public at large how Partec is considering taking legal action against the Tanzanian MoHSW for the corruption that led to the banning of all the CyFlow® CD4 counting machines in Tanzania.

One of the recipients of this E-mailed information in Canada said that the MoHSW rushed unduly to ban all versions of CyFlow machines without ascertaining their unsuitability by hundreds of positive reports of the CyFlow machines available in the internet. When asked by another Rai reporter about what was now termed the "CyFlow saga", the former Minister for Health, Hon. Mrs. Anna Abdallah, M.P. she said that if the reason for banning the CyFlow machines is its imprecision when determining low CD4 count samples of < 200 cells/&#956;l (see Annex 2.60.2), when she searched the internet, she found a number of reports on the CyFlow which contradict the MUCHS findings. In effect, the MoHSW and MUCHS are telling the world that the CyFlow is a killer because it gives false test results, but the scientific world is heaping positive praises for the performance of all the CyFlow machines. She said she thought it is often prudent to seek a second opinion whenever a sharp controversy like this arises.

She also said that, she has always preferred to have more varieties of important life saving machines, so that one can fall back onto another machine provided by a different supplier in case the first machine or its supplier misbehaves.

All this prompted the Hon. Minister for Health and Social Welfare of the United Republic of Tanzania, Professor David Mwakyusa, M.P. to appoint a three man Probe Team to look into the allegations of corruption leveled against some officials of the MoHSW, as well as some researchers and technicians of the Microbiology/Immunology Department of MUCHS.

Members of the Probe Team are:
1. Prof. Philip R.Hiza, Retired Consultant Surgeon/Chief Medical Officer, Ministry of Health and Social Welfare, Dar es Salaam.Tanzania.

2. Prof. Raphael A.Lema, Retired Consultant Pathologist, currently Vice Chancellor of IMTU, Dar es Salaam. Tanzania.

3. Dr. Jumah P. Madati, Retired Chief Government Chemist, Ministry of Health and Social Welfare, Dar es Salaam. Tanzania.

The Hon. Minister for Health gave the Probe Team eight Terms of Reference, (see Annex 11.2) seven of which deal with the CyFlow saga only, and the last one deals with the SD Bioline HIV 1/2 Rapid Antibody Test Kit.
 
Wakuu someni hizo attached files nadhani ndio nia ya huyu mgeni wetu ambaye laabda ndio kwanza kajifunza kurusha mawe..
Hapa chini nitanukuu kipande cha report hiyo:-

One of the first chorus of disapproval came from the Rai weekly newspaper (see Annex 2.60.1), whose issue dated 31/08/2006 blazed a front page headline: “Corruption of MoHSW is Shaking the World–Muhimbili is Involved in This”.
It quoted Dr.Roland Godhe, an International Director of Partec as having informed the scientific world and the international public at large how Partec is considering taking legal action against the Tanzanian MoHSW for the corruption that led to the banning of all the CyFlow® CD4 counting machines in Tanzania.
One of the recipients of this E-mailed information in Canada said that the MoHSW rushed unduly to ban all versions of CyFlow machines without ascertaining their unsuitability by hundreds of positive reports of the CyFlow machines available in the internet. When asked by another Rai reporter about what was now termed the “CyFlow saga”, the former Minister for Health, Hon. Mrs. Anna Abdallah, M.P. she said that if the reason for banning the CyFlow machines is its imprecision when determining low CD4 count samples of < 200 cells/&#956;l (see Annex 2.60.2), when she searched the internet, she found a number of reports on the CyFlow which contradict the MUCHS findings. In effect, the MoHSW and MUCHS are telling the world that the CyFlow is a killer because it gives false test results, but the scientific world is heaping positive praises for the performance of all the CyFlow machines. She said she thought it is often prudent to seek a second opinion whenever a sharp controversy like this arises.
She also said that, she has always preferred to have more varieties of important life saving machines, so that one can fall back onto another machine provided by a different supplier in case the first machine or its supplier misbehaves.
All this prompted the Hon. Minister for Health and Social Welfare of the United Republic of Tanzania, Professor David Mwakyusa, M.P. to appoint a three man Probe Team to look into the allegations of corruption leveled against some officials of the MoHSW, as well as some researchers and technicians of the Microbiology/Immunology Department of MUCHS.

Members of the Probe Team are:
1. Prof. Philip R.Hiza, Retired Consultant Surgeon/Chief Medical Officer, Ministry of Health and Social Welfare, Dar es Salaam.Tanzania.

2. Prof. Raphael A.Lema, Retired Consultant Pathologist, currently Vice Chancellor of IMTU, Dar es Salaam. Tanzania.

3. Dr. Jumah P. Madati, Retired Chief Government Chemist, Ministry of Health and Social Welfare, Dar es Salaam. Tanzania.

The Hon. Minister for Health gave the Probe Team eight Terms of Reference, (see Annex 11.2) seven of which deal with the CyFlow saga only, and the last one deals with the SD Bioline HIV 1/2 Rapid Antibody Test Kit.


Mkuu Mkandara,mimi bado nashindwa kuelewa hapa.
Hapa wanasema Prof.Mwakyusa ameunda timu ya kuchunguza hiyo kashfa,je ni lini hii timu iliundwa?Na je ilishakabidhi ripoti yake?Kama ndiyo,hiyo ripoti inasemaje na iko wapi tuione kama itawezekana?Manake Pamoja anadai kuwa Mwakyusa amewashangaza wanasayansi duniani kwa kutangaza ripoti ya uongo kuhusu mashine ya kuhesabia CD4s(CyFlow),sasa tunautaka huo uongo tuuone uko wapi?Na kama kuna rushwa,wizara imechukua kutoka kwa nani?Na huyo Director wa Partec alishachukua hiyo court action against MoHSW?
 
Niliku Nafanya Maongezi Na Rafiki Yangu Mmoja Mtaliano Maongezi Ya Kawaida Tu, Basi Nikajikuta Nagusia Suala La Ukimwi Tanzania Na Namna Gani Ya Kukabiliana Nalo Basi Yule Bwana Alinionea Huruma Sana Na Akaniambia Kuanzia Sasa Hesabu Miaka Kumi Mbele Na Siyo Tanzania Pekee Bali Na Karibu Nusu Ya Waafrica Wote Wanaoishi Africa Watakuwa Wameteketea Kwa Ugonjwa Huu Mbaya Kabisa Kutokea Tangu Kuumbwa Kwa Dunia. Nilipomuuliza Ni Kwanini Akaniambia Waafrica Huwa Hawajithamini Na Haswa Wale Waliooa Na Walio Olewa Akazidi Kusema Africa Ni Rahisi Kabisa Kufanya Ngono Na Mke Au Mume Wa Mtu Kuliko Mahala Pengine Popote Duniani Na Hata Hao Wanaojiita Maboyfriend Na Na Girlfriend Asilimia Nyingi Ni Wanafiki Wa Wanagawa Uroda Kwa Yeyote Mwenye Kuhitaji Akasema Asilimia 95 Ya Waafrica Hawajiheshimu Wala Kujithamini Ktk Suala La Ngono
 
IT CAN BE DONE....PLAY YOUR PART..! MIMI NA WEWE TUANZE KUBADILIKA.........! WASWAHILI HUSEMA MOJA NDIO MWANZO WA HESABU......SASA TUMEFIKA MBILI....(isiishie kuwa maneno matupu bali kwa vitendo) TUHAKIKISHE TUNATOKOMEZA UKIMWI KAMA KINA KAWAW,T.KOMBO NA WENGINEO WALIVYOTOKOMEZA UKOLONI....!
 
Hata mimi binafsi nilikuwa nazungumza na Daktari mmoja kutoka nje na liweza kusema kwa hali ya maisha tunayoishi hapa Tanzania ni vigumu kuzuwia ukimwi lakini haitoshi kukaa kimnya nilipo muuliza yeye binafsi nini kilichomfanya awe na wazo hilo alijibu kuwa Tanzania imejikuta katika mahali pabaja na katika wakati mbaya na hii imetokana na sisi watanzania wa kisasa kuiga mazingira ya kufanya Ngono yanayotumika katika nchi ya za west na pia utakuta mtu mmoja hapa Tanzania amekuwa na wasichana zaidi ya watano au msichana anakuwa na wavulana zaidi ya hao watano akasema imagine mmmoja kati yao amekuwa na maradhi sasa ukiweka hesabu utagunduwa hiyo inakuwa kama mnyororo umeungana na uazidi kunganisha wengi nihatari sana tena sana na hii imechangia wakati pale Aids imeanza kuingia Tz na viongozi wa kakata kudhibiti ile hali kwa wakati ule sasa na hili litakuwa hivyo hivyo na wakati utatueleza
 
Mkuu Mkandara,mimi bado nashindwa kuelewa hapa.
Hapa wanasema Prof.Mwakyusa ameunda timu ya kuchunguza hiyo kashfa,je ni lini hii timu iliundwa?Na je ilishakabidhi ripoti yake?Kama ndiyo,hiyo ripoti inasemaje na iko wapi tuione kama itawezekana?Manake Pamoja anadai kuwa Mwakyusa amewashangaza wanasayansi duniani kwa kutangaza ripoti ya uongo kuhusu mashine ya kuhesabia CD4s(CyFlow),sasa tunautaka huo uongo tuuone uko wapi?Na kama kuna rushwa,wizara imechukua kutoka kwa nani?Na huyo Director wa Partec alishachukua hiyo court action against MoHSW?

Mtarajiwa ufisadi upo karibu sehemu zote za serikari na wizara ya Afya ninavyofahamu ilishaoza siku nyingi tu, nakumbuka ufisadi kama huu aliufanya katibu Mkuu mmoja hapo wizarani siku za nyuma "ndugu na BWM na mbunge" hii kama sikosei ilihusu madawa na ilisababisha maofisa fulani kubadilishwa kazi kwa uonevu baada ya kubumburusha dili la mkubwa na baadhi yao walitolewa Muhimbili na kuwa desk officer pale wizarani, iliienda mpaka Ofisi ya Rais BMW baada ya Wakurugenzi fulani wizarani kuvalia njuga including other scandals ndipo mkuu akamtoa jamaa yake huyo na kuumpenyeza katibu mkuu mwingine ambaye pia ni ndugu
(Zaramo iko iba Kwere ficha)
Hebu soma hii http://www.jamboforums.com/attachment.php?attachmentid=1354&d=1206705423
 
While the concern is real and undisputable,I refuse to swallow the gross mischaracterization and condescending disguised racism.

If Africa will perish by AIDS, it will not be because Africans are more promiscuous than Europeans or North Americans froe example, it will be because of the following.

1.AIDS started in the jungles of Africa (at least if you do not buy the CIA conspiracy theory) and had much time to infect the population of Africa before anybody realized it was in our midst.There are cases of documented HIV/AIDS from as early as the 1950's

2.Africans cannot afford the type of health care to combat AIDS. Most HIV positive people do not know their status because they do no annual checkups and therefore live with HIV as carriers and end up unknowingly infecting others.

3.In a continent plagued with so many problems, many people take the "whatever will be will be" approach, with meagre resources and a bleek future in most cases, people have little to perservere for.I believe this is what the Italian is taking to mean "people do not value their lives"

4. Promiscuity.It is true there are problems.But when you put these problems in context Africans are no more promiscuous than other people, at least there is nothing scientifically sound to demonstrate this.

So yes, we may be slowly approaching "extinction level event" but this may sadly be more of a Malthusian economic check than because Africans are promiscuous.There is an innate Darwinism in evolution and Africa being the weakest continent may find itself facing all sorts of perils of catastrophic proportions,AIDS being one of the most immediate concerns.
 
Mtarajiwa ufisadi upo karibu sehemu zote za serikari na wizara ya Afya ninavyofahamu ilishaoza siku nyingi tu, nakumbuka ufisadi kama huu aliufanya katibu Mkuu mmoja hapo wizarani siku za nyuma "ndugu na BWM na mbunge" hii kama sikosei ilihusu madawa na ilisababisha maofisa fulani kubadilishwa kazi kwa uonevu baada ya kubumburusha dili la mkubwa na baadhi yao walitolewa Muhimbili na kuwa desk officer pale wizarani, iliienda mpaka Ofisi ya Rais BMW baada ya Wakurugenzi fulani wizarani kuvalia njuga including other scandals ndipo mkuu akamtoa jamaa yake huyo na kuumpenyeza katibu mkuu mwingine ambaye pia ni ndugu
(Zaramo iko iba Kwere ficha)
Hebu soma hii http://www.jamboforums.com/attachment.php?attachmentid=1354&d=1206705423


Nimekupata Kite,ngoja nijitahidi kusoma mpaka mwisho!
 
Back
Top Bottom