Godfrey Malisa: Kwa nini nilipinga uteuzi wa Samia CCM

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
260
Reaction score
998
MALISA JF.png

Mwanazuoni, mwandishi wa vitabu na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Godfrey Malisa, anasema msimamo wake wa kuhoji uteuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea urais wa chama hicho Januari 2025 ulitokana na kile anachodai kuwa ni ukiukwaji wa Katiba ya CCM na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika mahojiano haya, Malisa anazungumzia chanzo cha mgogoro wake na baadhi ya viongozi wa CCM, madai yake kuhusu kufukuzwa uanachama, hatua ya kwenda mahakamani kupinga uteuzi huo na kesi ya uhaini iliyomuweka gerezani kwa miezi sita kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Swali: Naomba kupata wasifu wako.

Jibu:
Nilizaliwa, nikakulia na kusoma Moshi, mkoani Kilimanjaro. Baadaye nilikwenda nje ya nchi ambako nimeishi kwa miaka mingi. Hata elimu yangu ya uzamifu nimeipata nikiwa nje ya nchi.

Swali: Uliishi nchi gani?

Jibu:
Nimeishi katika nchi nyingi, zikiwemo Japan, nchi za Ulaya na Marekani, ambako ndiko nilikoishi kwa miaka mingi.

Swali: Ulisomea nini nje ya nchi?

Jibu:
Nilisomea falsafa na theolojia. Pia mimi ni mwandishi wa vitabu.

Swali: Kuhusu uchungaji, ulikuwa mchungaji wa kanisa gani? Ulikuwa na usharika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)?

Jibu:
Hapana. Nimekuwa mwalimu wa wachungaji katika chuo cha kanisa.

Swali: Uliingia lini kwenye siasa, na umewahi kushika nyadhifa zozote za kisiasa?

Jibu:
Sijawahi kuingia kwenye siasa wala kushika nyadhifa zozote za kisiasa, kwa sababu mimi si mwanasiasa. Kuwa kada wa CCM hakunifanyi kuwa mwanasiasa zaidi ya kuwa mwanachama wa chama hicho. Sijawahi kushika nafasi yoyote ya uongozi wa kisiasa.

Swali: Ingawa watu wengi wanakufahamu, jina lako lilijulikana zaidi mwaka jana ulipoanza kuhoji uteuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika vikao vya CCM vya Januari 19, 2025. Hatua hiyo ilisababisha mgogoro hadi kutangazwa kuwa umefukuzwa uanachama, ingawa baadaye ulisema bado unatambuliwa kama mwanachama. Nini kilitokea?

Jibu:
Januari 19, 2025, katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM, chama kilikiuka Katiba yake, hususan Ibara za 102 na 104, pamoja na Ibara ya 38(1) na (2)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kumtangaza Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea urais wa CCM.

Hilo ndilo lililonifanya nitoe kauli. Niliamua kuzungumza kwa nia njema kabisa, nikisema kwamba tumekosea na tunapaswa kurudi kwenye utaratibu wa kikatiba. Wakati ukifika, tufuate Katiba. Tutampitisha Samia; hakuna namna ambayo tutazuia asipite. Lakini ni muhimu kufuata utaratibu.

Tatizo ni kwamba baadhi ya viongozi hawapendi kukosolewa, hata wanapokosea. Wanachotaka ni kuwapigia makofi na kuendelea mbele. Mimi nikasema hapana, siwezi kufanya hivyo. Niliona chama kimekosea na nikaamua kusema ukweli.

CCM ni chama kikubwa ambacho kinapaswa kuvumilia misimamo tofauti ya wanachama wake. Hata hivyo, haikuwa hivyo. Waliona ninakidhalilisha chama na kwenda kinyume na msimamo wake.

Nikajiuliza, ninawezaje kwenda kinyume na chama wakati, kwa mtazamo wangu, ni viongozi wachache ndio waliokuwa wanaenda kinyume na Katiba? Hawa si chama kizima, bali ni baadhi ya viongozi walioko juu.

Kwa hiyo, nilipinga uamuzi huo kwa nguvu zote kupitia vyombo vya habari. Hawakupendezwa na hatua yangu kwa sababu haikuwa kawaida kwa mwanachama wa CCM kupinga uamuzi wa Mkutano Mkuu, hata kama anaamini kuwa uamuzi huo umekiuka Katiba. Ndipo tatizo lilipoanzia.

Swali: Ni nini kilichokupa ujasiri wa kusimama dhidi ya chama kikubwa kama CCM?

Jibu:
Mimi nina nguvu sana. Hujawahi kuniona wala kukutana nami? Nina nguvu sana. Mtu mmoja kama mimi anaweza kukisimamisha CCM. Nakwambia!

Swali: Ulifanikiwa?

Jibu:
Sana, sana.

Swali: Lakini hawakutengua uamuzi wao.

Jibu:
Unajua, unapomwambia mtu mzima kwamba zipu ya suruali yake iko wazi, hawezi kuifunga hapo hapo mbele yako. Anaweza kugeuka, akaenda mahali na kuifunga.

Kwa hiyo, ninajua kilichotokea baada ya mimi kuzungumza. Ninajua mambo yaliyotokea ndani ya chama, ndiyo maana nasema kauli yangu ilikuwa na athari kubwa.

Swali: Hebu tufunulie kidogo kilichotokea ndani ya chama baada ya ukosoaji wako.

Jibu:
Hapana, hapana, samahani.

Swali: Turudi kwenye suala la kutangazwa kuwa umefukuzwa uanachama wa CCM. Nini kilitokea?

Jibu:
Hicho kilikuwa kikundi cha watu ambao walitaka kujipendekeza kwa viongozi. Ni watu ninaowaita machawa wa hapa Mkoa wa Kilimanjaro. Walidhani wakifanya hivyo wataonekana kuwa ni wapambanaji wa chama na kwamba wamemdhibiti mtu anayetoka katika eneo lao.

Lakini walikiuka Katiba na taratibu za kumsimamisha mwanachama na kumfukuza uanachama. Walifanya kinyume na utaratibu, na hilo lilikuwa jambo la aibu.

Swali: Je, ulichukua hatua ya kupigania uanachama wako?

Jibu:
Siwezi kupigania kitu ambacho sijapoteza. Napigania nini? Mimi bado ni mwanachama. Hata ukienda Makao Makuu ya CCM Dodoma, natambuliwa kuwa mwanachama. Ninayo kadi yangu, nimelipia na kila kitu kiko sawa.

Swali: Kwa hiyo, lile tangazo la kufukuzwa kwako lilitenguliwa?

Jibu:
Lile tangazo la watu hao halina haja ya kuhangaikiwa. Unatengua kitu gani? Kama uamuzi ungekuwa umetolewa rasmi, kama ilivyokuwa kwa Emmanuel Nchimbi, na kutangazwa kwa utaratibu, hapo tungezungumzia suala tofauti.

Lakini siwezi kuhangaika na tangazo lililotolewa na watu wachache ambao, kwa mtazamo wangu, hawakufuata utaratibu.

Swali: Tuizungumzie hatua yako ya kwenda mahakamani kupinga uteuzi wa Rais Samia. Nini kilikufanya uchukue hatua hiyo?

Jibu:
Nilienda Mahakama Kuu, Masjala ya Dodoma, baada ya kuzungumza na viongozi wa CCM. Awali tulikuwa na kikao kirefu kuhusu suala la kukiuka Katiba. Tulijadiliana, lakini kila upande ulibaki na msimamo wake. Wao waliona wako sahihi na mimi niliona niko sahihi.

Nikawaambia, kama hatuwezi kukubaliana, basi nitakwenda mahakamani ili iamue nani yuko sahihi kati yetu.

Kwa hiyo, nilienda Mahakama Kuu Dodoma kufungua shauri la kupinga uteuzi huo na kuomba utenguliwe. Hata hivyo, kwa maoni yangu, mahakama ilifanya makosa ya kisheria kwa kuingia katika masuala ya kiufundi badala ya kusikiliza kiini cha shauri.

Kesi ikatupiliwa mbali bila kusikilizwa kwa msingi wake. Sisi tumekata rufaa na sasa tunasubiri kuambiwa lini itasikilizwa.

Swali: Mbali na kesi hiyo ya kupinga uteuzi ndani ya chama, ulifunguliwa pia kesi ya uhaini na kesi ya makosa ya mtandao, Desemba 2025. Nini kilitokea?
Soma pia: Aliyekosoa mchakato wa uteuzi wa Samia ndani ya CCM, Mzee Godfrey Malisa ashtakiwa kwa uhaini

Jibu:
Nchi hii imefika mahali ambapo watu wameingiwa na hofu kiasi kwamba hawawezi kuthubutu kuikosoa Serikali yao. Watu wengi wananiona kama mtu wa ajabu na wamekuwa wakinikwepa.

Hata watu ambao nilikuwa nao karibu sana, wakiniona, wanaweza kugeuka na kuondoka kana kwamba walikuwa wanaenda mahali pengine. Wanaogopa kuhusishwa na mimi.

Sababu ni kwamba nilisimama na kusema mauaji yaliyotokea hayakuwa sahihi, waliohusika wanapaswa kuwajibishwa na kwamba kunapaswa kuundwa Serikali ya mpito, pamoja na mambo mengine. Nilikuwa mkali sana katika misimamo yangu.

Mwisho wa siku, waliona ninawasumbua na wakaamua nikamatwe.

Nilikuja kukamatwa na askari zaidi ya 20 wakiwa na bunduki. Nilikuwa tayari nimepata taarifa kwamba wangekuja kunikamata, lakini sikuamua kukimbia. Nilikamatwa na kukaa gerezani kwa miezi sita, baadaye wakaachiliwa kuniruhusu kutoka.

Swali: Kesi hiyo ilifutwaje?

Jibu:
Unamshtaki mtu kwa kosa ambalo hakulitenda, utaenda kueleza nini mahakamani? Kwa mtazamo wangu, kesi hiyo ilitumika kunidhibiti ili nibaki gerezani na nisiweze kuzungumza hadharani.

Kesi ya uhaini haina dhamana, kwa hiyo niliona walikuwa wanaitumia kama njia ya kunifungia mahali ambapo nisingeweza kuendelea kutoa kauli zangu. Wangeweza kutumia kesi gani nyingine kunidhibiti kama si hiyo isiyo na dhamana?

Soma pia: Aliyesema Rais Samia ajiuzulu kabla ya Disemba 9, Dkt. Malisa aachiliwa huru, Mahakama yamfutia kesi ya Uhaini

Swali: Kwa kiasi fulani, walifanikiwa kukudhibiti. Je, sasa umekuwa mpole?

Jibu:
Nilipokuwa gerezani haimaanishi kwamba nilizuiwa kuzungumza. Nilikuwa nikifika mahakamani na waandishi wa habari walikuwepo. Nilikuwa na nafasi ya kuzungumza nao.

Nilizungumza mara moja au mbili na kusababisha mjadala mkubwa nchini. Siku moja nilizungumza na waandishi wa habari mahakamani na kauli yangu ikaleta taharuki kubwa.

Baadaye nikaona ni busara kutumia hekima. Mtu ambaye ameshika mpini, huwezi kupambana naye kwa namna yoyote bila kufikiria matokeo. Kwa hiyo, niliamua kukaa kimya kwa muda. Haimaanishi kwamba walifanikiwa kuninyamazisha.

Nilipotoka gerezani, niliitisha mkutano na waandishi wa habari na kuzungumza kwa kina. Kwa hiyo, si kweli kwamba nilitoka gerezani na kuamua kutosema tena.

Hata hivyo, kukaa gerezani kwa miezi sita si jambo dogo. Ni kipindi kigumu sana. Nilikuwa nikiliwa na kunguni kila siku. Nililalamika, wakaja kupuliza dawa, lakini baada ya wiki mbili au tatu kunguni walirudi tena.

Niliporudi nyumbani, nilichukua muda mrefu kwa makusudi kupumzika kimwili na kisaikolojia ili kupona kutokana na adha niliyopitia. Hiyo ndiyo sababu kubwa ya kukaa kwangu kimya kwa muda.

Swali: Umetulia kwa kipindi fulani, huku ukisema bado unasubiri rufaa ya kesi ya kupinga uteuzi wa Rais Samia. Nini kinafuata katika mapambano yako? Utasubiri kesi hiyo pekee au utaendelea kutoa matamko?

Jibu:
Mimi sitoi matamko kwa sababu tu ya kutaka kuzungumza. Ndiyo maana utaona kwamba kumekuwa na matukio mbalimbali ambayo yametokea, lakini nikakaa kimya. Watu wakaanza kuuliza, kwa nini mzee Malisa amekaa kimya? Kwa nini hataki kuzungumzia matukio makubwa yanayotokea nchini?

Mimi si kipaza sauti cha kutangaza kila jambo linalotokea. Nazungumza pale ninapokuwa na sababu na hoja za msingi. Lazima niwe na sababu ya kuzungumza au kunyamaza.

Kwa mfano, Nchimbi alipokamatwa, sikutoa kauli yoyote, licha ya kwamba alikuwa rafiki yangu. Kuna mambo mengine mengi yametokea lakini sijazungumza.

Nataka kauli yangu ichochee mabadiliko au iwafanye watu wafikirie upya. Sitaki kuzungumza kwa ajili ya kuzungumza tu.

Swali: Mbali na masuala ya kisiasa, unaendelea na shughuli gani kwa sasa?

Jibu:
Ninafundisha na ninaandika vitabu. Hivi karibuni nimetoa vitabu viwili. Kimoja kinaitwa Understanding Philosophy na kingine African: The Tragedy of Africa.

Vitabu hivyo vinapatikana madukani na mtandaoni, ambako pia vinanunuliwa kwa wingi zaidi.
 
Upotoshaji wa namna hii CCM iuseme kwa nguvu kubwa ili kuudhibiti.

Kitendo Cha mtu mmoja kusema kakishinda CCM ni hatari kwa CCM maana CCM ni mfumo tena ni mfumo imara inakuwaje, mfumo wenye nguvu ukashindwa na mtu mmoja?

Mkutano Mkuu ni chombo Cha juu kabisa Cha maamuzi ndani ya CCM na maamuzi yanayokubaliwa na kuthibitishwa au kupitisha na Mkutano Mkuu Taifa hakuna chombo kingine chenye mamlaka ya kutangua au kubatilisha. Kwa kusema hili niseme kuwa uamuzi uliofanywa wa kumpendekeza na kumteua Samia kuwa mgombea ulikuwa ni sahihi.

Uamuzi huo unatakiwa kubatilishwa na mkutano Mkuu lakini kwa kuwa mpaka sasa mkutano Mkuu haujabatilisha ,niseme hakuna kosa lililofanyika.
 
View attachment 3691162

hawa ndio Chaga pipo ninaowajua. Ameishi ughaibuni penye raha zote. ila akakubali kuja kuliwa na kunguni gerezani kwa kosa lisilokuwepo kuuonyesha upumbavu wa waTanganyika
 
Back
Top Bottom