Kama kila post nzuri mambo yake ndio haya .....ni wazi kuwa competent individuals hawataomba hizi kazi na matokeo yake ndio watoto wa vigogo, wajukuu, na washirika wao wataendelea kutesa tu.
Nina sikikia sikia kuwa TTCL watu wa serikali wanafikiria kumpa jamaa anayeact kwa sasa ingawa kwenye interview hakuwa the best candidate. Au tunaweza kusikia kama haya tunayosikia hapa kuhusu NHC.
Swali: hivi hii NHC inajenga nyumba? Kama inajenga mara ya mwisho kujenga hizo nyumba ilikuwa lini na wapi na zinagharimu kiasi gani?
mmmmmm!!!!!!!!!!!! Maumivu ya kichwa huanza polepole!!!!!!!!!!!!!!
Bongo usawa huu by the time unasema ngoja tumpe benefit of doubt, ukifunga macho ukifungua ushapigwa bonge la bao, EPA jingine.
Mwaka wa uchaguzi huu, wenyewe ukiongea nao wanakwambia "kuna maswala nyeti ya logistics"
Hii kashfa ya kuhusishwa na EPA ni nzito sana.
hamkawii kusikia world bank/habitat wamesimamisha utoaji wa pesa zao mpaka apatikane mtu mwadilifu au mpaka wawaleteeni toka Ghana kama walivyo fanya Tanroads. mbona kuna watanzania wengi tu wenye qualifications na waadilifu, kuna Dr Assad pale university anaweza kupewa kama mnazungumzia head hunting, ikawa testing ground au kumpa exposure zaidi kabla ya kupewa madaraka makubwa zaidi kama bandari, tra nk . na hata hao ma-engineer, wasanifu majengo na blah blah kibao
sasa mmeona ile BODI mpya ya NHC ilivyo? yule mmbunge anafanya nini au ndio kusema wale jamaa wa Chiligati hawakuona ule mwongozo kuhusu wabunge na wanasiasa kuwa members wa bodi za mashirika ya Umma?
Just putting record clear!!! Wabunge hawaruhusiwi kuwa WENYEVITI WA BOARD. sio wajumbe wa Board...
1.Nehemia HAKUOMBA kazi hii kama ambayo sheria ilitaka afanye
2. Nehemia hakuitwa kwenye USAILI kama ambavyo sheria ilitaka ifuatwe
3. Nehemia kamapata kwa sababu ya presha na ufisadi wa hali ya juu uliyofanywa na Katibu Mkuu wa Ikulu bwana LUHANJO
4. Ambao walioomba na wakaitwa kwenye usaili hawajaandikiwa barua ni sababu zipi walikosa halafu kazi akaewa ambaye hakuomba hiyo kazi in the first place.
If anything hata kama Luhanjo alikuwa anamtaka kijana wake what was so difficult or worong UTARATIBU ukafuatwa?
Usitutoe kwenye hoja pls. Ishu si DINI hapa. Tunahitaji kufaham kama sheria na taratibu zilizoweka zilifuatwa. Kama zilifuatwa hatuna tatizo. Huna haja ya kukurupuka. Juzi hapa aliteuliwa balozi wa Malawi, watu wakamponda sana in the end ikatolewa qualification yake. Watu wakapotea. Watu hawakugusa dini. Hiyo ya majaji tunapenda uianzishie thread maana yaelekea una utafiti wa kutosha then tuijadili. Ngoja watu waseme.Huyo uliyemtaja hapo juu atatuletea mambo ya UDINI hivyo vyeo walivyompa jamaa zake vinamtosha!! Moja ya sababu jamaa wanalalamika ni kwasababu walitegemea kuwa atateuliwa mtu wa imani yao kwani sio siri kuwa awamu hii ajenda yake ni kutafuta kwanza watu wa imani ya mkulu ndio wajaze hizo nafasi kama hawapatikani basi ndio wateuliwe wengine; mfano ni kule kwenye uteuzi wa majaji nendeni mkafanye utafiti halafu mje mnisute!!!! G.T . welcome back na pole sana next time if you will be lucky hata hivyo NSSF haiwatoshi?!!
Let me be the devil's advocate..
Kuna ushahidi wowote kwamba hakuomba kazi; je akisema kuwa aliomba tunaweza kuthibitisha vinginevyo?
[/SIZE]
NI sawa na swali la hapo juu, je akithibitisha kuwa aliitwa au watu wa usaili kwenda kwake kumsaili.
Katibu Mkuu kiongozi ana jukumu la kuangalia pia appointments za Rais au watendaji ambao wako chini ya Rais kutokana na nafasi zao za kuteuliwa. Katibu Mkuu anayo haki na wajibu wa kufuatailia teuzi mbalimbali na watumishi mbalimbali. Kwanini hilo ni makosa?
Kama hili ni kweli wale ambao wanajua kuwa hawakupewa nafasi hiyo walete malalamiko wazi (kama alivyofanya Mbilinyi na Zinduka). Waseme kuwa kuna upendeleo umefanyika na ikibidi wafungue kesi mahakamani kama haki iko upande wao. Haitoshi kutujuza kuwa wamedhulumiwa.
How much leeway hizo taratibu zinatoa kwa Katibu Mkuu kiongozi?